Dr Ntinkutina.
JF-Expert Member
- Apr 25, 2013
- 309
- 55
Mkuu hata mimi hiyo imenishangaza sana au alikuwa ill adviced hata sielewi, JK mwenyewe kasoma economics kwa hiyo hata somo la hesabu inaliweza sana akipata muda wa kujitayarisha, huo ulikuwa ni utangulizi wangu kwanza - sasa tuje kwenye masoma ya HESABU na FISIKIA/SAYANSI raia walio somea fani ya Engineering wote wanayamudu masomo hayo kwa ufanisi mkubwa sana, mkuu Watanzania wana uwezo mkubwa sana katika masomo hayo wakipewa motisha wa kutosha.
Mimi nina mfano hai, nilibahatika kwenda kusoma katika nchi za magharibi shahada yangu ya kwanza ya Engineering enzi hizo, kitu kilicho washangaza Wazungu ni uwezo mkubwa wa Watanzania katika kumudu somo la Hesabu, na si hisabati tu hata fisikia na kemia - wanafunzi kutoka Kenya, Uganda, Zambia nk walikuwa awaoni ndani - hapo ndipo nilikuja gunduwa kwamba Kambarage alikuwa mahiri katika suala la Elimu nchini na alikuwa anawapa walimu motisha wa kutosha na walikuwa na nidhamu ya hali ya juu kweli kweli.
Mimi nashauri kitu cha kufanya ni kumueleza Waziri wa Elimu Mh.Kawambwa ajaribu kuwasiliana na ma Engineeer nchini ambaoa wako kazini na wale walio staafu, alafu ajaribu kuwasikiliza wanaweza kusaidia kivipi katika masomo hayo muhimu ya kisayansi - unajua mambo mengine unapaswa kuwa mbunifu wakati mwingine; wajaribu kumuhiga Mh.Mwakyembe - mambo mengine mengi Watanzania tuna uwezo wa kuyatatua sisi wenyewe bila ya kutegemea nchi za nje - ukosefu wa UBUNIFU na kutojiamini ndio naona ndilo tatizo kubwa nchini, chukulia suala kama hili la ukosefu wa walimu wa hisabati na sayansi kwani walikuwa awajuhi kwamba ma Engineer wanaweza kusaidia katika HILO??
Mkuu unaona mbali, chamsingi ni kuboresha mishahara ya walimu pia. Kwani walimu wapo isipokuwa wengine wameamua kuwa ma-tellers ktk mabenki. Ualimu umekuwa na maslahi duni sana.