JK Huyoo Hispania! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK Huyoo Hispania!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Buchanan, Jul 19, 2010.

 1. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #1
  Jul 19, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  na Mwandishi wetu

  RAIS Jakaya Kikwete ameondoka nchini jana kwenda Hispania kuhudhuria mkutano wa kimataifa wa kujadili maendeleo ya Afrika na nafasi na wajibu wa siasa za kimaendeleo katika nchi za Afrika kusini mwa Jangwa la Sahara.

  Mkutano huo wa siku moja, unaojulikana kama The African Progress Conference, unafanyika leo kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Palacio de Congresos de Madrid, mjini Madrid.

  Akiwa huko, Rais Kikwete ataungana na viongozi wengine wa Afrika kujadili maendeleo ya Afrika katika mkutano huo wa aina yake kuandaliwa duniani.

  Miongoni mwa viongozi ambao wataungana na Rais Kikwete katika mkutano huo ni pamoja na mwenyeji wake, Rais Jose Luis Rodriguez Zapatero wa Hispania, Rais wa Cape Verde, Pedro Pires, Waziri Mkuu wa Ethiopia, Meles Zenawi, Naibu Rais wa Afrika Kusini, Motlanthe Kgalema na Rais wa zamani wa Jamhuri ya Liberia, Amos Sawyer.

  Mbali na kuhutubia mkutano huo utakaowashirikisha wanasiasa, watunga sera, wanazuoni na wasomi, wawakilishi kutoka taasisi zisizokuwa za serikali zinazojihusisha na kufikria jinsi gani ya kuharakisha maendeleo ya Afrika, Rais Kikwete pia atashiriki katika majadiliano ya mwisho ya mkutano huo.

  Washiriki wengine wa mkutano huo wanatoka nchi za Tanzania, Ghana, Ivory Coast, Cape Verde, Kenya, Uingereza, Afrika Kusini, Mali, Ethiopia, Ureno, Msumbiji, Senegal, Ubelgiji, Equatorial Guinea na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

  Akiwa huko, Rais Kikwete atakutana na kufanya mazungumzo na Mfalme wa Hispania, D. Juan Carlos wa Kwanza na Rais Zapatero.


  Source: Tanzania Daima
   
 2. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #2
  Jul 19, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Si ajabu baada ya siku chache tukaletewa picha alizopiga na timu ya Taifa ya Spain. akiwa anapeana mikona na wachezaji wa Spain.
   
 3. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #3
  Jul 19, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Anaweza akaja na "mkukuta" mpya!
   
 4. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #4
  Jul 19, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,289
  Likes Received: 22,054
  Trophy Points: 280
  Kaona waganga wa tanga , sumbawanga na bagamoyo hawana kitu kaenda kutest uchawi unaoleta makombe ya dunia
   
 5. Mkosoaji

  Mkosoaji JF-Expert Member

  #5
  Jul 19, 2010
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 363
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  kwi kwi kwi hii nimeipenda.
   
 6. Scientist

  Scientist JF-Expert Member

  #6
  Jul 19, 2010
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 392
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  nyie subirini soon tutaona kapiga picha kashika jezi ya Andres Iniesta!!!!!!
   
 7. W

  WildCard JF-Expert Member

  #7
  Jul 19, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Vumbi la Dk Bilal kule Dodoma halikuwa la kawaida. Anahitaji kupumua kidogo.
   
 8. h

  housta Senior Member

  #8
  Jul 19, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 160
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Spain don't have a President - Uandishi wa siku hizi,mmmmh!Inakuwa kama hakuna Cheif Editor.Mbona nchi nyingine zimetuma wawakilishi tu?S.A wenyewe wamemtuma VP....!Kweli Bongo tambarare!No one is asking hizi safari zina faida gani.Akitudanganya kuwa ameongea na Mfalme,anajua deficit ya Spain at the moment?Kutusaidia haitowezekana kwa sababu wao wana matatizo makubwa sana kwa sasa - unemployment,economy n.k.Kwa hiyo akituambia anatafuta misaada na uwekezaji,huo ni UONGO!!Inaleta hasira sana.
   
 9. W

  WildCard JF-Expert Member

  #9
  Jul 19, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Linaweza kuwa ni bandiko limetoka Ikulu na huyu "Mwandishi wetu" akalikopi na kulibandika kama lilivyo! Spain wana Waziri Mkuu ambaye juzi alionyesha jeuri ya kutokaa meza moja na Kagame wa Rwanda.
   
