JK Kutangaza wakuu wapya wa Mikoa?

Status
Not open for further replies.
baadhi ya majina ni james ole millya, daniel ole porokwa,lenganasa soipe,fransis ikayo hawa wote ni wamasai wanaomwunga mkono EL katika harakati zake na majina yao yapo katika orodha ya madc wapya! usiulize source.
 
Lau Masha
Batilda Burian
Mohamed Abdulaziz
Basil Mramba
Anthon Dialo
..........
.........
.........
..........
 
habari nlizozipata jamaa kamaliza kuandaa orodha yake tayari kwa kusomwa hadharani

Haya Mzee wa Visasi atawakomoa wote:
-Ambao majimbo yao yalienda upinzania hasa CDM
-Ambao hawakuwapokea vyema wakaaji wa Ikulu RZ1 na Salma kipindi cha kampeni.
-Wale ambao waliambiwa warekebishe matokeo ili Kikwete apate asilimia nyingi wakakataa/Waliokataa kutoa ushirikiano kwa wezi wa Kura.
-Wale wapenda Ukweli ulio kinyume na Mawazo ya JK
-Wale wenye uwezo kuliko JK
Jiandaeni.
 
Aisee, siku zinazidi kuisha; mikoa mipya iliyotangazwa na KJ inatia huruma, ni lini watachaguliwa wakuu wa mikoa? Au zilikuwa ni hoja za kisiasa???
 
Aisee, siku zinazidi kuisha; mikoa mipya iliyotangazwa na KJ mbona inatia huruma!; ni lini wakuu wa mikoa watatangazwa? au zilikuwa ni hoja za kisiasa!!
 
Hii ni hatari sana. Watawala wetu hawaziheshimu kauli zao. Mtakumbuka mh. Mizengo Pinda alipokuwa Kagera alitutangazia kwamba wakuu wa wilaya na mikoa mipya wangeteuliwa Mei hii na kwamba wilaya na mikoa hiyo itaanza rasmi mapema Julai hii. Sijui labda kwa vile Mei haijaisha. Vinginevyo sitaamini tena chochote kitakachotamkwa na watawala wetu. Ushauri wangu kwa watawala wetu: wasiwe wanayatolea matamko mambo ambayo hawana uhakika nayo. Ni aibu. Tukiomba mwongozo wa nini kifanyike iwapo mtawala mkubwa analiongopea taifa, wanatwambia hatuna adabu!
 
SUALA LA WAKUU WA MIKOA NA WAKUU WA WILAYA naamini watateuliwa tu muda sahihi utakapofika, sio suala la kisiasa hili, bali ni suala linahitaji umakini wa hali ya juu, sio suala la kukurupuka kama walio wengi wanafikiri hata kidogo, Mh Rais Dr Jakaya kikwete naamini akishakamilisha taratibu naamini atawateua.

nakuomba ndugu yangu hapo juu usitie shaka katika hilo, nhi yetu inachangamoto nyingi sasa katika kukabiliana na changamoto hizo umakini unahitajika hasa katika nafasi hizo mbili maana hao wanakwenda kushughulika na matatizo ya wananchi moja kwa moja maana watakuwa nao huko mawilayani na mikoani.

tuendelee kuvuta subira mpaka watakapoteuliwa.
 
UTEUZI WA WAKUU WA MIKOA NA WILAYA: uteuzi wa nafasi hizo unazingatia pia baudget ya nchi, mipango ya kiuchumi ya mikoa na wilaya sio suala la kukurupuka tu, naamini rais wa nchi, waziri mkuu , makamu wa rais na wasaidizi wao wanalifanyia kazi hizo na muda ukifika wakuu wapya wa mikoa tutafahamishwa na pia wakifuatiwa na wakuu wa wilaya baadae sina shaka na hilo.

mimi naamini kila kitu ni muda sahihi maandalizi sahihi na wakati sahihi kwa faida ya wananchi wa Tanzania.
 
Vipi mama hasna mwilima DC tandahimba aliyekuwa na bifu na sofia simba akamtimua ukatibu uwt amepata tena?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom