JK aomba walimu toka Jamaica

JK aomba walimu toka Jamaica

Nitakachosikitika ni pale hao Mwl toka Jamaica atakuwa analipwa mara 4 ya huyu wa Tz ingawa huyu atakuwa nafanya kazi nzuri kuliko huyo mgeni. Yangu macho.
Atoke kwao kuja kulipwa mara nne ya mwalimu wa kitanzania? Mbona itakuwa pesa ndogo sana kumtoa mtu Jamaica kuja huku. Tupo tayari kuwalipa hao wageni mara 30 kuliko kuwawezesha walimu ndugu zetu. Roho mbaya za wakuu wetu.
 
Nitakachosikitika ni pale hao Mwl toka Jamaica atakuwa analipwa mara 4 ya huyu wa Tz ingawa huyu atakuwa nafanya kazi nzuri kuliko huyo mgeni. Yangu macho.

Kama hayo ni ya ukweli, kichwa cha JK kinaweza kuwa na matatizo kwenye kufikiri na kutafakari, kibaya zaidi ndiye mtu mwenye maamuzi ya mwisho katika nchi yetu.
Mtu mwenye kutafakari vizuri hawezi kuomba walimu kutoka Jamaica.
TZ walimu tunao wengi tu. Hata kwenye nchi zilizoendelea mwalimu sio yule tu aliyeenda chuo cha ualimu, mtu mwenye degree nzuri ya chuo akipewa kozi fupi (3months) ya jinsi ya kuelewesha wanafunzi anakuwa mwalimu mzuri tu.
Anachotakiwa kufanya JK ni kuhakikisha walimu wanapata mishahara katika muda muafaka na pia atangaze mishahara ya kueleweka kwa walimu.
 
Haaaa ukistahajabu ya shibuda utayaona ya JeiKei lol Hivi wale madktari wa jeikei wa cuba aliwaleta? Ya nin jamaic wakt sie 2na walimu kibao hawana ajira,aboreshe maslah ya walimu tu.
 
Last edited by a moderator:
Nitakachosikitika ni pale hao Mwl toka Jamaica atakuwa analipwa mara 4 ya huyu wa Tz ingawa huyu atakuwa nafanya kazi nzuri kuliko huyo mgeni. Yangu macho.

Ikiwa hivyo hali itakuwa mbaya zaidi kwa kuwa walimu wazawa waliopo will lay down tools unless wawe wanalipwa sawaswa au karibu na sawa. Yangu macho.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Hao walimu wa kitu gani maana yawezekana walimu lkn ikawa wa kujifunza kutengeneza umeme mbadala,km walimu wa shule kwajili ya masomo tu atachemka sana wakati walimu anao wengi tu na wengine kushindwa ht kuwaaajiri.
 
Nitakachosikitika ni pale hao Mwl toka Jamaica atakuwa analipwa mara 4 ya huyu wa Tz ingawa huyu atakuwa nafanya kazi nzuri kuliko huyo mgeni. Yangu macho.

Mimi sishangai hili OMBI...Lakini nitakachoshangaa ni kama NCHI yetu bado Watu wanajifanya kwamba hawajui ni NAMNA GANI YA KUWAPATA WALIMU WA MASOMO YA SAYANSI
Kuletewa walimu toka Jamaica sio suluhisho ZURI!
Ni kweli tuna TATIZO LA KUSULUHISHWA HARAKA ili tuweze kupata Walimu wa Sayansi.

Tatizo ni kwamba Nchini mwetu,kuna Watu wamekaa na kujifanya hawajui kwamba kuna tatizo la masomo ya Sayansi kuogopwa na Vijana/watoto wengi;hivyo zinahitajika jitihada za makusudi kabisa kabisa ili kuweza kuokoa jahazi.
Ukweli ni kwamba🙁Uso nimeukunja hapa,utake usitake)
1.Sayansi ni NGUMU zaidi ya ART
2.Kuanzishwe Olimpiki za masomo ya Sayansi mashuleni,watoto wengi zaidi wavutwe kupenda sayansi kama vile kuwapa zawadi na medali wale wanaofaulu vema masomo ya sayansi
3.Watu wahimizwe kusoma sayansi kuanzia form 2,wanaofaulu masomo ya Sayansi vizuri wapewe zawadi ikiwezekana hata kulipiwa ada
4.Waalimu wa Sayansi wapewe upendeleo maalumu sehemu yeyote wanayopangwa

Hii yote itasaidia hawa watu kuigwa....Watoto mashuleni watajua kwamba kusoma Sayansi vema ama nikiwa Mwalimu Sayansi mambo yangu yatakuwa sio haba.
Siku hizi kila mtu anataka awe Mwanasiasa...Kwanini?Kwa sababu Siasani ndio kuna motivation zote hizo...hela nzuri,gari nzuri,maisha mazuri.,....nani hataki hayo maisha?halaf ubaya ni kwamba kila kukicha sie pamoja na watoto tunasikia wanasiasa wengi hata hawajasoma...kumbuka zama hizi sio kama zamani ambapo information kama hizi ilikuwa ngumu kuzipata,na hata magazeti ya Chama hayakuwa yanandika,na wengine tuliokuwa vijijini enzi hizo mnasubiri magazeti ya wakatoliki ya Kiongozi ambayo yana makala za Mbunda msokile as a hot topic kwishneeey....sala kibwaaao!
Ninakumbuka Baba yangu enzi hizo nilimuuliza kama nataka "U- Nyerere@ nifanyeje,yeye akaniambia ni lazima niwe wa kwanza darasani kuanzia darasa la kwanza mpaka la saba!niliamini hivyo....mwambie mtoto wa siku hizi hayo!Looo

Watu wameanza kutoka Kozi za Sayansi(Ma engineer,Madaktari wanasoma MBA,Bcom---maksi zao za nyuma zinawaruhusu,i mean za Alevel),kwa sababu wanagundua late kwamba waliingia chaka kuchagua Kozi ambazo zina "sifa za Kijinga"...sifa nyingi halafu unaponda kwa mguu,wakati yule uliyekuwa unamcheka enzi hizo kwamba anasoma "art",leo hii anakwambia "Pole Bwana Mkubwa hebu nikufikishe mbele kidogo"?

Unajua tatizo linakuja kwamba mechanism ya kuwapata walimu ni ya aina yake.....wale watu ambao hawajafaulu vizuri,ndio wanaochukuliwa kwenda Ualimu.....na mara nyingi unakuta kwamba watu wanaojiweza kwenye science,in one way or the other hata masomo mengine wanayaweza...lakini watu wasioiweza sayansi,hakuna guarantee kwamba wanaweza hata masomo mengine,ni either hawayawezi yote,ama wanaweza ya Art tu....hivyo ni bora kuwakazania wanafunzi wakiwa bado wadogo wasiiiogope sayansi,kwani inahitaji nguvu za ziada kuweza kufanya watoto waipende....art watajua tu njiani,lakini huwezi ukawaacha ukasema sayansi wataijua njiani.

Ni lazima Sayansi itambuliwe kama Special subjects zinazohitaji special treatment,iki involve programe,na washika dau wake,yaani walimu wa sayansi na wanafunzi wanaopenda sayansi

Unless tutaendelea kujificha vichwa udongoni na kuacha i kibinda nkoi iko nje,tukidhani kwamba hatuonekani,kumbe sie ndio hatuoni kinachoendelea.....Kuwapata walimu wa sayansi sio mchezooooo,kunahitaji gharama na nguvu ya ziada isiyohitaji aibu ya kwamba "tutakuwa tunawatenga ama kuwadhalilisha waalimu wa makundi masomo mengine"

Am out
 
Yes class, iz evibadi ina di clas?
We gwan learn somting nu today!
..................................
...sd#$%fgdg^YTY..
..................................
Whoz gat weed in here, me iz thursty!

:bange::bange::bange::bange::bange::bange::bange::bange:

Jah Bless!

Hahahaha, tunaomba mno, kila kitu tunaombaomba tu
Cha muhimu sasa naona tumwombe Xi Jinping atusaidie kuongoza mwaka mmoja tuone kama tunaweza kupiga hatua!
Design hii ole wako uwacheleweshee mshahara! Ndo utajuwa utamu wa ndumu!
 
Zigg marle bob marle nesta marle msuba msuba tu yan huko mwalim ndum dent ndum jamica B
 
JK badala ya kupoteza hela zetu za kodi kwa kuwaleta hao Wajamaika hebu fanya hivi.Fanya overall systematic reforms on education kwa kuanzisha matumizi ya intelligence testing[psychological testing] wakati wanapotaka kujiunga na shule kuanzia elimu ya chini kabisa,Hii ni mbinu ya kuaminika kama mnataka kuwapata watoto wenye kulimudu somo la hisabati na mengineyo vyema.Na utaratibu huo muendelee kuutumia katika ngazi mbali mbali za kielimu ili pia kuwasaidia wale waliopotea njia kwa kuwepo katika kozi wasizozimudu na kuwarudisha katika mstari.Hapa nazungumzia kuhusu kuwawaandaa walimu wa hisabati makini na sahihi wa kesho.Pia motisha kwa walimu wa Sayansi iboreshwi ili kuwatia moyo na hari walimu waliopo wafundishe vizuri.Lakini pia methodologies zinazotumiwa na walimu kufundishia wanafunzi zibadilishwe.Ningepelea kuona wanafunzi wanapewa madaraka zaidi katika process za kujifunza darasani hasa wale walioko katika madasa ya juu hii itawasaidia kuongeza udadisi wao wa mambo na kujifunza mambo mengi zaidi.
 
