JK aomba walimu toka Jamaica

JK aomba walimu toka Jamaica

Ni kweli usemavyo ndugu yangu, Jamaica ni wavuta bangi kuliko mahali popote labda kama anataka walimu wa reggae music. Umeona hali ya Mzumbe special school? Kwa mtaji huo ndani ya utawala wa CCM tuhesabu tumezikwa wakenya na waganda watatunyang'anya hata kazi za ulinzi.

Labda anataka waje kuwafundisha vijana wetu namna ya kupuliza JANI huku wakifanya Scientific experiments...

Kweli Rais tunae, anaenda kutafuta walimu Jamaica wakati vyuo tunavyo!! Hii tabia ya MaCCM ya kutoshugulisha ubongo zinapotokea changamoto na badala yake wanaenda kuomba kwa wazungu, ndio inafanya nchi izidi kuwa maskini. Kikwete changamoto ya ukosefu wa walimu wa sayansi suluhisho lake ni kujenga vyuo na kuwalipa vizuri walimu waliopo.
 
Jamaica tena? Au ndio after effects za kubembea? Hawa jamaa watatufundisha kula ndumu kwa staili mpya wakija!


Haaaaaahaaaa ama kweli ukiruka hatua fulani utototni utairudia ukubwani yaani JK anasafiri hadi Jamaica kwenda kubembea haaaaaaaahaaaaaaa daa nimecheka sana
 
kwl tunashida ila jmn hv vitu vya kuomba tuwe tunaangalia c kuomba omba tu!
 
kwl tunashida ila jmn hv vitu vya kuomba tuwe tunaangalia c kuomba omba tu!

Wakija tuwagomee na tusiwape ushirikiano wowote pumbavu sana huyu jamaa nadhani anavuta sana bangi...kila mahali scandal haziishi sijui kama tutavuka salama
 
Mimi sishangai hili
OMBI...Lakini nitakachoshangaa ni kama NCHI yetu bado Watu wanajifanya
kwamba hawajui ni NAMNA GANI YA KUWAPATA WALIMU WA MASOMO YA SAYANSI
Kuletewa walimu toka Jamaica sio suluhisho ZURI!
Ni kweli tuna TATIZO LA KUSULUHISHWA HARAKA ili tuweze kupata Walimu wa
Sayansi.

Tatizo ni kwamba Nchini mwetu,kuna Watu wamekaa na kujifanya hawajui
kwamba kuna tatizo la masomo ya Sayansi kuogopwa na Vijana/watoto
wengi;hivyo zinahitajika jitihada za makusudi kabisa kabisa ili kuweza
kuokoa jahazi.
Ukweli ni kwamba🙁Uso nimeukunja hapa,utake usitake)
1.Sayansi ni NGUMU zaidi ya ART
2.Kuanzishwe Olimpiki za masomo ya Sayansi mashuleni,watoto wengi zaidi
wavutwe kupenda sayansi kama vile kuwapa zawadi na medali wale
wanaofaulu vema masomo ya sayansi
3.Watu wahimizwe kusoma sayansi kuanzia form 2,wanaofaulu masomo ya
Sayansi vizuri wapewe zawadi ikiwezekana hata kulipiwa ada
4.Waalimu wa Sayansi wapewe upendeleo maalumu sehemu yeyote wanayopangwa

Hii yote itasaidia hawa watu kuigwa....Watoto mashuleni watajua kwamba
kusoma Sayansi vema ama nikiwa Mwalimu Sayansi mambo yangu yatakuwa sio
haba.
Siku hizi kila mtu anataka awe Mwanasiasa...Kwanini?Kwa sababu Siasani
ndio kuna motivation zote hizo...hela nzuri,gari nzuri,maisha
mazuri.,....nani hataki hayo maisha?halaf ubaya ni kwamba kila kukicha
sie pamoja na watoto tunasikia wanasiasa wengi hata hawajasoma...kumbuka
zama hizi sio kama zamani ambapo information kama hizi ilikuwa ngumu
kuzipata,na hata magazeti ya Chama hayakuwa yanandika,na wengine
tuliokuwa vijijini enzi hizo mnasubiri magazeti ya wakatoliki ya
Kiongozi ambayo yana makala za Mbunda msokile as a hot topic
kwishneeey....sala kibwaaao!
Ninakumbuka Baba yangu enzi hizo nilimuuliza kama nataka "U- Nyerere@
nifanyeje,yeye akaniambia ni lazima niwe wa kwanza darasani kuanzia
darasa la kwanza mpaka la saba!niliamini hivyo....mwambie mtoto wa siku
hizi hayo!Looo

