Jk na awamu ya pili...

Mkandara

JF-Expert Member
Mar 3, 2006
15,772
8,955
Maadam uchaguzi umekwisha na rais wetu Mh. Jakaya Mrisho Kikwete ameshakabidhiwa mamlaka ya kuiongoza nchi yetu nadhani huu ni wakati muafaka wa kuzungumzia kero za wananchi -Mnataka JK afanye nini? au. Kifanyike kipi na serikali iliyoingia madarakani ili kuijenga nchi yetu toka hapa tulipo kwani kuendelea kulalalamika haiwezi kusaidia kitu bali kuongezea machungu. Na kwa Unafiki wetu hatuwezi hata kushirikiana na kukubaliana kwa jambo lolote muhimu linalohusu mustakabali wa nchi yetu.. Hivyo ni bora zaidi tugange yajayo maanake imeshakuwa uchawi mtupu.

1. Baraza la Mawaziri.
JK anatakiwa kupunguza baraza hilo na kuwa na wizara chache iwezekanavyo na kama yawezekana arudishe upya wizara tulokuwa nazo enzi ya Mwinyi na mamlaka ya kimaendeleo yashikwe zaidi na Hamalshauri husika.

2. Kuondoa viti vya Wakuu wa mikoa na Wilaya ambao kusema kweli kwa muda mrefu wamekuwa mzigo kwa serikali kwa sababu hawa watu hawana makazi zaidi ya kuzunguka nchi nzima. Hivyo hushindwa kuendeleza sehemu moja wakijua kesho watahamishwa tena kwenda sehemu nyingine wakati makazi yao haswa ni mikoa wasiyoiongoza. Ujamaa ilikwisha zikwa na wakuu hawa sehemu hizi sii kwao, why should they care? - Kama wakuu wa mikoa na wilaya wataendelea kuwepo basi iwe ni wakazi wa sehemu hizo na cheo hiki wakishike kwa jumla ya miaka minne ya uchaguzi kumwakilisha rais aliyepo madarakani.

3.Uchumi.
Ili kukuza uchumi wetu ni muhimu kwa Kikwete kufahamukwamba tanzania ni nchi maskini na haiwezi kuondoka ktk umaskini kwa kuomba. Hata siku moja nchi ombaomba haiwezi kuondokana na kilema hicho maadam hiyo mikopo ndiyo imekuwa source of income kwa Taifa. Hivyo ni muhimu sana kwa uojgozi wake kutumia vema mikopo na misaada inayopatikana hasa ktk sekta za Miundombinu ambayo haihitaji usanii wa kuwapa wazalendo uwezo mkubwa ktk ujenzi wa vitu hivi. Ufisadi mkubwa umefanyika na fedha nyingi tumepoteza wakati miundombinu yetu imebakia kuwa hafifu na isiweza kukimu mahitaji yetu.

Nguvu kubwa iongezwe ktk Kilimo kwa mfano n vizuri sana kwa rais wetu kufanya ziara nchi za Pakistan au India ili kupata mbegu asili za mpunga aina ya Pishori (Bismati) na nchi kama Thailand ili kupata mbegu za aina ya Jasmine (mchele wa Mbeya). Jitihada kubwa iongezwe ktk kupata soko la kilimo cha Kahawa kwa kushirikiana na mashirika makubwa duniani ambayo ndiyo wanunuzi na wasambazaji wa kahawa dunia nzima. Kilimo cha asili kama mahindi, mihogo, ndizi, na matunda pia kipewe kipaumbele zaidi kwa kutafuta masoko hata nchi za jirani (Freetrade) kwani Unguja ni moja ya nchi zinazosifika duniani kwa uzalishaji wa matunda lakini sifa hizo zimeishia visiwani hazina soko hata Tanzania Bara na hakuna sababu zaidi ya ukiritimba wa sheria na taratibu kinzani ya utandawazi. Na mwisho, rasilimali watu na maliasili zetu ni lazima zitumike kwa manufaa ya nchi yetu kwani ni aibu kubwa sana kuona Mkenya au Mganda akija nchini na kuchukua ajira za wananchi kwa sababu tu ya lugha ya kigeni.

