Jk, makamba na familia: Zingatieni ujumbe huu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jk, makamba na familia: Zingatieni ujumbe huu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nyumbu-, Jun 1, 2010.

 1. N

  Nyumbu- JF-Expert Member

  #1
  Jun 1, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 969
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 60
  Ridhiwani, Januari walikwina?


  [​IMG]
  Na Ezekiel Kamwaga - Imechapwa 26 May 2010

  [​IMG][​IMG] Waraka wa Wiki


  [​IMG]


  ALIPOUAWA mtawala wa Urusi, Nicholaus II, 17 Julai 1918, mauti hayakumfika yeye peke yake. Aliuwawa na watoto wake watano; Alexei, Olga, Maria, Tatiana na Anastasia.
  Hata mkewe wake, Alexandra, daktari wake, nao waliuawa pamoja naye. Nicholaus II aliuwawa kwa kupigwa risasi na wale waliojipachika jina “Bolshevik” – wapinzani wa utawala wa kifalme wa Urusi.
  Hasira ya wananchi wa Urusi ilikuwa kwa ukoo wote wa kifalme. Kama Wakomunisti wale wangepata nafasi wangetekeza ukoo mzima wa mtawala huyo.
  Baada ya Bolshevik kumiminia risasi Nicholaus na familia yake, mabinti wale wanne walikuwa hawajakata roho. Kwa sababu kila mmoja alikuwa amevaa vidani na nguo zilizodariziwa kwa almasi kiasi kwamba risasi hazikuweza kupenya milini mwao.
  Walichokifanya wauaji, ni kuwasogelea karibu mabinti hao – Olga, Maria, Tatiana na Anastasia – kisha kuwaua kwa kuwakata vichwa kwa kutumia mapanga na mashoka!
  Ni ukatili ambao ni vigumu kuueleza kwa binadamu wa kawaida. Na hii ndiyo hatari ambayo naiona kwa wanasiasa ambao wanajitahidi kuingiza familia zao kwenye ulingo wa siasa.
  Kinachotokea ni kwa jamii nzima kuichukia familia nzima badala ya mtu mmoja.
  Kwanza niseme mapema kwamba mimi si miongoni mwa watu wanaopinga watoto wa wanasiasa kuingia katika siasa hususani katika mwaka wa uchaguzi kama huu.
  Roho yangu haisononeki kabisa kwamba Amani Abeid Karume, amekuwa rais wa Zanzibar nafasi ambayo baba yake, Abeid Amani Karume aliishikilia kwa miaka nane.
  Wala sitakuwa na shida iwapo, Balozi Ali Abeid Karume na Dk. Hussein Mwinyi watakuja kuwa marais ama wa Zanzibar au Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
  Aidha, siwezi kuwa na kinyongo iwapo, January Makamba, Kippi Warioba, Ridhiwani Kikwete, Nape Nnauye, John Mongella, Dk. Mwele Malecela, Makongoro Nyerere, Mohammed Moyo, Vita Kawawa na wengine, watabahatika kupata utukufu ambao wazazi wao walikuwa nao huko nyuma.
  Kusema kwamba hawafai kwa sababu tu, baba zao walikuwa wanasiasa ni kuwaonea. Hii ni sawa na kupingana na asili. Kila mmoja anastahili kujiandikia historia yake.
  Tatizo langu kubwa lililopo kwa viongozi wetu, ni kule kutaka “kuchomeka” watoto wao, ambao hawana uwezo wa kuongoza. Kwamba mtu anapanda vyeo kwa sababu ya wadhifa wa baba yake.
  Kama Amani Karume ana sifa na uwezo wa kuwa rais, hakuna sababu ya kutompa nafasi. Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alisema, “Tusichague rais kwa kutokana na kabila lake, dini yake au ukoo anaotoka.”
  Lakini pia hatuwezi kukataa kuchagua kiongozi kwa kuwa tayari baba yake alishika nafasi hiyo.
  Kwenye fani nyingine, kwa mfano kwenye mpira, mtoto atapata mafanikio tu iwapo atakuwa na uwezo. Kwamba Ngassa anaweza kucheza Yanga kwa sababu alikuwa na uwezo.
  Kama angekuwa hajui kucheza mpira kama mimi, asingepangwa Yanga hata kama baba yake angekuwa Imani Madega. Ndiyo maana watoto wa Pele hawapangwi kwenye timu ya Brazil. Kama mtu hana uwezo, hawezi kupangwa.
  Kwenye siasa, mtu ambaye alikuwa hafahamiki wala kujulikana, ghafla anapanda vyeo na kuwa na ushawishi mkubwa mara mzazi wake au ndugu yake anapokuwa na madaraka ! Hapa ndipo kwenye matatizo.
  Nicholas aliuawa kwa sababu hakuwa kiongozi mzuri. Alifanikiwa tu kuwa mtawala wa Urusi kwa sababu baba yake, Alexander III alikuwa Mfalme na alipokufa yeye akamrithi.
  Katika kitabu cha Guns of August, mwanahistoria Barbara Tuchman aliandika kwamba mfalme Alexander III alikuwa hajampa mafunzo yoyote mwanaye (Nicholaus) kuhusu mambo ya utawala.
  Alikuwa amepanga kumpa mwanaye huyo mafunzo rasmi atakapokuwa ametimiza umri wa miaka 30 lakini kwa bahati mbaya mfalme akafariki wakati mtoto ana umri wa miaka 26.
  Kwa hiyo, kwa sababu tu Nicholaus alikuwa mtoto wa mfalme, akapewa fursa ya kurithi bila ya kujua kitu kuhusu utawala.
  Katika kitabu hicho, Tuchman anaeleza tukio moja kumhusu Nicholaus, kwamba wakati alipopewa taarifa za awali kuhusu mashambulizi yaliyokuwa yakifanywa na Wakomunisti hao, “aliisoma taarifa hiyo na kisha kuiweka mfukoni kabla ya kuendelea kucheza tennis.” Hakufanya lolote!
  Ni vema, katika mwaka huu wa uchaguzi, wanasiasa wetu wakawa makini sana katika namna ambavyo wanahusisha familia zao na mambo ya siasa.
  Kama mtu alikuwa si lolote wala si chochote kabla baba au mama hajawa rais au waziri mkuu, anakuaje kila kitu wakati baba anapokuwa mkubwa?
  Uongozi unahusu ugawaji na matumizi ya rasilimali za taifa. Ni vema, kwa kiongozi na familia yake, akafahamu wananchi wanapomka wanakuwa na uchungu sana na matumizi ya rasilimali zao.
  Kama kiongozi anaona mkewe au mwanaye ana sifa na uwezo wa kuwa kiongozi, ni vema akamruhusu ili asilinyime taifa uongozi murua.
  Lakini, atakuwa anafanya jambo la hatari sana kama ataruhusu watu wake wa karibu kutumia cheo na ushawishi wake kujiingiza kwenye mambo ya nchi.
  Hapa atakuwa anaiingiza familia yake katika matatizo makubwa bila ya kufahamu. Wakati utakapofika wa yeye kuondoka madarakani, afahamu hataondoka peke yake, ataondoka na familia yake.
  Na kama walifanya vibaya, afahamu kwamba ataandamwa, yeye na familia yake, kwa kiwango ambacho kuna kipindi hakuna mtu wa familia huyo atapenda kutumia ubini wao kujitambulisha.
  Kabla kiongozi hujamruhusu mwanao au mkeo kuingia kwenye siasa wakati wewe ni mtawala, ni vizuri ujiulize ni kwa nini hawakuingia kwenye siasa kabla hujawa kiongozi.
  Kwamba inakuaje ghafla wanakuwa na sifa za uongozi baada ya wewe kuwa madarakani? Mbunge wa Njombe, Dk. Ndembela Ngunangwa, alikemea hilo kwa kuuliza: Walikwina – walikuwa wapi - kabla ya wewe kuwa madarakani?
  Kimsingi hili ni jambo rahisi sana kulifanya. Hakuna sababu ya viongozi wetu kuingiza familia zao kwenye matatizo. Makosa yao yanaweza kusamehewa na kizazi cha jana na leo.
  Nani ajuaye kizazi cha kesho kitakuwa na maamuzi gani?