 10. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #10
  Jul 19, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Ghosh, My education International Relation/Politics is very poor. nilijua Hispania in Mfalme na waziri Mkuu ambaye ni Jose Luis Rodriguez Zapatero. Kumbe Zapatero ni Presidaa? I didnt know this.

  Hakuna editor hapo Tz Daima ?
   
 11. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #11
  Jul 19, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Hivi huyu mkulu wetu hawezi akamtuma hata Pinda, Shein etc ni lazima aende yeye tu kila siku?
   
 12. Rose1980

  Rose1980 JF-Expert Member

  #12
  Jul 19, 2010
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 5,701
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  hahahaha km ulikwepo kwenye mind yangu yan!!!!!!!!!!!!!!!!!!!1
  ata km atutaiona bt ni lazima ataenda kupata nao brkfast au dina ao wachezaji labda wamkatalie like we r sor mr presdnt we r lil tyt we dnt ave tym 4t!!!!!!!!!
  dah rais anapenda shangwe usipime bt its natural for any human being!!!!!!!
   
 13. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #13
  Jul 19, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Si anashindana na juniors wake kufukuzia posho? sasa awatume tena? hilo liposho atalipata saa ngapi?
   
 14. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #14
  Jul 19, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,289
  Likes Received: 22,054
  Trophy Points: 280
  bora mwandishi angemtaja raisi wa REAL MADRID
   
 15. Bantugbro

  Bantugbro JF-Expert Member

  #15
  Jul 19, 2010
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 2,684
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Lazima akamshuhudie PWEZA Paulo
   
 16. Iza

  Iza JF-Expert Member

  #16
  Jul 19, 2010
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,848
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Ikulu hawafanyi Fumigation nadhani kuna kunguni wanamtesa sana Mzee...?
  Bona cuento..!!
   
 17. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #17
  Jul 19, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  nafikiri huyu ana daftari lake anatia muhuri wa kila nchi anayokwenda akiwa rais....

  nafasi ya spain ilikuwa tupu ikabidi afanye haraka aijaze kabla ya uchaguzi
   
 18. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #18
  Jul 19, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 863
  Trophy Points: 280
  Miaka ya themanini kulikuwa na Waziri mmoja wa kike...; sikumbuki alikuwa Waziri wa nini. Mama huyu naye alikuwa anapenda sana trip za nje, alichotaka ni kijisababu chochote, yeye atatinga. Siku moja alikutana na waziri mmoja wa Nigeria akamwamabia nia yake ya kwenda kutembelea Nigeria, yule jamaa akamjibu yule mama casually tu kuwa "anakaribishwa." Mama kusikia vile, akafunga safari hadi Nigeria bila kuwa na mwaliko wowote wa kiserikali, mradi tu kuna waziri wa Nigeria alisema anamkariobisha. Jambo hilo lilileta tafrani sana ya kidiplomasia kwa sababu serikali ya Nigeria haikuwa na taarifa za ugeni huo, na wala balozi wa Tanzania huko Nigeria wakati huo (Mwasakafyuka???? -sikumbuki jina sawasawa) naye hakuwa na taarifa za kibalozi kuhusu ujio wa huyo mama. Unfortunately, mama yule baada ya kuadhjirika huko Abuja, akapaeleka malalamiko yake kwa Rais Mwinyi kuwa balozi wetu hakumtendea heshima, na kusabisha balozi yule kafukuzwa kazi.

  Rais wetu pia anapenda sana vitrip, anachohitaji ni kisababu tu cha kwenda huko hata kama kiwe kisababu kidogo namna ipi, yeye atakwenda tu. Kuna nchi nyingi zitakazoshiriki mkutano huo: Tanzania, Ghana, Ivory Coast, Cape Verde, Kenya, Uingereza, Afrika Kusini, Mali, Ethiopia, Ureno, Msumbiji, Senegal, Ubelgiji, Equatorial Guinea na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC). Ni Tanzania, Ethiopia na Cape Verde tu ndizo ambazo zimewakilishwa na viongozi wa nchi. Cape Verde inaeleweka kuwa ni koloni la zamani la hispania na kisiwa kinachoitegemea sana Spain kutokana na ujirani wake, kwa hiyo kiongozi wa Cape Verde kwenda Spain ni jambo la kawaida sana. Meresi Zenawi wa Ethiopia naye ni kama Kikwete tu. Zaidi ya hao wawili hakuna Rais mwingine wa Afrika aliyehudhuria mkutrano huo japo unahusu Afrika kwa sababu ni mkutano mdogo sana. Hebu angalia ratiba yao:


  Registration

  09h00 – 09h30
  Welcome address
  Jesús Caldera, Vice-president, IDEAS Foundation, Spain
  Elena Valenciano, Secretary for International Policy and Cooperation, PSOE, Spain
  Ebrahim Ebrahim, Deputy Minister, Department of International Relations and Cooperation/Head of African National Congress International Relations Department, South Africa

  09h30 – 10h30
  Opening panel :
  Elena Valenciano, Secretary for International Policy and Cooperation, PSOE, Spain
  Leire Pajín, Secretary for Organization, PSOE, Spain
  Manuel Chaves, Vice-President, Spain/ President of PSOE
  Kgalema Motlanthe, Deputy President, South Africa

  10h30 – 11h30
  The progressive agenda of Africa

  Speakers:
  Ebrahim Ebrahim, Deputy Minister, Department of International Relations and Cooperation/ Head of the African National Congress International Relations Department, South Africa
  Ousmane Tanor Dieng, General Secretary, Socialist Party/Chair of the Socialist International Africa Committee, Senegal
  Dr. Siphamandla Zondi, Director of IGD, South Africa

  Discussants:
  Paul Nugent, President of AEGIS, Europe
  Carlos Mulas, Director, IDEAS Foundation, Spain

  11h30 – 12h00
  Coffee Break


  12h00 – 14h00


  Towards sustainable economic growth and further equality in Africa
  Speakers:

  Ernst Stetter, Secretary General, FEPS, Belgium
  Basilio Ramos, Minister of Health/ Vice-president of African Party of Independence of Cape Verde, Cape Verde
  Modibo Diarra, Pathfinder Foundation/President Microsoft Africa, Mali
  Margaret Kamar, Member of Parliament, Orange Democratic Movement, Kenya

  Discussants:
  Patricia Mamonare Chueu, African National Congress Women League National Executive, South Africa
  Fernando Jorge Cardoso, Research Director and Head of the Africa Program at the Institute for Strategic and International Studies (IEEI)/ head of EARN, Portugal

  14h00 – 15h00

  Lunch

  15h00 – 17h00

  Migration, opportunities and inclusion
  Speakers:
  Juan Moscoso, Member of Parliament, PSOE, Spain
  Aminata Traoré, Scientific Committee of IDEAS Foundation/Director of Centre Amadou Hampaté Bâ, Mali
  Matlotleng Matlou, CEO, Africa Institute of South Africa (AISA)
  Joel Netshitenzhe, African National Congress National Executive Committee Member, South Africa

  Discussants:
  Colette Tshomba, Fr Vice Minister for Foreign Affairs, RDC
  Winnie Kathurima-Imanyara, Change & Strategy Director, Housing Finance, Rehani House, Kenya

  17h00 – 17h30
  Coffee break

  17h30 – 19h30

  Progressive Leaders´ Panel: Towards a new progressive political era in Africa
  Introduced by: Jesús Caldera, Vice-president, IDEAS Foundation, Spain
  José Luis Rodríguez Zapatero, President, Spain
  Jakaya Mrisho Kikwete, President, United Republic of Tanzania
  Pedro Pires, President, Republic of Cape Verde
  Meles Zenawi, Prime Minister, Federal Democratic Republic of Ethiopia
  Amos Sawyer, Former Interim President, Republic of Liberia
  Pascal Affi N'Guessan, President Ivorian Popular Front (FPI), Republic of Ivory Coast
  Kwabena Adjei, President National Democratic Congress (NDC), Republic of Ghana
  Ousmane Tanor Dieng, General Secretary, Socialist Party/Chair of the Socialist International Africa Committee, Republic of Senegal

  20h30 – 23h00
  Dinner for participants
  Jose Luis Rodriguez Zapatero ni Waziri Mkuu siyo Rais,
   
 19. O

  Ogah JF-Expert Member

  #19
  Jul 20, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  ....lol..............Prof.............kuna special invitation kwa president wetu aisee...........hapo hujamtendea haki JK kumlinganisha na yule Mama Waziri wetu..........kutokwenda kwa presidents wengine wa Afrika haina maana mkutano ule hauna uzito wa JK kuhudhuria.............
   
 20. C

  Chief JF-Expert Member

  #20
  Jul 20, 2010
  Joined: Jun 5, 2006
  Messages: 1,490
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Membe alishaahidi kueleza umma faida ya safari za JK, na sasa ni kama miaka miwili tangu atoe ahadi hiyo na bado hajatimiza.
   
Loading...