Sheria ya madini lazima ianze kazi yake kama alivyoahidi, wawekezaji wote ni lazima walipe kodi kwani ndivyo alivyowaahidi wananchi ifikapo mwaka 2010 mashirika yote ya madini yatatakiwa kulipa corporate tax. Na hakuna tena mashirika kuuzwa baada ya miaka mitano ya msamaha, wakishindwa kulipa yachukuliwe (Taifishwa) na accounts zao kuwa freezed.

4. Elimu na Afya
Ni wakati mzuri kwa rais kutazama upya wizara hizi hasa ktk maswala ya wahudumu wake. Walimu na Madaktari wapewe mishahara mizuri zaidi ili kuwawezesha kuishi pasipo kutegemea kazi ya pili..Marufuku kwa mwalimu au Daktari kufanya kazi au kufungua shughuli yoyote inayohusiana na ajira alopewa na serikali. Maadam chama kinaamini kwamba elimu na Afya bure HAIWERZEKANI basi ni bora kupitia upya gharama hizo kwa wanafunzi wa shule za sekondari kufikia kidato cha sita.

Kutokana na upungufu wa walimu ningependekeza sana kila mwalimu mmoja awezeshwe kufundisha zaidi na masomo manne au matano tofauti, hivyo kila shule hailihitaji walimu wengi na tofauti kufundhisha masomo tofauti. Hapa Canada ndivyo wenzetu wanavyofanya utakuta shule ina waalimu wachache lakini wana uwezo mubwa wa kufundisha masomo tofauti..Bila shaka kama walimu watakuwa Graduates wanaolipwa mishahara mizuri,mbinu hii inawezekana kabisa kutumiwa kuliko kuendelea kutumia walimu wa UPE kuzailisha zaidi (quantity) wakati tunaua elimu yenyewe.

5. UFISADI...
Hili ni kubwa kuliko uwezo wa Kikwete mwenyewe lakini bado anaweza kupunguza Ufisadi kwani nina imani kubwa kwamba itahitaji utawala mpya na tofauti kabisa kuweza kuua Ufisadi nchini kwani ndio wanaotawala nguzo zote za kiuchimi na sheria. Hata hivyo, ahadi yake ya kuondoa kofia mbili kwa viongozi wa serikali ni lazima aitekeleze kwani nina mashaka sana kama baraza hili la mawaziri halitakuwa na wafanya biashara. Sidhani kama sheria hii itatumika ktk uchaguzi wa baraza hili la mawaziri maadam Azimio la Zanzibar bado linatumika, hivyo, sidhani kama itatokea kinyume....

Lakini pia zipo sehemu nyeti sana ambazo anatakiwa kuzitazama upya. Uongozi ktk mashirika kama Bandari, TRA pamoja na mashirika mengine ambayo bado yameshikiriwa na serikali kuu, Sheria za Imports taxation, Utaratibu wa kulipisha kodi baada ya mauzo na sii kukadiria, kuboresha njia za mikopo ktk Uwekezaji wa viwanda na biashara ndogo ndogo, kuthibiti matumizi ya Dollar dhidi ya Tsh. Vibali na liseni za biashara, ufanisi ktk ukusanyaji wa ushuru kulazimu kila Mtanzania kuwa na namba ya kulipia Tax hata kama hana kipato. Mbali na kuthibiti tax, hii itasaidia zaidi ktk utoaji wa vitambulisho vya uraia na hata kurahisisha kupata idadi ya wakazi nchini (sensor).

KATIBA... huko wala siwezi kusema zaidi...

Kwa leo wakuu zangu natanguliza hayo machache nadhani wengine mnaweza changia zaidi au hata kunisahihisha pale nilipokosea ama kutokubaliana..Tupo hapa kujifunza.
 
Mkandara;

Heshma nyingi Mkuu!!

Nimevutiwa zaidi na Kipengele cha ufisadi!!

