Haya mambo wakati mwingine nii burudani sana,uzuri ukiwa ndani uwezi kuona nje na wakati mwingine Mungu anaongea na walio nje kuwaonyesha wa ndani.Ndio maana kukiwa na mechi ya mpira wakati mwingine watazamaji umlazimisha kocha kwa kumwambia toa huyo!!!!!!!!.....toa huyo tena wakishambulia kwa mbija kubwa sana pfyuuuuuuu!!!!!!!!!!!!pfuuuuuuuuuuu!!!!!. Mwisho wa yote kocha usikia makelele ya mashabiki na umtoa mcheza nje.Mchezo huo ama style hiyo imekwenda mpaka sasa imefikia hatua hata makocha wamefikia kuwa nao hatima ya kuendelea kuwemo uwanjani kama makocha wa timu ya mashabiki ni kuweka ushindi kwenye timu ya mashabiki,vinginevyo kitakachofuata baada ya kubolonga mara kadha wa kadha ni kushinikiza kocha atoswe kama ilivyotokea kw maxio maximo. [Kocha Mbrazil]
Haya yanayosemwa sana siku hizi mitaani kuwa fulani anatyarishwa kuwa Rais kimepanda kikashuka,hakika kama mtanzania nianetafakari kupitia ukweli halisi na si kwa kuwa fulani anafedha na watu wa kumfanya awepo pale wanasahau kuwa fedha sio kila kitu.
Mwaka 1985 Baba wa Taifa alikuwa na chaguo lake ambalo alitaka kumlithisha kuwa Rais mwaka huo lakini pamoja na nguvu zote hizo za Umwalimu wake kwa Serikali dhamira yake haikufanikiwa. Mwaka 1995 Rais ambae alikuwa madarakani alikuwa na chaguo lake ambae alipenda amlithishe pia,lakini siye aliyekuja kuwa Rais wa Tanzania kipindi hicho.Mwaka 2005 Rais na wale waliokuwa madarakani walikuwa na machaguo yao mwaka huo ambao waliwaanda kuwaweka madarakani lakini matokeo yake alieingia sie aliekuwa chaguo lao hata kama wako chama kimoja.
Leo hii tunaenda mwaka 2015,tunajua kama binadamu Mungu alivyotuumba tuna utashi na chaguzi zetu binafsi lakini, katika swala la urais Mungu nae ucheza turufu yake kwa sababu anazozitaka yeye na sio sisi binadamu watu wazima uwa na msemo wao wewe unapanga na Mungu anapanga.Hili la Rais kuhusishwa na kumwandaa huyu jamaa kama ni kweli au La hakika ni utashi tu na si jambo la ajabu na yeye si mtu wa kwannza uzuri mwenyewe anajua jinsi alivyokutana na vizuizi mpaka akafika hapo ndivyo hivyo huyo wasie mtaka hao wengine awe Rais wa mwaka 2015,hatatoka kwa Watawala bali watawala watalazimika kumsimamisha ili iwe ni heri ya nusu shari kuliko shari kamili.Muda ukifika mbona kitaeleweka tu.Kuna mmoja huyo alitayarisha timu idara zaote Serikalini akiwa anategemea Urais wa 2005 lakini chakachua ni kuchakachue iliyopita uwezi kuamini, urais aliusikia kwenye bomba.
Uzuri wa maswala hayo utoa ajira kwa baadhi ya watanzania na wengine kujipatia kipato kupitia michakato hiyo hivyo yote heri,lakini uzaniaye ndiye kumbe siye na uzaniaye sie kumbe ndie, kwenye msafara wa mamba kenge nao wamo.Huwezi kutumia Devil style Strategy [Fisadi] kumpandisha chati Mtu wa Kiti cha Urais [Utakatifu],sijawi kuona aina hiyo ya mikakati.Kwa kuwa wanapenda sana kufananisha na style ya southh africa ya Jacob Zuma,wanasahau wale jamaa walikuwa na mtafaruku wa kweli,na hatimae imejibu kwa kijana malema.Na pia kihistoria Tanzania ni Taifa lenye watu wengi wenye uzoefu kisiasa ambao jicho lao kwa mtu anaitwa Rais liko pana sana kuliko ilivyo kawaida.