Watu wameanza kutoka Kozi za Sayansi(Ma engineer,Madaktari wanasoma
MBA,Bcom---maksi zao za nyuma zinawaruhusu,i mean za Alevel),kwa sababu
wanagundua late kwamba waliingia chaka kuchagua Kozi ambazo zina "sifa
za Kijinga"...sifa nyingi halafu unaponda kwa mguu,wakati yule uliyekuwa
unamcheka enzi hizo kwamba anasoma "art",leo hii anakwambia "Pole Bwana
Mkubwa hebu nikufikishe mbele kidogo"?

Unajua tatizo linakuja kwamba mechanism ya kuwapata walimu ni ya aina
yake.....wale watu ambao hawajafaulu vizuri,ndio wanaochukuliwa kwenda
Ualimu.....na mara nyingi unakuta kwamba watu wanaojiweza kwenye
science,in one way or the other hata masomo mengine wanayaweza...lakini
watu wasioiweza sayansi,hakuna guarantee kwamba wanaweza hata masomo
mengine,ni either hawayawezi yote,ama wanaweza ya Art tu....hivyo ni
bora kuwakazania wanafunzi wakiwa bado wadogo wasiiiogope sayansi,kwani
inahitaji nguvu za ziada kuweza kufanya watoto waipende....art watajua
tu njiani,lakini huwezi ukawaacha ukasema sayansi wataijua njiani.

Ni lazima Sayansi itambuliwe kama Special subjects zinazohitaji special
treatment,iki involve programe,na washika dau wake,yaani walimu wa
sayansi na wanafunzi wanaopenda sayansi

Unless tutaendelea kujificha vichwa udongoni na kuacha i kibinda nkoi
iko nje,tukidhani kwamba hatuonekani,kumbe sie ndio hatuoni
kinachoendelea.....Kuwapata walimu wa sayansi sio mchezooooo,kunahitaji
gharama na nguvu ya ziada isiyohitaji aibu ya kwamba "tutakuwa
tunawatenga ama kuwadhalilisha waalimu wa makundi masomo mengine"

Am out

inabidi tuwe na maabara kwanza katika shule zetu za msingi .ninafikiri vijana wengi watavutiwa na masomo ya sayansi, kwani sayansi ni rahisi sana ukiiso kwa nadharia navitendo. sayansi inahitaji vitendo zaidi.
 
sisi wana taaluma tunalalamika kilasiku juu ya, ubakaji wa kanuni na taratibu za elimu hapa nchini zinazo fanywa na wana siasa, tunameona madhara mengi waliyo yafanya hawa wenzetu juu ya uvurugaji wa taaluma kwa kubadilisha maitaala ya eleimu na ukurupukaji wa kutoa matamuko yahusuyo elimu, pasipo kushirikisha wataalamu wa liopo na walio watendaji wa kuu,tuna mifano juu ya wanasiasa kama mungai wanaokaa na wakezao nakuja na maamuzi kanakwamba wamekaa na watalau na kuchambua na kupata mwafa , ukweli mimi husema najuta kuwqa MTANZANIA ivisisi tumerogwa?????, huyumuheshimiwa kila aendako lazima aombe misaada?????? ukweli anatutia aibu, hivi jamaika mfumo wa elimu yao unatofauti na sisi?????,tunawataalamu kibao wa masomo hayo kwanini wasipewe motisha wakapewa kazi tuone je wameshindwa????,tatizo la nchi hii na serikari yake wanaona walimu ni kama watumishi walio kosa dira hivyo wanastahili kupewa mishaha kidogo namengi ya kusema ila naishia hapa ,mungu tusaidie huyu mutu amalize kipindi chake salama akapumuzike msoga,mungu tupe rais 2015 mwenyekuguswa na matatizo shida za watanzania.mungu ibariki africa mungu wabaliki tanzania na watu wake.
 
somo la reggae music liingizwe kwenye mtaala plz na bado aombe na mateacher toka mexico nasikia ni wazuri sana kwa marijuana
Huyu jakaya anaumwa haki ya nani so bure... Anaweza akaomuomba hadi matonya
 
Umeambiwa ni wa hisabati na sayansi@filbonde
 
Nafikiri itakuwa zaidi ya mara 10. Hawa jamaa sio wajinga. Watataka mkataba uwepo na sitoshangaa mkataba ukijumuisha, nyumba, gari, mafuta, nauli kutoka kwao na kurudi, matibabu wanapougua, pamoja na mshahara in US$.

