JK Kutangaza wakuu wapya wa Mikoa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK Kutangaza wakuu wapya wa Mikoa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by faithful, Nov 24, 2010.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. faithful

  faithful JF-Expert Member

  #1
  Nov 24, 2010
  Joined: Aug 10, 2010
  Messages: 375
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  taarifa nilizozipata kutoka chanzo ninachokiamini ni kwamba orodha ya wakuu wa mikoa tayari imeshaandaliwa!
  wale ma rc waliodondoka kwenye majimbo wote imekula kwao,
  wale wote ambao ni wabunge hawatapata u r.c kwani hakuna kofia mbili.
  kuna ma dc vijana ambao wamefanya vizuri katika wilaya zao watapata promosheni
  kuna ma rc watakao pumzishwa kwa sababu ya umri
  wale wabunge waliopoteza majimbo katika uchaguzi mkuu wote hakuna huruma ya kupozwa u r.c walie tu
  hata hivyo kuna waliotajwa kupata u rc kama vile mzee tibaigana,rainfred nasako,mama jannet mbenne,aisha kigoda na erick shigongo
  habari zaidi nitawaletea!
   
 2. Kashaijabutege

  Kashaijabutege JF-Expert Member

  #2
  Nov 24, 2010
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 2,699
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Katika wanaokisiwa, nimempenda Rainfed Masako, huyu ni mchapa kazi. Huyu akiingia ulabu utanikoma pale Huduma Baa Mbagala. Mungu amsaidie kichaa wangu.

  Ila Diodorus Kamala umemsahau.
   
 3. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #3
  Nov 24, 2010
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Chanzo ni kipi ( cha fununu)
   
 4. faithful

  faithful JF-Expert Member

  #4
  Nov 24, 2010
  Joined: Aug 10, 2010
  Messages: 375
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  vyanzo vingine sio heshima kuviweka hadharani.....ila niamini mimi ni chanzo ninachokiamini!
  kamalaa hayupo kabisaaa!
   
 5. M

  Mbalinga JF-Expert Member

  #5
  Nov 24, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 1,380
  Likes Received: 407
  Trophy Points: 180
  Mimi nadhani JK hatawatupa Fredrick Mwakalebela na Dr Raphael Chegeni. Unajua hawa aliwaingiza kwenye timu yske ya kampeni, ni lazima aliwaahidi kitu.
   
 6. Lenana

  Lenana JF-Expert Member

  #6
  Nov 24, 2010
  Joined: Oct 10, 2010
  Messages: 422
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  kulipana fadhila au ndio tusemeje?
   
 7. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #7
  Nov 24, 2010
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  kwa hiyo idadi ya ma-rc wapya ni ngapi inayotarajiwa
  haya FAITHFULLY tuweke wazi kwa fununu zilizokufikia mpaka sasa...
   
 8. kiraia

  kiraia JF Gold Member

  #8
  Nov 24, 2010
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 1,614
  Likes Received: 268
  Trophy Points: 180
  Pia Bashe umemsahau
   
 9. Saharavoice

  Saharavoice JF-Expert Member

  #9
  Nov 24, 2010
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 2,644
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Tegemea M rc ambao ni watiifu kwa EL
   
 10. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #10
  Nov 24, 2010
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  ha ha haa,
  eti watiifu kwa EL a.k.a mamvi
   
 11. j

  jilala Member

  #11
  Nov 24, 2010
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 38
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  .
  Kweli Edward Lowassa ana kazi kubwa sana.
  amesemwa kwenye uwaziri,lakini hatujaona jina lake.leo jina lake limeamishiwa kwenye u- rc.Kazi kweli wana jf.
   