Kwani Ukiwa na chatu 80 ndani ya chumba cha kulala na ukafanikiwa kuwapunguza hadi 61 ni mafanikio na tunamtakia kila la gheri awapunguze chatu wawe 0 kwani tunataka watoto waingie wakalale ndani ya chumba hicho chenye nyoka ..yaani mafisadi...wa uchaguzi wa mwaka 2005 kura kwa 80% na kuwapunguza na kuwa 61%...wa sasa...Mtukufu Rais ...chumba hakilaliki bado!!. Lakini Mkandara kasema sasa tuwe kitu kimoja... na hilo ni jambo muhimu!!
 
Hana jipya, balaza la mawaziri halitakuwa na tofauti na lile lilopita, labda ataongeza mafisadi
 
Mawazo mazuri Mkandara, ila wasi wasi wangu ni kuwa kiongozi wetu hana upeo huo wa fikra. Kwa kweli ilishangaza ulimwengu mzima wakati alipoingia na kuteua Mawaziri 60 kwa nchi kama Tanzania ambayo zaidi ya asilimia 50 ya bajeti yategemea mikopo. Utasema hiyo ni akili?
Sina hata imani kama ataweza kubadili lolote la maana katika kipindi hiki, kwani la muhimu kwake hivi sasa ni kulipa mabilioni aliyokopeshwa katika uchaguzi.
Kitu kidogo tu namwomba: awaondoe Wachina wachuuzaji...hata hili pia gumu? Kwa nini hatuwezi kusema biashara za uchuuzaji ziwe za wazawa tu? Watanzania wangapi wanachuuza Beijing? Kha, Mwafrika sijui kama ana akili! Kuna mzungu mmoja alisema ' jambo litakalomfurahisha zaidi pindi atakapokufa ni kumwomba Mungu ampasulie kichwa cha Mwafrika mmoja atazame ameweka nini ndani yake'
Hata mimi pia!
 
Mkuu Mkandara tatizo kubwa la JK na viongozi wa Africa kiujumla ni "THEY DON'T LISTEN". Ushauri uliotoa ni mzuri sana lakini hata ukifikishwa kunakohusika, they can simply say hiyo haipo kwenye ilani yetu. Lakini enwayz hii isituzuie kuwapa ushauri whenever possible. Mimi msisitizo wangu zaidi kwenye elimu, yaani hapo tunahitaji ikiwezekana hata kutangaza hali ya hatari. The situation is really pathetic.

Tunahitaji kucombine quantity and quality, pia kuwe na incetives kwa walimu mfano bili za maji na umeme walipe nusu. Kuwe say na housing schemes kwa walimu, maabara bora na Library za kisasa (Audio books zianze pia kutumika).
 
Deni l;a Taifa, Deni la Taifa, Deni la Taifa, Deni la Taifa, Deni la Taifa!

Kupunguza na Kubana Matumizi, Kupunguza na Kubana Matumizi, Kupunguza na Kubana Matumizi!

Kuongeza Mapato ya Nchi, Kuongeza Mapao ya Nchi, Kuongeza Mapato ya Nchi!
 
Mkandara, mawazo/ushauri mzuri sana.

Tatizo ni uadilifu na umimi. Hivi unategemea nini kama mtu anautafuta ubunge kwa kutumia gharama ya TSh. milioni 300 hadi 500 katika kampeni???? Kwanza wanatoa wapi pesa nyingi namna hii??

Mtu wa namna hii anapopewa uongozi kazi kubwa inakuwa nikurudisha hizo pesa zote na apate na ziada. No wonder wengi wanakimbilia ubunge.
Hivi kweli wanawezaga vipi kurudisha hizo pesa? au ndo mtindo wa kuchomoa kidogokidogo kwenye project za maendeleo ya wananchi?
 
Ameonyesha kuwa hanazo sifa za kutekeleza vitu kama hivyo. He has neither the intellect nor the initiative and energy of a true leader, rather he happens to be as weak as my 3-months old baby daughter plus the fact that his hands are tied. What a freak!
 
Wakuu zangu nimewasikia lakini tutafanya nini ikiwa tayari JK ndio rais wetu?..Mimi nadhani atajifunza kutokana na makosa na sidhani kama wananchi waliomchagua wanafahamu fika hali halisi na itakapo fika hata wao wakapoteza imani zao na kuacha ushabiki basi CCM itakufa mikononi mwa JK jambo ambalo sidhani kama wapo tayari kulishuhudia.

Wakuu zangu nina wasiwasi mkubwa sana kwa Tanzania ya kesho ikiwa hali hii itaendelea kwani sisi sote sii wanaChadema wala CCM ila ni Watanzania na lolote litakalo tokea litakuwa na maafa kwetu sote pasipo kuchagua mtu au chama. Na hakuna kitu kibaya zaidi kama kukata tamaa mapema wakati uwezekano upo. Wapo Wana JF waliokuwa karibu na kina Pinda, Membe, Mwandosya, Mwanri, Magufuli na wengineo ambao hata nyie mnawakubali na utendaji kazi wao, hivyo watumieni watu hawa kufikisha salamu zetu. Tusikate tamaa bandugu, hapa tupo ICU hivyo kukata tamaa kuna maana moja tu..Muflis na Wakenya watatucheka sisi wote na sii JK tena.
 
..Kusema mali ya wizi imeshapatikana, tusahau wizi uliofanyika bali tupange namna ya kutumia mali hiyo ni kijinyima authority ya kuzuia wizi. Vorster wa Afrika ya kusini aliwahi kusema watu weusi ni wasahaulifu sana wakipata chochote kidogo. Kama tuliona tumetukanwa wakati huo, ni kwa nini leo tunataka kujitukana wenyewe leo? Wenzetu wanamaliza mmbo magumu ya aina hii mahakamani, siyo kinyeji. Kushindwa kuonyesha utii kwa sheria kubwa sana ya uchaguzi ni dalili ya wazi kuwa hatutaweza kutii sheria ndogo ndogo nyingi sana za kutoonea wanyoge. Kikwete ana watu wengi sana wa kufadhili kwa kumsaidia wizi wa uchaguzi ambao hatawafanya lolote kipindi kijacho hata wakivunja sheria gani.
 
Kwa hiyo unashauri vipi mkuu wangu tumfikishe JK mahakamani? mahakama ambayo inachaguliwa na yeye pasipo kupitishwa tena kisha mwapisha jaji mkuu mara tu baada ya ushindi..hiyo kesi itafika wapi?..
 
Nyumba bila msingi (foundation); si nyumba; hata uipambe vipi; haiwezi kuwa nyumba. CCM haina maadili (Ethics). Kama umefuatilia uchaguzi uliokwisha utaona kuwa rushwa ilitawala sana, rushwa ndiyo imekuwa uti wa mgongo kwa uchaguzi. Kama First Lady anapita na kurusha kanga; na pesa kwa wapiga kura what do you expect? Kikwete inasemekana alikuwa anatoa madau ya fedha kwa walioshinda ili waseme wameshindwa. Na hizo pesa zilizokuwa zinatajwa zilikuwa kubwa. Imagine tunaambiwa Wenje aliahidiwa 0.8 billion; mama mia what kind of money is that for an average Tanazian? That is big money. ASk yourself where does all that come from? Corruption is a virus which have taken host of all our organs; and for sure nothing will be done before killing this virus; and in case we want to kill it, that organ must diel; meaning that CCM has to be abolished; because it cannot be repaired.

Swahiba; haiwezrkani kabisa priority ya Kikwete sasa hivi iwe kujenga nchi; priority yake itakuwa ni kulipa fadhila, kulipa madeni na kutaka kumridhisha kila mtu ambaye alimsaidia. This will eat some years in his five years. For your information mafisadi wanaeleweka; tunambiwa zile helkopta zilikodiwa na mafisadi. Wafanyakazi walikatwa mishahara yao; na wafanyabiashara Nchi nzima walichangia pesa kusaidia CCM. Makampuni yote makubwa ya wageni na wenyeji vile vile yametoa michango yao do you expect him to turn them away? Na ujue hiki ni kipindi chake cha mwisho; lazima ajitayarishie retirement; hatakuwa na muda na maendeleo yetu.

