JK ataja sifa za viongozi waliofilisika kifikra

JK ataja sifa za viongozi waliofilisika kifikra

waliofilisika ni pamoja na slaa,lipumba,sugu,lema nk
 
Rais Jakaya Kikwete jana alipuliza kipenga kuzindua Tamasha la Matumaini Dar es Salaam na kuwanyooshea kidole viongozi wa dini wanaohubiri siasa katika maeneo ya ibada akisema kufanya hivyo ni kufilisika kifikra.

Akizungumza muda mfupi kabla ya kupiga filimbi kuashiria ufunguzi wa tamasha hilo lililofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Rais Kikwete alisema ni jambo la hatari kwa Watanzania kukubali kugawanywa kwa misingi ya udini, rangi au maeneo wanakotoka.

Alitaka dini zitumike kuwaunganisha wananchi na siyo kuwagawanya akisema Watanzania wanakwenda makanisani na misikitini kusali na siyo kufanya siasa. Alisema kiongozi yeyote wa dini anayesisitiza waumini wake kuunga mkono chama chochote cha siasa amefilisika kifikra.

“Ni hatari tukigawanyika, ni lazima tuwaambie watu wanaotaka kutugawanya kwa misingi ya dini, rangi au maeneo tunakotoka kwamba hatutaki na wala hatukubali. Nchi hii wakoloni waliishindwa hivyo lazima tuendeleze utamaduni wa kukataa kugawanywa kwa msingi wowote ule,” alisema Rais Kikwete.

Aliwataka wanasiasa kuepuka kauli zenye kuchochea vurugu miongoni mwa wananchi wanapokuwa kwenye harakati zao za kisiasa akisema madaraka ya kisiasa yatafutwe kwa njia ya amani na siyo kuingiza kauli za uchochezi zenye kuwagawa wananchi.

“Nawaasa wanasiasa wasipandikize chuki za kidini au maeneo wanakotoka wananchi, kama ni madaraka yatafutwe kwa njia ya amani kwenye sanduku la kura,” alisema Rais. Alisema Tamasha la Matumaini liwe mfano wa kuigwa wa kutumia michezo kuwaunganisha watu badala ya kuwagawanya.

Alisema timu zilizotumbuiza jana zilimebeba majina ya Simba na Yanga, zimejumuisha wabunge kutoka vyama vyote ikionyesha kuwa wote ni wamoja licha ya tofauti za kisiasa.

Alipongeza mkakati wa waandaaji wa tamasha hilo ambao wametangaza kwamba mapato yatakayopatikana yatatumika kusaidia shule za sekondari katika mikoa minane nchini.
Safi sana Jk, wanafiki wa dini watakuwa wameupata ujumbe.
 
Ujumbe huu umfikie Prof.Lipumba na wale wote wanaomuunga mkono!
 
tumia miwani uongeze uoni utayaona mkuu.
nimeshatumia mpaka hadubini sioni kitu, pia nimekuuliza ktk moja ya post yangu huko juu unaelewa maana ya kiunganishi KAMA?
 
Hivi huwa ana kumbukumbu au ana tatizo la kukumbuka ?

hata haelewi unachosema. Nafikiri hii ni aina nyingine ya mipasho ... Afuate ushauri aliopewa na OBAMA kuhusu Demokrasia ya kweli mbali na hapo hakuna kingine zaidi ya kupiga duru muda uende serikali ibadilike ...
 
nimeshatumia mpaka hadubini sioni kitu, pia nimekuuliza ktk moja ya post yangu huko juu unaelewa maana ya kiunganishi KAMA?

Usitupotezee muda na mada zako za kiswahili cha kidato cha pili.
 
vipi! hakugusia ule msemo wake wa usipo kubali kuliwa nawe huli....
 
tunao wanasiasa uchwara wengi tu wengine mpaka wanatia aibu sana hawana kitu kabisa weupe pe mf...........
 
kuna mmbea huku jukwaani km wewe?
Jenga hoja siyo unakurupuka tu hata kama umetumwa siyo hivyo mkuu, hivi unataka kusema alichokisema JK ni uongo? Mbona tunawaona alina SLAA wanavyojaribu kurumia akina ASKOFU GWAJIMA kueneza upuuzi wao. Usifanye kuweka pamba masikioni.
 
Huwezi kutaona maendeleo yalitoletwa na JK kwa vile umepigwa upofu wa macho na propaganda za akina SLAA.

hapo kwenye red ulikuwa unataka kusema nini vile?wewe huoni umepigwa upofu wa macho na propaganda za akina mwigulu na daktari wa tembo?
 
aliendelea kusisitiza kuwa wenye mapembe lazima yakatwe tu.
 
Back
Top Bottom