JK aomba walimu toka Jamaica

JK aomba walimu toka Jamaica

JK aomba walimu toka Jamaica

Na Mwandishi wetu
Jumatano 29 Mei, 2013

RAIS Jakaya Kikwete ameomba msaada wa walimu wa Hisabati na Sayansi kutoka nchini Jamaica ili kukabiliana na upungufu wa wataalam hao nchini.

Rais Kikwete alitoa ombi hilo juzi kwenye Hotel ya Sheraton mjini Addis Ababa, Ethiopia wakati wa mkutano wake na Waziri Mkuu wa Jamaica, Mama Portia Simpson Miller.

Ikulu ilisema kuwa Rais Kikwete alikuwa Addis Ababa kuhudhuria sherehe za miaka 50 tokea kuanzishwa kwa Umoja wa Afrika, Juni 25, 1963 na Mkutano wa 21 wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa AU wakati Mama Simpson Miller alipokuwa mmoja wa viongozi mashuhuri wa nchi mbali mbali duniani walioalikwa kuhudhuria sherehe hizo.

Taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu iliyosambazwa jana kwa vyombo vya habari, ilisema kuwa katika mazungumzo ya viongozi hao wawili, Mama Portia Simpson Miller ambaye aliapishwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamaica Januari 5, 2012 baada ya chama chake cha Peoples National Party (PNP) kushinda uchaguzi mkuu nchini humo, alimwuliza Rais Kikwete jinsi gani Jamaica inavyoweza kuisaidia Tanzania.

Kutokana na swali hilo, Rais Kikwete aliomba mambo mawili, mosi kupatiwa walimu wa masomo ya hisabati na sayansi pamoja na kocha wa riadha.
“Mawili makubwa ambayo mnaweza kutusaidia, moja ni walimu wa hisabati na masomo ya sayansi kama mnao wa kutosha na pia kocha wa riadha ili tuweze kufufua upya mchezo huo ambao Tanzania ilikuwa inatamba nao duniani katika miaka ya 1970,” alisema Rais Kikwete.
Kutokana na ombi hilo, mama huyo alimwahidi Rais Kikwete kuwa Jamaica ina uwezo wa kusaidia katika maeneo yote mawili.

“Hili la walimu tutaliangalia mara moja nikirejea nyumbani. Tutasaidia kwa kadri inavyowezekana kwa sababu najua fika juhudi zako kubwa ambazo umekuwa unafanya katika eneo hili la elimu na mafanikio makubwa ya jitihada zako.”

Kutokana na makubaliano hayo, serikali sasa inatarajiwa kupata walimu wa masomo hayo mawili na kocha wa mchezo wa riadhaa. Hata hivyo taarifa hiyo haikutaja idadi ya walimu wa masomo hayo.

Katika matokeo ya kidato cha nne na sita, kumekuwa na idadi kubwa ya wanafunzi wanaofeli masomo hayo kwa madai kuwa walimu wanaoweza kufundisha masomo hayo ni wachache.
Lakini kibaya zaidi wataalam wa masomo hayo licha ya uchache wao, hawana motisha na ndio sababu yao kutofundisha vizuri na kusababisha matokeo mabaya katika masomo hayo.

Mbali ya makubaliano hayo, nchi hizo mbili zimeahidi kuongeza ushirikiano katika nyanja mbalimbali na kuangalia uwezekano wa Tanzania kufungua aina ya uwakilishi katika Kisiwa hicho cha Caribbean katika miaka miwili ijayo.

Kuhusu kocha wa riadha, Mama Simpson Miller amesema kuwa na hilo halina pingamizi kwa sababu yeye alikuwa Waziri wa Michezo kwa miaka mingi na kuwa kwa sasa Wizara ya Michezo iko kwenye Ofisi yake ya Waziri Mkuu.

“Nilikuwa waziri wa miaka mingi wa michezo katika nchi yangu na kwa sababu ya umuhimu wa michezo, nimeamua kuiweka shughuli ya michezo katika Ofisi yangu ya Waziri Mkuu.”
Jamaica ni moja ya nchi zinazoongoza katika mchezo wa riadha duniani ikiwa imetoa wanariadha wengi mabingwa wa dunia akiwamo bingwa wa sasa wa Olimpiki na dunia katika mbio fupi za mita 100 na 200, Usain Bolt.

Gazeti la Tanzania Daima

"Jah man,king of haile selasiai,jah rastafarai,king of caribean,man to man from jamaica,the man himself watagwan man bum bum".
 
Lkn jamani hao walimu alioomba mnawajua walimu wa kufundisha nini??maana isiwe tunabwatuka tu kumbe ni walimu wa fani ambazo hapa nchini hazipo,yawezekana ni walimu wa kufundisha jinsi ya kutengeneza nuclier,au walimu wa kuja kufundisha uchimbaji wa gesi na mafuta,maana sisi tukiskia walimu tunajua kuwa ni wa kufundisha hesabati na historia tu.
 
It hapi nu ting to stay doun in tiz especial in arusha wi bway get biz inna dar is hot like in hot pot slam a gyal 2times mi a get flot das y mi lovu a city weda si doun wi mi bway stackin togeda inna consat mi gi dem fleva mi ana i pon de back.

Rude bwoy. Mi Irites
 
Duh! Tanzania yenyewe ni maajabu tosha ya ulimwengu. Watanzania wenzangu, wana JF hivi huyu namba moja ndy amefika mwisho wa kufikiri kiasi cha kutaka kutuletea wajamaica kuja kutufundishia watoto wetu hisabati na sayansi! hvi wajameica wa rekodi gani duniani ya uvumbuzi iwe wa madawa, technology au chochote? Ina maana ktk nchi yenye watu milioni karibia 50 hamna wataalamu wa masom ya hesabu, masomo ya sayansi? kuna maswali mengi sana ya kujiuliza khus uwezo wa akili za namba moja. Angesema anaomba hawa jmaa waje kutufundisha kilimo cha Ndizi, Riadha na Kuvuta bange ningemuunga mkono kwa asilimia mia ila siyo kwenye hy sekta. Wako wahindi, hawa jamaa wanajulikana duniani kwa kuwa wazuri wa hisabati na masomo ya akaunti, wajerumani . Y jameicans?
 
Mkuu kwani Jamaicans kuwa walimu kuna tatizo gani?
 
Mkuu kwani Jamaicans kuwa walimu kuna tatizo gani?

nadhani kwanza system yetu ya ufundishaji iimarishwe kama alivyopendekeza Mbatia..amasivyo hao wajamaica hawataleta mabadiliko yyte. St Mary's watakuwa na uzoefu mzuri na waalimu wa kigeni na jinsi perfrmnce ya shule hzo zilivyoporomoka ghafla...
 
Iimarishwe vipi?
 
Matatizo ya msing ya walimu yatatuliwe na wanaojiunga na mafunzo ya ualimu wawe wenye ufaulu mzuri big results now itaonekana
 
Matatizo ya msing ya walimu yatatuliwe na wanaojiunga na mafunzo ya ualimu wawe wenye ufaulu mzuri big results now itaonekana

Ufaulu wa vipi mkuu? Manake walimu wengi wa sasa tayari walishafaulu
 
Yes class, iz evibadi ina di clas?
We gwan learn somting nu today!
..................................
...sd#$%fgdg^YTY..
..................................
Whoz gat weed in here, me iz thursty!

:bange::bange::bange::bange::bange::bange::bange::bange:

Jah Bless!

Hahahaha, tunaomba mno, kila kitu tunaombaomba tu
Cha muhimu sasa naona tumwombe Xi Jinping atusaidie kuongoza mwaka mmoja tuone kama tunaweza kupiga hatua!

Watagwan!
 
Back
Top Bottom