Muke Ya Muzungu
JF-Expert Member
- Jun 17, 2009
- 3,444
- 264
Kwa wale wanaofuatilia sakata la Umeme, majina mawili mtakuwa mnayafahamu vizuri sana. January Makamba na William Ngeleja. William Ngeleja ni Waziri aliyeteuliwa na Rais JK, na January Makamba ni kijana ambaye amewahi kumfanyia JK kazi, kama mwandishi wa hotuba. Baada ya JM kukosa uwaziri, aliahidi kuwafanyia wana bumbuli kazi waliyomtumia bungeni. Wengine wamemuita JM mnafiki na msaliti wengine wanamuona kama kijana mwenye ndoto kubwa
Kumekuwepo mvutano, wa vuta nikivute kati ya ngeleja na makamba Jr. Mara Barua, mara kukingiana kifua, mara rushwa. Haya yote kwa mtizamo wangu yanafanywa ili kuonyesha uwezo mdogo wa Bwana ngeleja katika wizara ya nishati na madini, na uwezo wa JK katika uteuzi wake wa mawaziri. Wachambuzi wengi wa kisiasa wamekuwa wakitoa lawama nyingi dhidi ya JM kwamba ni kibaraka wa mafisadi na mtu mwenye ubinafsi mkubwa. Lakini mwisho wa siku yote ni maneno, ila ujumbe mzito ni kwamba
1. Amedhiirisha wazi, na anaendelea kuudhiirishia umma kwamba JK hana uwezo wa kuiongoza nchi
2. Ameamua kumtumia taarifa JK kwamba nafasi yoyote anaweza kuipata bila usaidizi wake JK