That will be 10 times more!
 
Hii kali wapite nchi zoooooteeeee kuja TZ kwa mshahara na makazi gani?

Aibu jamani as wa kwetu hawasikilizwi.
 
kitendo cha rai kuomba walimu toka nje bila kujali wanatoka wapi au nini ni AIBU SANA\

tuna zaidi ya raia milioni arobaini, natural resources, stable government etc for over 50 years............. leo tunaomba taifa dogo kama wilaya moja hapa nyumbani ni aibu
 
Tabia ya kuombaomba ni ugonjwa ambao uko ndani ya damu ya mtu. Kuna watu ambao wako tayari kuomba hata maji machafu mradi tu wawe wameomba.

I think one thing that fantasize JK is "Kuombaomba." This is tooooooooooooooooooo much.

Lets assume that we really need help in Math and Science (which is not true)

Maswali ambayo nimejiuliza baada ya kuona hii habari ni:

1. Je, J.K alishauriana na wadau wa elimu kabla ya kuomba huu msaada?
2. Je J.K alishauriana na vyuo vikuu na vya ualimu kabla ya kuomba msaada?
3. Je J.K alishauriana na hazina kuona kama kuna fungu la kuwalipa hawa waalimu?

4. Kama J.K aliyafanya yote hapo juu, je huu mkataba utakuwa wa miaka mingapi?
5. Je ameweka mkakati gani wa kuhakikisha kuwa baada ya muda huo tutaweza kujitosheleza?

6. Kama hii itaenda through, itabidi aombe na waalimu wa English kutoka hukohuko Jamaica kwani wanafunzi hawataelewa English ya WaJamaica. Let me tell you, it is rough and they don't give a rat!

Solution:
Lipa waalimu wetu mshahara unaostahili, boresha mazingira yao ya kazi na makazi na pia waendeleze kielimu. Mwalimu wangu aliyenifundisha hesabu primary (sasa anafundisha chuo) alinifanya nipende hesabu kwa umahiri wake. Tunao wengi tu hapa Tanzania ila J.K na CCM yako mnawapuuza.

This makes me sick!
 
Hii ni aibu isiyostirika wala kumithilika. Miaka 50 plus baada ya kupata uhuru bado unchi kama nchi imeshindwa kuzalisha walimu wa kutosha kwa ajili ya kufundisha kwenye shule zake? Ni Rais huyuhuyu mwaka 2010 alisema kuwa kufikia 2012 uhaba wa walimu nchini utakuwa historia, leo hii ameenda kuomba Jamaica? Tutafikia mahala tutaanza kuomba hata wanaume kuwatimizia wake zetu
MAdhara ya chama chashika hatamu ni mabaya hata kupita mpigane vita wenyewe kwa wenyewe. Kikwete sio wa kulaumiwa ila wale walioleta ualimu wa Upem na kujenga mavyuo ya siasa kigamboni, hombolo na handwani na mikumbi ya mikutano ya chimwaga! pesa hizo zingetosha kuelimisha wataalamu wa hsesabu na sayansi badala ya kusomesha makada wa siasa!
 
janga anaomba walimu waje na bembea sio?
 
Huku Tunakoenda siko kabisa wakuu wa meza.
Jamaica ni kama kisiwa chetu cha ukerewe tu na ni masikini. Sisi nchi tajiri bila aibu tunaenda kuomba msaada kwenye nchi masikini, what a shame. kocha wa riadha kweli bongo hakuna??????
Duh hii ni kali:embarassed2:
 
...Huu utumwa wa kuombaomba huu ni mbaya sana na aibu kubwa kwa taifa......japo huko anakoomba hawasemi.....Unaomba waalimu Jamaica wakati waalimu wazalendo ulionao TZ unashindwa kuwahudumia!!.....alafu nchi yenyewe Jamaica!!.....Utajiri ilionao nao TZ si wa kwenda kuombaomba waalimu Jamaica...hii ni aibu kubwa.....

.....Wale waalimu wachache ulionao TZ unashindwa kuwahudumia ipasavyo....alafu unaenda kuomba wengine nje ya nchi....hii tuite nini hii?.....hivi kweli TZ ya leo inashindwa kujitosheleza kwa waalimu wa level ya secondary?....na uwepo wa vyuo vikuu vyooote kweli!!.....
 
Back
Top Bottom