Kuongeza mapata na kubadilisha uchumi. For a country like Tanzania this is very simple; but it is a very difficult issue for CCM. Kwanza muulize Kikwete priority yake kwenye uchumi; hawezi kukuambia; hana sera. Kote alokokwenda alikuwa akitoa ahadi tu; without policy. Kilimo Kwanza hakuiongelea; we expected him to go deep how he can make implementation of this. Vitu muhimu kwa 80% ya population ya Tanzania ni Kilimo; pale ndipo alibidi asistizie namna atakapofanya. Aliongelea kuleta Industries Tanga, Mtwara, Kigoma kuwa Dubai; lakini hakuongelea how he will do that. Aliongelea kujenga machinga Centres 6 Dar; these machinga centres to Sell what; from where? Na akasema kahaidiwa dollar 100 million na wachina; what I was expecting was; kujenga angalau light industry good; textile mills, bulding materials factories, etc to create a foundation for an export oriented economy. Also infrastructure. After you have those then these machinga centers will come by themselves.

Education, Healthy care; these are the foundation of a healthy Nation; a Nation without healthy people is not a strong nation. Kudharau Elimu na Afya za wananchi ni dhambi na ni kudumaza Taifa.

Solution sasa hivi siyo kuanza kuungana na mafisadi; bali kuangalia tulikotoka na ktathmini yote yaliyotokea hadi sasa, tumepoteza miaka 50; miaaka 5 siyo mingi; from day one; CCM iachwe ifanye mabo yake; in case they will change then well and good. Lakini kumbuka ni taabu kumfundisha mbwa mzee mbinu mpya. Hawa makada wote pamoja na viongozi wa CCM tangu Uhuru; which changes do you expect?

Miaka mitano hii CUF na Chadema zijiendeleze kama zilivyo; kwa sababu zishakuwa na support base; na itikadi; which are well defined. CCM is going to die a nutural death. For a new constitution, new independent NEC, and a body to monitor corruption it will not be easier for CCM to survive.
 
Ushauri mzuri sana Mkandara lakini kama wenzangu walivyowahi kusema hapo juu huyu mtu hana upeo wa kusikiliza ushauri mzuri kama huu. Amezungukwa na wapambe ambao watamweleza anachotaka kusikia. Kikwete angelikuwa na washauri wazuri, huu uchaguzi angeushinda bila wizi kwa sababu wananchi walikuwa wanataka ajitenge na mafisadi na hakuweza. All the people wanted from him is something that would show them that he is not one of the Mafisadis but he failed even that. Kwa sababu hiyo, simuoni kama mtu ambaye anaweza kusikiliza ushauri mzuri kama huo wa Bwana Mkandara.
 
quote_icon.png
Originally Posted by Kichuguu
..Kusema mali ya wizi imeshapatikana, tusahau wizi uliofanyika bali tupange namna ya kutumia mali hiyo ni kijinyima authority ya kuzuia wizi. Vorster wa Afrika ya kusini aliwahi kusema watu weusi ni wasahaulifu sana wakipata chochote kidogo. Kama tuliona tumetukanwa wakati huo, ni kwa nini leo tunataka kujitukana wenyewe leo? Wenzetu wanamaliza mmbo magumu ya aina hii mahakamani, siyo kinyeji. Kushindwa kuonyesha utii kwa sheria kubwa sana ya uchaguzi ni dalili ya wazi kuwa hatutaweza kutii sheria ndogo ndogo nyingi sana za kutoonea wanyoge. Kikwete ana watu wengi sana wa kufadhili kwa kumsaidia wizi wa uchaguzi ambao hatawafanya lolote kipindi kijacho hata wakivunja sheria gani.

Kichuguu;

Kimsingi nina mtizamo kama huu!

Kwa hiyo unashauri vipi mkuu wangu tumfikishe JK mahakamani? mahakama ambayo inachaguliwa na yeye pasipo kupitishwa tena kisha mwapisha jaji mkuu mara tu baada ya ushindi..hiyo kesi itafika wapi?..

Mkandara;

Nina dilema kama ..hiyo unayoiyohoji...

