JK kuhutubia taifa kesho usiku

JK kuhutubia taifa kesho usiku

Hii siku ndiyo aliyoifanya bwana tutakaa na kumsikiliza rais wetu hakuna kama jk amethubutu kaweza sasa anasonga mbele.
 
Rais Kikwete leo usiku ameamua kuhutubia taifa ikiwa ni hotuba ya mwisho wa mwezi septemba pamoja na kwamba mwezi umemalizika.

Moja ya mambo tunayotarajia kupewa uzito ni swala la kusainiwa kwa muswada wa sheria ya mabadiliko ya katiba. Nikipata full text mapema nitawamwagia hapa jamvini.

Stay tuned

=========
Update:


TUNAPENDA KUWAJULISHENI KUWA HOTUBA YA MWEZI YA MHESHIMIWA RAIS ILIYOKUWA ITOLEWE LEO, JUMATANO, OKTOBA 2, 2013, SASA ITATOLEWA KESHO, OKTOBA 3, 2013. TUNAOMBA RADHI KWA MABADILIKO HAYO NA TUNAWAOMBA MSIITUMIE ILE PRESS RELEASE YA KWANZA. KWA MARA NYINGINE, TUNAOMBA RADHI.

ASANTENI

SALVA RWEYEMAMU
MKURUGENZI WA MAWASILIANO
IKULU,
DAR ES SALAAM.
2 OKTOBA, 2013

Hana jipya.
 
...desa halijakaa vizuri tu,mzigo unarekebishwa,mbona mkapa aliwahi kuhutubia taifa akiwa nje ya nchi...
Unadhani slaa na jk ni wamoja au mkapa na jk ni wamoja,
ndiyo maana jk ni rais slaa ni mwanaharakati .
 
Kuna sakata la mabilioni ya Uswiss ($6 billion) zaidi ya mwaka sasa. Kama kiongozi wa nchi alitakiwa azungumzie hili kwa kina lakini tangu lianikwe hadharani June, 2012 analikimbia kwa miezi 16 sasa!!!
Jk haongeangi ujinga daima hujadili maswala ya kitaifa utotoutoto kama wa akina slaa kutoa matamko yasiyo na maana huo mda hana.
 
Unadhani slaa na jk ni wamoja au mkapa na jk ni wamoja,
ndiyo maana jk ni rais slaa ni mwanaharakati .

Katika hii thread inaoneka asilimia kubwa unachangia wew tu, tena kwa kutokwa na povu jingi!! Kulikoni hayo yakukute ndugu!!!?
 
Rais alikuwa nje ya nchi karudi juzi tu sasa ulitaka awahutubie wananchi akiwa Marekani...subiri hotuba leo mtamsikia rais.

Mbona mara kibao tu wanatuwekea CD wakati jamaa yuko majuu? Hivi yeye huwa ni ulaya na marekani tu kwa nini hafanyi ziara kwenye nchi zingine za kiafrika kama Botwana, Angola, Rwanda, Mali, Ghana nk? Kunanini ulaya?
 
Jk haongeangi ujinga daima hujadili maswala ya kitaifa utotoutoto kama wa akina slaa kutoa matamko yasiyo na maana huo mda hana.
Katika watu wanaoongea upuuzi JK anaongoza. Si ndio huyu anayesema ana majina ya wauza madawa ya kulevya ila anatoa muda wajirekebishe? Tuuiteje huo kama sio ujinga?
 
Mbona mara kibao tu wanatuwekea CD wakati jamaa yuko majuu? Hivi yeye huwa ni ulaya na marekani tu kwa nini hafanyi ziara kwenye nchi zingine za kiafrika kama Botwana, Angola, Rwanda, Mali, Ghana nk? Kunanini ulaya?

Ataenda kuomba nini nchi za kiafrica,
 
Agusie yafuatayo kama mkuu wa nchi;

1) Tanzania kutengwa ktk ushiriki wa maamuzi ya EAC
2) Uamuzi wa serikali kuyafungia magazeti ya Mwananchi na Mtanzania
3) Uamuzi wa TRA kuendelea na kudai kodi ya laini za simu
4) Hali ya usalama wa nchi kama amri jeshi mkuu hasa tishio la ugaidi (namna tulivyojipanga) na wimbi kubwa la ujambazi
5) Maoni yake kuhusu shinikizo la wananchi kutosaini mswada wa katiba mpya
6) Hatua maalum ilizozichukua serikali kupambana na biashara ya madawa ya kulevya.

...............
Hiyo namba NNE haiongelewi ovyo....Hata kenya iliwagharimu ....kusemasema ovyo kwa ole lenku
 
Back
Top Bottom