Zak Malang
JF-Expert Member
- Dec 30, 2008
- 5,404
- 234
Wanajamvi:
Habari kutoka vianzo vyangu vya habari (msiniulize ni vyanzo vipi) ni kwamba kuna uwezekano mkubwa kwa JK kuachana kabisa na wazo la Katiba mpya katika kipindi chake cha utawala kilichobakia.
Hii itatokea iwapo Bunge litakwamisha marekebisho ya Katiba yaliyopelekwa Bungeni. habari zilizozagaa ni kwamba Wabunge wa CCM, ambao ndiyo wengi wanasema wataukwamisha muswada huo wa marekebisho ya katiba kutokana na kutoafikiana na JK kuhusu posho, na pia kwa sababu eti marekebisho hayo yalitoka kwa viongozi wa CDM.
Habari zaidi zinasema baada ya JK kusaini ule Muswada wa awali, alipata shinikizo kubwa kutoka pande mbali mbali wakiwemo kwa wafadhili, kwamba Sheria ile haifai jinsi ilivyopitishwa na kwamba ni lazima ifanyiwe marekebisho ili kupata katiba iliyo bora, kwani hii ni nafasi pekee ya nchi kupata katiba iliyo bora kama kweli inataka kuepuka kukumbwa na machafuko hapo mbeleni.
Kwa hivyo iwapo marekebisho yatakataliwa, basi JK ataachana na ile sheria mama iliyopitishwa kwani hataishughulikia kwa maana ya kutoteuwa wajumbe wa kuratibu maoni na pia wajumbe wa Bunge la Katiba -- hivyo fursa yote itakuwa imepotea, naye atajikosha kwa wafadhili na wadau wengine kwamba yeye hana tena makosa isipokuwa Bunge.
Kulikuwapo hatua nyingine pia iwapo marekebisho hayatapitishwa, kulivunja Bunge na kuitisha uchaguzi mwingine, kama vile alivyofanya Mwl Nyerere mwaka 1973 Bunge lilipokataa kupitisha Sheria ya Kodi ya Mapato kuirithi ile ya iliyokuwa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki.
Hatua hiyo ya kuitisha uchaguzi mpya meonekana kuwa na gharama kubwa.