Lakini;

1. Nafikiri haitakuwa sahihi kunyamazia hali hii hata kama kwa sasa hatuna jibu au utatuzi sahihi.

2. Kulisemea jambo hili sehemu yeyote unapopatika upenyo.. wana harakati ..etc..ni vema!

3. Kwa kuwa hatuna njia nyigine kwa sasa hata kulifungulia kesi... ambayo tunajua haitaleta matunda ya kina...bado itakuwa ni jukwaa la kusemea jambo hili kwa umma, itakuwa ni sehemu ya kuamsha umma ambao inaonekana unachukua muda mrefu kuamka.

Kwa mfano;

Mh Mramba na Daniel Yona... Kesi yao inasua sua mahakamani so far!

Ingawa hatutegemei sana...kupata hukumu ya maana ..lakini nafikiri ni chanzo kizuri cha kujengea uamasho kwa jamii!

Nafikiri imemcost Mramba na Jk mwenyewe aliyejaribu kumsafisha kiana fulani alipo mpigia kampeni...lakini hatimaye wananchi wakawa sio wajinga wa kiwango cha viongozi hao!

Wakati haya yanaendelea then tutakuwa tunaedelea kutafakari mikakati mingine ...more effectively!

Kwa hiyo Hata makosa yaliyofanywa na NEC kwenye uchaguzi huu, hayana budi kutafutiwa namna ya kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria ...hata kama vitakuwa ni vya kimataifa nk!

Hivi mnajua kama hali ingeachiwa kidogo tu...vurugu zilizotokea kwenye majiji kama arusha, mwanza, shinyanga nk... yangeweza wakati wowote kufikia karibu kama hali zilizotokea kenya?...Na simply mtummoja tu ...ametoa amri ya kuchelewesha matokeo/kuyabadili...alafu leo anaachwa ..anatembea mtaani anafuraha na kuwatunza wote waliowezesha hayo kutokea nk...Tatizo kubwa .... Mambo haya yatafanywa tabia...! Maana swali ni kwamba ..nini kitazuia uchaguzi mwingine ukifanyika haya yasirudiwa na kutunzwa kwa sifa za kem kem za kifisadi?... No no we have to do something to clearn the house before its too late!
 
Mimi nina wasi wasi mno kwamba hataanza safari za kujitangaza kwamba yeye ni Rais tena wa Tanzania baada ya kushinda kipindi cha pili kwa 61% maana hizi ndiyo zake mkuu wetu huyu kabla mkandala hujampa mawazo mazuri na mazito maana naamini hata akiyasoma maneno yako atakuwa haelewi .
 
HAYO NI MANENO YA LACK OF APPRECIATION.

The guy has done alot and promises to do more. Dont be mean man!

Ameonyesha kuwa hanazo sifa za kutekeleza vitu kama hivyo. He has neither the intellect nor the initiative and energy of a true leader, rather he happens to be as weak as my 3-months old baby daughter plus the fact that his hands are tied. What a freak!
 
Mkandara;
Nyumba bila msingi (foundation); si nyumba; hata uipambe vipi; haiwezi kuwa nyumba. CCM haina maadili (Ethics). Kama umefuatilia uchaguzi uliokwisha utaona kuwa rushwa ilitawala sana, rushwa ndiyo imekuwa uti wa mgongo kwa uchaguzi. Kama First Lady anapita na kurusha kanga; na pesa kwa wapiga kura what do you expect? Kikwete inasemekana alikuwa anatoa madau ya fedha kwa walioshinda ili waseme wameshindwa. Na hizo pesa zilizokuwa zinatajwa zilikuwa kubwa. Imagine tunaambiwa Wenje aliahidiwa 0.8 billion; mama mia what kind of money is that for an average Tanazian? That is big money. ASk yourself where does all that come from? Corruption is a virus which have taken host of all our organs; and for sure nothing will be done before killing this virus; and in case we want to kill it, that organ must diel; meaning that CCM has to be abolished; because it cannot be repaired.

Swahiba; haiwezrkani kabisa priority ya Kikwete sasa hivi iwe kujenga nchi; priority yake itakuwa ni kulipa fadhila, kulipa madeni na kutaka kumridhisha kila mtu ambaye alimsaidia. This will eat some years in his five years. For your information mafisadi wanaeleweka; tunambiwa zile helkopta zilikodiwa na mafisadi. Wafanyakazi walikatwa mishahara yao; na wafanyabiashara Nchi nzima walichangia pesa kusaidia CCM. Makampuni yote makubwa ya wageni na wenyeji vile vile yametoa michango yao do you expect him to turn them away? Na ujue hiki ni kipindi chake cha mwisho; lazima ajitayarishie retirement; hatakuwa na muda na maendeleo yetu.