 12. MmasaiHalisi

  MmasaiHalisi Senior Member

  #12
  Nov 24, 2010
  Joined: Jan 15, 2009
  Messages: 192
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Aden Rage mkuu wa mkoa Tabora
   
 13. faithful

  faithful JF-Expert Member

  #13
  Nov 24, 2010
  Joined: Aug 10, 2010
  Messages: 375
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  wazee wote wenye zaidi ya miaka sitini hawapo kwenye list.watakaorudi tena wapo kama sita tu!ma dc watakaopanda wapo kama 5.........watakaobaki wote ni wapya!
  huenda na wewe upo!!!!
   
 14. K

  Kagalala JF-Expert Member

  #14
  Nov 24, 2010
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 2,372
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 145
  Haya ndo mambo ya kubadilisha katika katiba mpya. Inabidi ma rc wachaguliwe na wananchi wa mkoa huo kuondoa mambo ya wakuu wa mikoa kufanya kampeni kulipa fadhila kwa rais. Inabidi mkuu wa mkoa awe mtu anayeujua huo mkoa na tamaduni zao
   
 15. faithful

  faithful JF-Expert Member

  #15
  Nov 25, 2010
  Joined: Aug 10, 2010
  Messages: 375
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  wazo lako zuri sana lakini kabla hatujafika huko tujiulize,je hao wanaochaguliwa na wananchi wanachaguliwa kwa haki?manake uchaguzi wa wananchi pia umejaa fitna umejaa rushwa na ukishapita kwa mbinde huwa unaogopa hata kukosoa wananchi!mfano kama wavivu ni ngumu kukuta kiongozi wa kuchaguliwa anawasema wananchi wawivu ataogopa kukosa kura uchaguzi ujao...............ataogopa kuweka watu ndani!atakuwa hana nguvu ya kukaripia!
   
 16. J

  JokaKuu Platinum Member

  #16
  Nov 25, 2010
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,729
  Likes Received: 4,948
  Trophy Points: 280
  ..how about Januarius Makamba?
   
 17. T

  TanzActive JF-Expert Member

  #17
  Nov 25, 2010
  Joined: Nov 14, 2007
  Messages: 350
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ili Swali limeniacha hoi

  Hivi Mkwere anaweza kuja na manaibu wakuu wa mikoa enh ?
  au akasema mikoa fulani kwa sababu ya ukubwa wake Ma-Rc wanakuwa wawili ?
   
 18. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #18
  Dec 20, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  RAIS Jakaya Kikwete anatarajiwa kutangaza wakuu wa mikoa wapya wakati wowote kuanzia leo, Mwananchi Jumapili limedokezwa. Habari zilizopatikana kutoka serikalini zinaeleza kuwa orodha ya wakuu hao imeshaandaliwa na kwamba idadi ya wakuu wa mikoa wanawake imeongezeka ikilinganisha na ya sasa.

  “Kuna ma DC (wakuu wa wilaya)vijana ambao wamefanya vizuri katika wilaya zao wamepata promosheni (wamepandishwa) kuwa wakuu wa mikoa. Pia kuna ma RC (wakuu wa mikoa) wamepumzishwa kwa sababu ya umri,’’ kilisema chanzo chetu. Baadhi ya wakuu wa mikoa waliotajwa kurudi ni Kanali mstaafu James Simbakali (Kigoma), Kanali Mstaafu Enos Mfuru(Mara), Kanali mstaafu Anatoly Tarimo(Mtwara) na Said Meki Sadiki (Lindi) ambaye kwa sasa anakaimu nafasi hiyo mkoani Dar es Salaam.


  Baadhi ya Ma DC wanaotajwa kupata ukuu wa mkoa ni Chiku Galawa ambaye ni mkuu wa Wilaya ya Temeke, Dar es Salaam na DC wa Lushoto. Chanzo hicho kimemtaja Hilda Ngowe, Injinia Stella Manyanya, ambaye ni mbunge wa viti maalumu, pamoja na Mary Chatanda ambaye ni mbunge viti maalumu na Katibu wa CCM mkoani Arusha kuwa ni miongoni mwa wakuu wa mikoa wapya.


  Wengine ni Mary Mwajelwa, Mwaka Abdulham Ramadhan, Dk Charles Chizeba ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Buchosa mkoani Mwanza na Dk Batilda Buriani ambaye alikuwa Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais(Mazingira) katika baraza la mawaziri lililopita. Akiwa katika kampeni za urais, Rais Kikwete aliahidi kuteua wakuu wa mikoa katika mikoa mipya mapema kabla ya kuanza mwaka mpya.


  Novemba 24, mwaka huu Rais Kikwete aliteua baraza lake jipya la mawaziri na kubadilisha muundo wa wizara zake. Tangu Rais Kikwete aingie madarakani mwezi Desemba 2005, inakuwa ni mara yake ya pili kufanya uteuzi wa wakuu hao huku akiwa amewafanyia mabadiliko mara moja tu. Kwa mara ya kwanza, Februari 11, 2006 Rais Kikwete aliwaapisha wakuu 21 wa mikoa, wakiwemo 11 wapya na 10 wa zamani. Tukio hilo lilifanyika katika Ikulu ya Chamwino, Dodoma.


  Sherehe ambazo zilihudhuriwa na viongozi wakuu wa kitaifa, akiwemo Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, ambaye wakati huo alikuwa Makamu wa Rais, Edward Lowassa, aliyekuwa Waziri Mkuu kabla ya kujiuzulu na Waziri wa wa Afrika Mashariki Samuel Sitta wakati huo ambaye alikuwa Spika wa Bunge la Tisa. wakuu wa mikoa walioapishwa wakati huo ni Yussuf Makamba kuwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, ambaye kwa sasa ni Katibu mkuu wa CCM, Anatoly Tarimo (Manyara), Ditopile Mzuzuri (Tabora), Daniel Ole Njoolay (Rukwa), Jaka Mwambi (Iringa) na Isidore Shirima(Mara).


  Wengine ni William Lukuvi (Dodoma), Enos Mfuru (Kagera), Said Meki Sadiki (Lindi), John Mwakipesile (Mbeya), Henry Shekifu (Mtwara), James Msekela (Mwanza), Christine Ishengoma (Pwani), Johannes Balele (Shinyanga), Monica Mbega (Ruvuma), Parseko Kone (Singida) na Mohammed Abdulaziz (Tanga).

  Wengine ni Abbas Kandoro (Arusha), Helima Kasungu (Kigoma), Said Kalembo (Morogoro) na Mohamed Babu (Kilimanjaro).

  Hata hivyo, kufuatia kifo cha Ditopile Mzuzuri na kumteua Makamba kuwa Katibu Mkuu wa CCM, Rais alifanya madadiliko kidogo kwa kumhamisha Kandoro mkoa wa Dar es Salaam kutoka Arusha na kumteua Mwinyi Musa ambaye alikuwa ni Mkuu wa Wilaya ya Rungwe kuwa mkoa wa Tabora.


  Aprili 15, 2009 aliwabadilisha vituo vya kazi wakuu wa mikoa 11 na kuteua wengine wapya ambapo Lukuvi aliamishiwa Dar es Salaam, Kandoro(Mwanza), Msekela (Dodoma), Mfuru (Mara), Machibya (Morogoro), Kalembo (Tanga), Abdulaziz(Iringa), Amina Mrisho(Pwani) Dk Christine Ishengoma(Ruvuma), Monica Mbega(Kilimanjaro), na Mohammed Babu(Kagera)

  CHANZO: Gazeti la Mwananchi
   
 19. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #19
  Dec 20, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  Very reliable. Thanks for your info.
   
 20. Mathias Byabato

  Mathias Byabato Verified User

  #20
  Dec 20, 2010
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 905
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 45
  Habari hii ni nzuri lakini ina mapungufu makubwa kitaaluma.

  Hii ni tetesi na siyo habari kwani haina source, haina upande wa pili inafaa kuchapishwa kwenye new media kama JF ambao wanatoa option ya tetesi na confirmed stories.

  Nadhani Mwananchi wamepotoka kidogo
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...