  BINAFSI NILISHALIONA TATIZO HILI. NAAMINI KABISA WENYEWE WANALIJUA, ILA SI VIBAYA KUKUMBUSHANA. INGAWA NDIO FASHENI SIKU HIZI KWA EAST AFRICA. MFANO NI MUSEVENI. BUT IT IS WORTH NOTING.
   
 2. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #2
  Jun 1, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  MIMI katika Vijana woote ni nafuu, huyu mtoto wa Kikwete kabadilika sana, akiwa chuo hakujivunia cheo cha Babake, lakini leo, anazunguka mitaani mikono juu, akijivunia mamlaka ya baba yake, akijivunia Ikulu, mimi sijui anakasoro gani, simpendi.
   
 3. Eng. SALUFU CA

  Eng. SALUFU CA Senior Member

  #3
  Jun 1, 2010
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 146
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni kweli usemayo Nyumbu lakini mahakimu ni wapiga kura ambao wamejibweteka wakipiga kura bila kujua au kwa ushawishi fulani bila kuangalia maslahi ya majority. Anyway time will tell the truth!!
   
 4. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #4
  Jun 1, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Ole wenu na makasri yenu mliyojijengea! Ipo siku mtayakimbia hayo na mkailaani siku mliyozaliwa!
   
 5. N

  Nyumbu- JF-Expert Member

  #5
  Jun 1, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 969
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 60
  Hatuombei iwe hivyo, lakini ajidhanie amesimama, aangalie asianguke. Ufalme wowote ule huanguka pale unapodhani umefikia kilele. Nebukadnezar wa Babeli alitumia vyombo vitakatifu kwa kiburi cha kwamba hakuna kilich juu yake. Aliangamia.
  Na tutafakari!
   
 6. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #6
  Jun 1, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  We eh NABUKANDNEZA MKUU! Ninani aliyekuambia kuwa kiti chako kitasimama milele?
  Tubu kabla haijaja ile siku ambayo BABYLON itateketezwa mbele yako! Haya ndo maono yangu kwa watawala hawa.
   
 7. andrewk

  andrewk JF-Expert Member

  #7
  Jun 1, 2010
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 3,103
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  story nzuri, nyerere aliisona sana nan kuelewa,
   
 8. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #8
  Jun 1, 2010
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Ingekuwa ni kweli hawa wapiga kura wana judgement power mada hii ingekuwa haina mantiki, lakini kwa nchi kama Tanzania wapiga kura ni wapo kama njia ya kuonesha something democracy has taken place but in reality, wapiga kura hawachagui viongozi bali wanashirikishwa kuonesha kuwa wanachagua wakati maamuzi yote yanafanywa kwa mizengwe na hila za kutangazana wao kwa wao ndani ya CCM. Huwezi kuwa na free and fair election kama watendaji wa tume ya uchaguzi ni makada wa CCM (wanaochaguliwa na mwenyekiti wa CCM-Rais) na kwa wao kumtangaza non-CCM candidate kuwa ameshinda ni kumwaga unga kuwa ameshindwa kazi. Au anapewa onyo next time asirudie!
   
 9. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #9
  Jun 1, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  What a post, Well done!

  Huwa nasikia kichefuchefu kila ninapomuona mama fulani akikemea na kuongea kama waziri mkuu, hujisikia kutapika nikisikia mtoto wa katibu mkuu wa chama fulani ndiye mwandishi wa hotuba za rais wa nchi fulani, huwa naumwa nikisikia mtoto wa rais ndiye amewaweka akina fulani pale walipo.... Naamini mwisho uko karibu na watalia na kusaga meno pale watakapovuliwa utukufu waliojivika
   
 10. d

  damn JF-Expert Member

  #10
  Jun 1, 2010
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 585
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  JK (ridhiwani), CCM (mafisadi) na MAKAMBA(Januari) - --MENE MENE TEKELI NA PELESI!!!!!!!!!
   
 11. N

  Nyumbu- JF-Expert Member

  #11
  Jun 1, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 969
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 60
  You have said it! Halafu unashangaa inakuwaje vyama vya upinzani havipigii kelele hili, au hata kususia uchaguzi, au kuzuia uchaguzi mahakamani mapa tume guru iundwe. Hii inaniaminisha kuwa wapo kuzuga tu, na ndio maana wanaiogopa CCJ kwani hawana mkono wao kule!
   
 12. Songoro

  Songoro JF-Expert Member

  #12
  Jun 1, 2010
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 4,136
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 0
  Rejeeni historia ya nchi zote za dunia ya kwanza hakuna taifa lolote lililoondoa viongozi wabovu kama wetu kwa njia ya Kura. Hitler, Mussolin, Tito,King leopard, King William wote hawa waliondolewa kwa mawe ya wananchi sio makaratasi ya kura,nyie mnaosubiri mafisadi wa sign karatasi za kura kuthibitisha kuondoka kwao MSICHOKE KUSUBIRI PIA MSITEGEMEE KUPATA, viongozi bora
   
Loading...