Kuongeza mapata na kubadilisha uchumi. For a country like Tanzania this is very simple; but it is a very difficult issue for CCM. Kwanza muulize Kikwete priority yake kwenye uchumi; hawezi kukuambia; hana sera. Kote alokokwenda alikuwa akitoa ahadi tu; without policy. Kilimo Kwanza hakuiongelea; we expected him to go deep how he can make implementation of this. Vitu muhimu kwa 80% ya population ya Tanzania ni Kilimo; pale ndipo alibidi asistizie namna atakapofanya. Aliongelea kuleta Industries Tanga, Mtwara, Kigoma kuwa Dubai; lakini hakuongelea how he will do that. Aliongelea kujenga machinga Centres 6 Dar; these machinga centres to Sell what; from where? Na akasema kahaidiwa dollar 100 million na wachina; what I was expecting was; kujenga angalau light industry good; textile mills, bulding materials factories, etc to create a foundation for an export oriented economy. Also infrastructure. After you have those then these machinga centers will come by themselves.

Education, Healthy care; these are the foundation of a healthy Nation; a Nation without healthy people is not a strong nation. Kudharau Elimu na Afya za wananchi ni dhambi na ni kudumaza Taifa.

Solution sasa hivi siyo kuanza kuungana na mafisadi; bali kuangalia tulikotoka na ktathmini yote yaliyotokea hadi sasa, tumepoteza miaka 50; miaaka 5 siyo mingi; from day one; CCM iachwe ifanye mabo yake; in case they will change then well and good. Lakini kumbuka ni taabu kumfundisha mbwa mzee mbinu mpya. Hawa makada wote pamoja na viongozi wa CCM tangu Uhuru; which changes do you expect?

Miaka mitano hii CUF na Chadema zijiendeleze kama zilivyo; kwa sababu zishakuwa na support base; na itikadi; which are well defined. CCM is going to die a nutural death. For a new constitution, new independent NEC, and a body to monitor corruption it will not be easier for CCM to survive.
Mkuu habari hii nzito sana!... nimekusikia sana lakini mbona bado unaweka UCCm na Uchadema? nauliza tufanye nini leo hii maadam mtu huyu Dr.Kikwete ndiye katangazwa kuwa rais?

Najiuliza la kufanya na ndio nimekuja na hoja hii hata kama. Hivi kweli ni busara tuache JK akilipa fadhila zake na pengine kulipa kisasi kwa wale walioacha kumpigia kampeni, tusubiri hadi mwaka 2015 kwa imani kwamba CCM will die a natural death! and what if sisi wananchi tutakufa wengi before CCM dies! maanake sisi sii Miungu wala hatufahamu mbinu mpya ya CCM itakuja na rumba gani...Kumbuka tu kwamba hata wao wanatazama jinsi ya kuua Upinzani.

Uchaguzi huu pekee wameiba kura kibao, nimeshtuka sana kuona walopiga kura mwaka 2005 walikuwa millioni 11 na ushee kisha mwaka huu tunaambiwa wamepiga kura watu millioni 8 tu hali vuguvugu la upigaji kura mwaka huu lilikuwa kubwa kuliko wakati wowote ule na hata sehemu za upigaji kura zinathibitisha hilo. Kwa hili tumekuja na hoja zetu ili kuipangua kabisa NEC na kuundwa chombo kipya na huru lakini tunasahau kwamba bado tunaongozwa na mtu yule yule aliyefanya machafu haya...

Na zaidi mimi nadhani kusubiri miaka mitano ijayo wakati JK akilipa fadhila na kuweka visasi kwa wale ambao hawakumuunga mkono tunajiweka katika nafasi mbaya zaidi kitaifa. Ni wakati wa kushusha bendera za chama (kuondoa Chuki) na kupeperusha ile ya Taifa kwa mawazo yanayojenga nchi yetu kinyume cha hapo ni kukubali kwamba tuna wakati mgumu sana mbele yetu.
 