Walimu wa kuifundisha TOT labda, mawazo kapata kwa Komba
 
miaka 50 ya uhuru umeshindwa kuzalisha hata waalim
au anataka waalimu wa rege kwa kuwa baba mwanaisha naye
ana vituko vyake.
 
Kwani Tanzania walimu wa hisabati na sayansi hawapo? wapo wengi tu! Waliosoma fani za uhandisi wote wangeweza kuwa walimu wa masomo hayo km kungekuwa na maslahi mazuri na mazingira bora ya kufundishia..

Mkuu hata mimi hiyo imenishangaza sana au alikuwa ill adviced hata sielewi, JK mwenyewe kasoma economics kwa hiyo hata somo la hesabu inaliweza sana akipata muda wa kujitayarisha, huo ulikuwa ni utangulizi wangu kwanza - sasa tuje kwenye masoma ya HESABU na FISIKIA/SAYANSI raia walio somea fani ya Engineering wote wanayamudu masomo hayo kwa ufanisi mkubwa sana, mkuu Watanzania wana uwezo mkubwa sana katika masomo hayo wakipewa motisha wa kutosha.

Mimi nina mfano hai, nilibahatika kwenda kusoma katika nchi za magharibi shahada yangu ya kwanza ya Engineering enzi hizo, kitu kilicho washangaza Wazungu ni uwezo mkubwa wa Watanzania katika kumudu somo la Hesabu, na si hisabati tu hata fisikia na kemia - wanafunzi kutoka Kenya, Uganda, Zambia nk walikuwa awaoni ndani - hapo ndipo nilikuja gunduwa kwamba Kambarage alikuwa mahiri katika suala la Elimu nchini na alikuwa anawapa walimu motisha wa kutosha na walikuwa na nidhamu ya hali ya juu kweli kweli.

Mimi nashauri kitu cha kufanya ni kumueleza Waziri wa Elimu Mh.Kawambwa ajaribu kuwasiliana na ma Engineeer nchini ambaoa wako kazini na wale walio staafu, alafu ajaribu kuwasikiliza wanaweza kusaidia kivipi katika masomo hayo muhimu ya kisayansi - unajua mambo mengine unapaswa kuwa mbunifu wakati mwingine; wajaribu kumuhiga Mh.Mwakyembe - mambo mengine mengi Watanzania tuna uwezo wa kuyatatua sisi wenyewe bila ya kutegemea nchi za nje - ukosefu wa UBUNIFU na kutojiamini ndio naona ndilo tatizo kubwa nchini, chukulia suala kama hili la ukosefu wa walimu wa hisabati na sayansi kwani walikuwa awajuhi kwamba ma Engineer wanaweza kusaidia katika HILO??
 
  • Thanks
Reactions: KUN
Yes class, iz evibadi ina di clas? We gwan learn somting nu today! .................................. ...sd#$%fgdg^YTY.. .................................. Whoz gat weed in here, me iz thursty! :bange::bange::bange::bange::bange::bange::bange::bange: Jah Bless! Hahahaha, tunaomba mno, kila kitu tunaombaomba tu Cha muhimu sasa naona tumwombe Xi Jinping atusaidie kuongoza mwaka mmoja tuone kama tunaweza kupiga hatua!

Mkuu CYBERTEQ naona umepania kutuvunja mbavu kwa vicheko!! Yaani nimecheka karibu nikate roho - unajua kuna mambo mengine yanatia simanzi SANA, kuona nchi za wenzentu zinapaa kimaendeleo kutokana kuchukulia nyanja ya Elimu Seriously mfano China, wanafunzi nilio kuwa nasoma nao wote walirudi kwao China na kuendeleza nchi yao, matokeo yake sasa hivi China itakuwa na uwezo wa kuhipiku Merikani kiuchumi siku si nyingi, sisi tunabaki kwenye ngonjera na tamthilia na malumbano ya kisiasa! Oh yes mambo ya siasa yamekwisha kuwa deal i.e yanapewa kipa umbele kuliko kitu kingine hapa nchini, we jiulize kwa nini ma Profesa wanahamua kuachana na chaki na kukimbilia siasa! Hawataki kuwa condemmed to abject poverty maisha yao yote - nani anaweza kuwalahumu?
 
anpenda kuomba huyuuuuuuuuuuu............!
sasa tengeneza vyako anzia vyandrua mpaka walimu
 
Tabia ya kuombaomba ni ugonjwa ambao uko ndani ya damu ya mtu. Kuna watu ambao wako tayari kuomba hata maji machafu mradi tu wawe wameomba.

Kichuguu nasoma huu uzi siamini kama kweli chief nanga kaomba walimu kutoka jamaica?! Nadhani alikuwa anatania,ilikuwa ni utani tu,si unajua chief akiona madem.ili jamaa bure kabisa
 
This must go beyond the shame to our country to ask experts in a country thats not equal even with a district of kahama.
 
Back
Top Bottom