JK Kutangaza wakuu wapya wa Mikoa?

JK Kutangaza wakuu wapya wa Mikoa?

Status
Not open for further replies.
Watu wengi wenye akili wamekuwa wakihoji..nn kazi ya wakuu wa wilaya na mikoa? Ukifatilia kiundani utagundua hawana kazi yoyote ya maana zaidi ya kuongeza gharama. Toka uchaguzi uishe mpaka leo JK hajateua wakuu wapya wa wilaya na Mikoa. Hiyo inatudhihirishia kuwa hawa jamaa ni mzigo tu, wangekuwa muhimu rais asingeweza kukaa mpaka leo (almost a year) bila kuappoint hawa watu. Hii kada ifutwe. Najua magamba hawawezi kufanya hivyo, hii ni rai yangu kwa CDM tutakapochukua nchi mwakani baada ya nguvu ya umma kuyatoa magamba madarakani.
Mnachukuaje mwakani.???..
 
Wana kazi kubwa sana, hivi huoni pengo aliloacha Nape kule wilayani kwake? nasikia mambo kibao yamesimama baada ya kupangiwa kazi nyingine. au huoni pengo lolote hapa Dsm baada ya kuchelewa kuteua Mkuu wa Mkoa?

Hakuna lolote zaidi ya ulaji. Hivi hilo pengo lingekuwa linaonekana si wananchi wangelalamika. Kazi ya Wakuu wa wilaya na mikoa ilikuwa ni kwa ajili ya kupiga propaganda za chama enzi za chama kimeshika hatamu (sorry utamu). Kwa hivi sasa ni mzigo tu na badala yake wangeweka magavana ambao pia wangepatikana kupitia kura za wananchi.
 
Wana kazi kubwa sana, hivi huoni pengo aliloacha Nape kule wilayani kwake? nasikia mambo kibao yamesimama baada ya kupangiwa kazi nyingine. au huoni pengo lolote hapa Dsm baada ya kuchelewa kuteua Mkuu wa Mkoa?
kuna pengo gani kwenye mikoa/wilaya zisizo na wakuu wake? Hizo ni nafasi za kisiasa, kuna haja gani ya wakurugenzi na maafisa tawala wa mikoa na wilaya? Wote huo ni kujiongezea gharama zisizo na tija. Hakuna haja ya kuwa na wakuu wa mikoa/wilaya wakati kuna wakurugenzi na maafsa tawala.
 
Watu wengi wenye akili wamekuwa wakihoji..nn kazi ya wakuu wa wilaya na mikoa? Ukifatilia kiundani utagundua hawana kazi yoyote ya maana zaidi ya kuongeza gharama. Toka uchaguzi uishe mpaka leo JK hajateua wakuu wapya wa wilaya na Mikoa. Hiyo inatudhihirishia kuwa hawa jamaa ni mzigo tu, wangekuwa muhimu rais asingeweza kukaa mpaka leo (almost a year) bila kuappoint hawa watu. Hii kada ifutwe. Najua magamba hawawezi kufanya hivyo, hii ni rai yangu kwa CDM tutakapochukua nchi mwakani baada ya nguvu ya umma kuyatoa magamba madarakani.
Umekunywa viloba vingapi mkuu? maana unaongea pumba kweli. Wewe unataka ateue wa nini wakati wapo na kazi wanafanya? kwani lazima awabadilishe? tumia akili.............
 
Wana kazi kubwa sana, hivi huoni pengo aliloacha Nape kule wilayani kwake? nasikia mambo kibao yamesimama baada ya kupangiwa kazi nyingine. au huoni pengo lolote hapa Dsm baada ya kuchelewa kuteua Mkuu wa Mkoa?

Hawana kazi yoyote..sana sana wanakwamisha maendeleleo koz wengi wao ni vihiyo.
 
kuna pengo gani kwenye mikoa/wilaya zisizo na wakuu wake? Hizo ni nafasi za kisiasa, kuna haja gani ya wakurugenzi na maafisa tawala wa mikoa na wilaya? Wote huo ni kujiongezea gharama zisizo na tija. Hakuna haja ya kuwa na wakuu wa mikoa/wilaya wakati kuna wakurugenzi na maafsa tawala.

Hapa nimefurahishwa na Avatar yako mkuu.Umekaa ukafikiria sana kuhusu hiki kiatu cha Nyerere,sasa ungeweka mtu ambaye anafaa kwa mbali kama viatu vinamfaa kidogo kavaa gwanda za mgambo
safi sana.
 
Umekunywa viloba vingapi mkuu? maana unaongea pumba kweli. Wewe unataka ateue wa nini wakati wapo na kazi wanafanya? kwani lazima awabadilishe? tumia akili.............

Nikuulize ww usiyejua ni mikoa na wilaya ngapi hazina RCs and DCs.
 
JK amegundua kuwa yeye na chama chake kimekosa mvuto kwa wananchi hivyo kwa vile chama kinachokubalika kwa wengi ni CDM ameamua kinyemela kutekeleza sera za CDM.
 
waziri mkuu alishatoa ufafanuzi wa jambo hili........fuatilia habari kabla ya kuleta upuuzi hapa,, eboo!

Yule waziri wenu ambaye kila kukicha anachanganya maneno..leo anasema posho zinatusaidia kugawa nauli kwa wapiga kura, kesho atasema serikali imeona posho ni tatizo inalifanyia kazi. Vp mkuu..declare interest naona unatukana tu
 
Hana bajeti ya kuwalipa wanaostaafu wanaohamishwa na wapya!!!ana by time tu ila hana pesa kabisa....alikimbiliaa ikulu alidhani mchezo...apambane sasa wenzake kila kitu kilikuwa kina flow na barabara kajenga pesa za ndani yeye mishahara tu hakuna shughuli maendeleo
 
Silazima kubadili Wakuu wa Wilaya na Mikoa kila baada ya uchaguzi nadhani wewe umekalili vibaya, Kama Ridhiwan alikuahidi ukuu wa Wilaya alikudanganya
 
Samahani wakuu zangu kuuliza sii ujinga..
Hivi kumbe mikoa yote haina wakuu wa mikoa na wilaya?
 
Silazima kubadili Wakuu wa Wilaya na Mikoa kila baada ya uchaguzi nadhani wewe umekalili vibaya, Kama Ridhiwan alikuahidi ukuu wa Wilaya alikudanganya
Wewe ndo tatizo usiyejua kuwa mikoa mitatu haina wakuu na wilaya chungumbovu hazina maDC
 
Naunga mkono hoja? Hatuhitaji kuwa na wakuu wa wilaya na mikoa. Kama vipi tuwe na maseneta wa mikoa ambao wanachaguliwa na wananchi na si hawa wateule wa Rais wasiokuwa na kazi. Kazi kubwa ya mkuu wa wilaya au mkoa, inafanywa na wakurugenzi. Wao kazi yao kuhudhuria vikao tu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom