JK ataja sifa za viongozi waliofilisika kifikra

JK ataja sifa za viongozi waliofilisika kifikra

R.B

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2012
Posts
6,296
Reaction score
2,578
Rais Jakaya Kikwete jana alipuliza kipenga kuzindua Tamasha la Matumaini Dar es Salaam na kuwanyooshea kidole viongozi wa dini wanaohubiri siasa katika maeneo ya ibada akisema kufanya hivyo ni kufilisika kifikra.

Akizungumza muda mfupi kabla ya kupiga filimbi kuashiria ufunguzi wa tamasha hilo lililofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Rais Kikwete alisema ni jambo la hatari kwa Watanzania kukubali kugawanywa kwa misingi ya udini, rangi au maeneo wanakotoka.

Alitaka dini zitumike kuwaunganisha wananchi na siyo kuwagawanya akisema Watanzania wanakwenda makanisani na misikitini kusali na siyo kufanya siasa. Alisema kiongozi yeyote wa dini anayesisitiza waumini wake kuunga mkono chama chochote cha siasa amefilisika kifikra.

“Ni hatari tukigawanyika, ni lazima tuwaambie watu wanaotaka kutugawanya kwa misingi ya dini, rangi au maeneo tunakotoka kwamba hatutaki na wala hatukubali. Nchi hii wakoloni waliishindwa hivyo lazima tuendeleze utamaduni wa kukataa kugawanywa kwa msingi wowote ule,” alisema Rais Kikwete.

Aliwataka wanasiasa kuepuka kauli zenye kuchochea vurugu miongoni mwa wananchi wanapokuwa kwenye harakati zao za kisiasa akisema madaraka ya kisiasa yatafutwe kwa njia ya amani na siyo kuingiza kauli za uchochezi zenye kuwagawa wananchi.

“Nawaasa wanasiasa wasipandikize chuki za kidini au maeneo wanakotoka wananchi, kama ni madaraka yatafutwe kwa njia ya amani kwenye sanduku la kura,” alisema Rais. Alisema Tamasha la Matumaini liwe mfano wa kuigwa wa kutumia michezo kuwaunganisha watu badala ya kuwagawanya.

Alisema timu zilizotumbuiza jana zilimebeba majina ya Simba na Yanga, zimejumuisha wabunge kutoka vyama vyote ikionyesha kuwa wote ni wamoja licha ya tofauti za kisiasa.

Alipongeza mkakati wa waandaaji wa tamasha hilo ambao wametangaza kwamba mapato yatakayopatikana yatatumika kusaidia shule za sekondari katika mikoa minane nchini.
 
Huyu ndio Kikwete mtu anayependa kuongelea jambo kwa pande zote za mdomo.Anadhani tumesahau namna ulivyorudi madarakani?
 
Ana hoja nyepesi kwenye jipu alilolitunga na sasa limeiva linakaribia kulipukaaaa...

Yangu macho tu.
 
Profesa Lipumba amekiri kuwa yeye na JK walitumia udini kushinda uraisi 2010!
Aaache unafiki!! anataka afikishe miaka mingapi ndio ajitambue kuwa amekua??....

Kama ni kupandikiza chuki yeye ndie kinara..atueleze kweli serikali imeshindwa kuwapata walio watesa Ulimbokaa na Kibanda?? Kwanini akampandisha cheo Kamuhanda alieshiriki moja kwa moja kwenye mauaji ya Daudi Mwangosi, badala ya kumuadhibu??

Kumbe JK hataki kubadilika na yuko tayari kuiletea nchi hii machafukoee....atakuja kushangaa!!
 
Du atlast jamaa kajistukia,kwani huu upuuzi wa kufanya campaign kwenye sehemu za sala sizilikuwa mbinu chafu za CCM,kwenye uchaguzi wa 2010?sasa wanajidai kitu gani hapa?na infact Kikwete ndo alikuwa anatumia zaidi misikiti kufanyiwa campaign,hata juzi juzi mzee wa meno ya Tembo ameshaanza kupita pita sehemu nyingi akihubiri hilo tusisahauliane ndugu zangu,alafu kikwete unataka kumstonewash nani hapa?acheni usanii
 
Rais Jakaya Kikwete jana alipuliza kipenga kuzindua Tamasha la Matumaini Dar es Salaam na kuwanyooshea kidole viongozi wa dini wanaohubiri siasa katika maeneo ya ibada akisema kufanya hivyo ni kufilisika kifikra.

Akizungumza muda mfupi kabla ya kupiga filimbi kuashiria ufunguzi wa tamasha hilo lililofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Rais Kikwete alisema ni jambo la hatari kwa Watanzania kukubali kugawanywa kwa misingi ya udini, rangi au maeneo wanakotoka.

Alitaka dini zitumike kuwaunganisha wananchi na siyo kuwagawanya akisema Watanzania wanakwenda makanisani na misikitini kusali na siyo kufanya siasa. Alisema kiongozi yeyote wa dini anayesisitiza waumini wake kuunga mkono chama chochote cha siasa amefilisika kifikra.

“Ni hatari tukigawanyika, ni lazima tuwaambie watu wanaotaka kutugawanya kwa misingi ya dini, rangi au maeneo tunakotoka kwamba hatutaki na wala hatukubali. Nchi hii wakoloni waliishindwa hivyo lazima tuendeleze utamaduni wa kukataa kugawanywa kwa msingi wowote ule,” alisema Rais Kikwete.

Aliwataka wanasiasa kuepuka kauli zenye kuchochea vurugu miongoni mwa wananchi wanapokuwa kwenye harakati zao za kisiasa akisema madaraka ya kisiasa yatafutwe kwa njia ya amani na siyo kuingiza kauli za uchochezi zenye kuwagawa wananchi.

“Nawaasa wanasiasa wasipandikize chuki za kidini au maeneo wanakotoka wananchi, kama ni madaraka yatafutwe kwa njia ya amani kwenye sanduku la kura,” alisema Rais. Alisema Tamasha la Matumaini liwe mfano wa kuigwa wa kutumia michezo kuwaunganisha watu badala ya kuwagawanya.

Alisema timu zilizotumbuiza jana zilimebeba majina ya Simba na Yanga, zimejumuisha wabunge kutoka vyama vyote ikionyesha kuwa wote ni wamoja licha ya tofauti za kisiasa.

Alipongeza mkakati wa waandaaji wa tamasha hilo ambao wametangaza kwamba mapato yatakayopatikana yatatumika kusaidia shule za sekondari katika mikoa minane nchini.

Mzee wa kukata shingo naona sasa anapwaya huyu .Udini uko kwa Ilunga , Lipumba , Mwigulu , Membe na Lowasa kwa uwazi yaani uko CCM na hakuna hatua za dhati .Naona anakwepa kusema kwa nini hakwenda Arusha kwenye bomu la Olasiti na kutaja nani alirusha bomu mkutano wa Chadema .
 
Aisee!jamaa alikuwa rais kibahati mbaya, ianwezekana kabisa kuna mtu mwingine ndani yake, na wana peana zamu kujiendesha. Hivi kwani nini huyu jamaa ansadhani watanzania ni "Mapinda"?
 
Jamaa katutia kwenye wakati mgumu sana, Unafiki ni mapya saan!
 
vipi kuhusu 'mwanasiasa' anayepiga misele makanisani na misikitini?

alimzungumzia?
 
No doubt JK Hakuwa amejiandaa kuwa Rais...Jamaa aliipata nafasi ili tu kutimiza kuwa 1995 alikuwa nyuma ya Mkapa,so to make the law of series and sequence akachukua tena form....Ni kama amemuazima mtu ubongo!Anasahau alichokiongea na anakumbuka asichowahi kutenda
 
Jana nilishangazwa sana na tukio moja ambalo sikulitarajia kabisa. Baada ya Rais kikwete kukemea mambo ya Udini kwenye mambo yenye sura ya kitaifa ; mpira kati ya washabiki wa yanga na simba (wABUNGE) ulianza.Baada ya kipindi cha kwanza wachezaji walienda mapumziko.Kilichonishangaza ni pale nilipoona kikundi cha nyimbo za injili kikiingia uwanjani na kuanza kuimba injili hata nikajiuliza "Hivi hawa walikuwa mamemsikia Rais alichozungumza?" Kusema kweli hili liliniboa.Hivi kwa pale kulikuwa na haja gani ya kuingiza jambo lenye mtizamo wa kiudini?
 
JK na polisi wake ndio wavunja amani wakuu nchini. Hivi kipi ni rahisi kati ya kumkamata aliyemuua afande Balow wa Mwanza Usiku wa manane na aliyerusha bomu kwa mkono mchana kweupe kwenye umati wa watu arusha na polisi wakiwepo?
Yeye anawaona wahubiri tu? polisi wake kwa kuwa pengine ndiye anayewatuma anajitia upofu,
 
Aisee!jamaa alikuwa rais kibahati mbaya, ianwezekana kabisa kuna mtu mwingine ndani yake, na wana peana zamu kujiendesha. Hivi kwani nini huyu jamaa ansadhani watanzania ni "Mapinda"?

Mbona hilo linajulikana?!
 
Attachments

  • uploadfromtaptalk1373264965402.jpg
    uploadfromtaptalk1373264965402.jpg
    47.5 KB · Views: 255
Back
Top Bottom