Kwanza kabisa ondoa maneno "visasi" au "Uchadema na UCCM" i am not of that type. I am trying to just be "serious". Wewe unataka tukubali kuwa CCM has done it illigetimate then we should not bother these issues let us join them. Ninachosema CCM did it wrong; then; kwa sababu ile misingi iliyokuwepo ishabomolewa; leo ili uwe kiongozi CCM cha kwanza sifa kubwa lazima uwe corrupt; mwongo nk nk No ethics at all. CCM inajenga society gani?? Swahiba wewe na mimi tumesoma siku zilee! Education was free and it was meant for all, literacy was above 90%. Leo hii Literacy sijui ni below 60% hivi huoni kuwa Taifa lipo hatarini? Kigumu kipi kufanya shule zetu zisomeshe watu?

Swahiba ulishaenda kijijini juzijuzi; au ndiyo umejichimbia huko mida yote? Sasa wewe ukitaka kujua CCM na madhambi yake nenda kijijini; ndiyo utajua dunia ya Afrika ni dhihaka. Not only no health care nor Education; kwanza watu wanaishi kama wanyama, huko kuna mbunge na mkuu wa wilaya. Mkuu wa wilaya akitembelea huko vijijini anapewa gunia la mahindi mbuzi hata kuku. Tanzania ilibidi iwe inapanda juu siyo kushuka chini.

Nikirudi kwenye topic hapo juu ni kuwa Tanzania iliyopo sasa hivi haitabidilika mikonni mwa CCM, kama itabadilika basi ni kwenda chini meaning kuwa it will be worse. It will take at least two years to recoup all resources utilised by Mr. Kikwete during election; that is massive amount of cash money. Sijui wali-print wapi zile pesa. Hiyo inflation itakuwa kubwa sana. In this case system ya CCM ishakuwa hivyo haiwezi kubadilika. Sasa hivi lazima tujenge vyama vyenye nguvu at least hata kama haviwezi kutawala lakini uwezo wa ku-influence decision uwepo. Slaa factor was very very strong na iliwatia kiwewe watawala. That is what we want.

Kushirikiana na CCM ni kucheza muziki wao; ndiyo maana nimesema kuwa; raslimali ya CCM ni matajiri na mafisadi hawawezi kukusikiliza wewe; lakini wanasahahu kuwa vijana ndiyo ingekuwa raslimali kubwa zaidi; na hii ndiyo Chadema inabidi wai-exploit. Sasa hivi CCM si chama cha Wafanyakazi na Wakulima tena.

Halafu ule msemo kuwa CCM ipo vijijini imeimarika, thubutu; wananchi wa vijijini wameangushwa tu na wasimamizi wa uchaguzi, lakini majority wamechagua opposition. That was Slaa factor. Watu bwana wanapenda maadili siyo propoganda. Huku unaiba kule unasema ni chama cha wanachi.

Soma hiii article ambayo imeandikwa na East African ukishamaliza niambie:
The East African:  - News |How CCM won an election but felt the earth move under its feet
 
Ndugu yangu Mkandara, fahamu kwamba huyu RAisi wetu aliingia madarakani akijua kuongoza nnchi ni suala la kifari na kujijengea mazingira ya kuwa na jina duniani hivyonbkuingia kwenye historia na kupata umaarufu.

Hivyo alikuwa na nia na dhamira tofauti kabisa na Uraisi, kwan umesahau baraza lake la kwanza la mawazir? Baadae akalivunja.. Hajui cha kufanya uoeo ni mdogo sana. RAisi gani hajui kwa nini nchi ni maskini? Kana kwamba haitoshi hata suala la foleni kwake ni maisha bora..

UShauri wako kwake ni sawa na kumwaga sukari baharini, kama huamini ngija uone baraza lake la mawaziri. Na usishangae jina la spika mpya, na wale wote mawaziri waliopigwa chini tokea kura za maoni kupewa madara.. How? Ukistaajabu ya MUsa utayaona ya firauni.
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom