JK Ampeleka Augustino Mrema kutibiwa India?

Ni haki yake kulipiwa kwanza amelitumikia taifa hili kuliko huyo Shekhe Yahya ambaye naye alilipiwa na JK kweli Mrema amelitumikia Taifa hili kwa hali na mali uaminifu wake kwa taifa ndio ulimpoza ndugu yangu alifikiri wako wengi wa aina yake serikalini kumbe yupo pekeyake.

sheikh yahya amelitumikia taifa hili tokea enzi za nyerere, amemtumikia sana nyerere "devil advocate"
 
hii picha inatia simanzi kubwa... ninachosikitika zaidi ni kwa nini jamaa bado anataka kugombea wakati afya yake mbaya??

Jamani kuweni na huruma hata angelikuwa wewe Mrema tunayemjua amefikia hapa kweli?

Muonee huruma alikuwa na nia njema na Tanzania sasa hivi ameona asipojikomba atakufa kabla ya siku zake naomba tumuonee huruma hata wengine ambao wana uwezo wa kumchangia mchangieni.

Ningeshauri Mrema astahafu mambo ya siasa maana afya yake pamoja na mimi kutokuwa na ufahamu wa kuwa Daktari hila mzee huyu inaonekana ni mgonjwa sana .
 
Augustine Lyatonga Mrema anaonekana mgonjwa.





katika hali hii huwezi kuacha kumsaidia mrema ..ukiachilia upinzani yeye amepata kuwa naibu waziri mkuu na waziri wa mambo ya ndani aliyetukuka......[cheo cha naibu waziri mkuu amepewa heshima hiyo yeye na salim tu nchi hii]

kuachilia utumishi....ana haki pia ya kulipiwa na ofisi ya rais kwani amepata kuwa afisa wa TISS...na mkufunzi.

inaweza ikaonekana amelipiwa na ofisi ya rais ..lakini mjuwe kuwa TISS ipo ofisi ya rais...na kama atakuwa ameenda kwa mgongo wa kiongozi wa zamani ....atakuwa ametumia kasma ya ofisi ya rais manejimenti ya utumishi wa umma.....zote hizo ni ofisi za rais ambapo rais ni kikwete....so katika hali ya kawaida lazima watu watasema rais amempeleka .....kwani pia angeweza kumkatalia ...kwani nchi hii kuna uhusiano mkubwa kati ya stahili za mtu na ridhaa ya watawala......kuwa ni haki yake kutibiwa pekee ..kama former senior minister au agent..hakutoshi!!!!.....mimi i have many of my friends ..in TISS ambao ni watu wazima ..huwa wakipata matatizo wanapelekwa india kutibiwa na TISS....HAINGEKUWA halali ...na hata hivyo wamechelewa sana kumsaidia mzee mrema....hadi ionekane kama fadhila!!!
 
Kumtendea binadamu mwenzio ni jambo jema tatizo ni nia ya kumsaidia binadamu mwenzako ina tokana na nini? Kuna wale wanao saidia kuonekana mbele za watu, kuna wanaosaidia kwa ajili wana furahi mtu mwingine aki hitaji msaada wake na kuna anaye saidia kwa sababu ana taka fadhila fulani. Sawa JK labda kamsaidia lakini what is the motive behind it? Kama kamsaidia kwa nia njema tu basi JK azidi kuongezewa la sivyo....
 
Amelipiwa gharama zote na JK ,na hapa sisemi kuwa ni serikali no. Ni JK personaly ndio amelipia gharama zote kuanzia tiketi ya ndege hadi matibabu yake yote akiwa huko.

basi kama ni kweli ameifanya binafsi atakuwa anatumia kasma ya matibabu ya nje kama turufu ya kisiasa...kwani alivyomlipia yule mama aliyegombea urais[sasa amehamia ccm]...ingeweza kuwa personal kwa sababu yule mama hajapata kuwa afisa wa juu serikalini..

lakini kwa mrema hakukuwa na haja ya matibabu yake kufanywa personal....wakati mrema anastahili kuangaliwa na serikali[pale anapokuwa na matatizo makubwa].....kwa kuzingatia kuwa alikuwa seniour civil servant and deputy premier.......

tusijefikia mahali tunajeuza stahili za watu kama reward ya kuwazawadia au kununua loyality.....tutawanunua wengi kwa staili hii...na hivi magonjwa ya uzee yanakuja!!

so tuseme ikitokea mawaziri wakuu wakajiunga na CCJ...haki yao ya kikatiba ya kuhudumiwa itakatizwa??????...nafikiri hiyo ndiyo fimbo...ondoa ulinzi,ondoa huduma,ondoa mishahara..ONDOA MATIBABU!!....si wamemuona mrema anavyotaabika....na hata seif alivyotaabika ...sijui kama watajaribu !!
 
Taarifa nilizozipata hivi punde Nikiwa hapa mjini Dodoma kutoka kwa source ya kuaminika ni kuwa Agustino Mrema amepelekwa Nchini India kutibiwa .

Aliyemsafirisha ni Rais Jakaya Kikwete.

My take;
Ndio maana alikuwa anampigia filimbi JK kumbe alikuwa anataka kupata malipo?
Akirudi anaweza naye kuwa mtabiri kama Sheikh Yahaya,juu ya urais wa JK?

Kiranja; Mrema akipitisha bakuri la msaada kuwa anahitaji hela za matibabu kwenda India, je watanzania wangapi wako tayari kumsaidia??

just be honesty!
 
nadhani hapa duniani hakuna kitu chenye thamani kubwa kuliko uhai wa binadamu; haununuliki. Kwa hiyo, juhudi zozote za kurefusha uhai wa binadamu yeyote bila kujali itikadi yake ni jambo la muhimu sana. Namshukuru JK kwa hilo ingawa nilisikitika sana kusikia kuwa General Nyirenda hakupewa msaada wa namna hiyo alipokuwa mgonjwa.


Ninadhani kuwa jambo kubwa lisiwe la kuwapeleka hao wateule kutibiwa nje na kuwaacha akina Kichuguu wajifie Mwananyamala bila hata kitanda. Kinachotakiwa ni kujenga huduma za afya nchini ziwe za ubora wa juu kiasi kuwa hata watu wa nje waje kutibiwa kwetu. Tumeona siku hizi wachezaji wa mpira kutoka nje wanakuja kucheza kwenye vilabu vyetu, inabidi hata huduma zetu za elimu na afya pia tuziinue katika viwango vya kukubaliwa kimataifa kusudi watu wa nje nao waje kuzifuata kwetu.

Kichuguu,Meja Alex Gwebe Nyirenda(Si General Nyirenda) naye pia alipatiwa msaada na serikali ya Tanzania kwa kumpeleka nchini India kwa matibabu na kisha baadaye alirejeshwa Tanzania na kuendelea na matibabu katika hospitali ya Muhimbili kabla mauti hayaja,kuta...Soma habari hii hapa chini;


Kwa huzuni na masikitiko makubwa tumezipokea habari za msiba wa Major Alex Gwebe Nyirenda.Huyu ndiye shujaa aliyepandisha bendera ya Tanganyika huru na Mwenge wa Uhuru kileleni Mlima Kilimanjaro usiku ule wa mkesha wa Uhuru miaka 47 iliyopita.

Marehemu Nyirenda ambaye alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kansa kwa muda sasa, amefariki jana majira ya saa moja jioni(saa za Afrika Mashariki) katika hospitali ya taifa Muhimbili alikokuwa amelazwa.Mapema mwaka huu Major Nyirenda alipelekwa nchini India kwa matibabu zaidi kufuatia kudhoofika kwa afya yake.

Marehemu Nyirenda anatarajiwa kuzikwa siku ya jumatano ijayo katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar-es-salaam.Msiba upo nyumbani kwake huko Mbezi Beach,Flats za National Milling karibu na njia panda ya kwenda Africana.

Ni siku chache tu zilizopita ambapo tuliweka mahojiano tuliyofanya na Major Nyirenda kuhusiana na harakati za uhuru,zoezi zima la sherehe za uhuru nk.Unaweza kuyasoma mahojiano hayo kwa kubonyeza hapa.

Katika mahojiano yale,Major Nyirenda aliongelea mambo mengi.Lakini katika mengi hayo pengine ushauri au usia aliotuachia wa kujitolea,uvumilivu na uaminifu ndio ambao hatuna budi kuufanyia kazi ipasavyo kwa minajili ya kumuenzi Major Nyirenda na pia kwa maendeleo yetu binafsi na jamii zetu.


Na hii hapa chini


Lakini Jumapili iliyopita ya Desemba 21, 2008 shujaa huyo wa mwenge alifariki dunia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam baada ya kusumbuliwa na kansa ya koo.

Alilazwa kwanza katika Taasisi ya Magonjwa ya Moyo Kinondoni (THI), Dar es Salaam na baadaye Muhimbili kabla ya kupelekwa India kwa matibabu zaidi Februari mwaka huu.

Baada ya kupata nafuu huko India, alirudi nyumbani Mei mwaka huu na kwenda tena India kwa vipindi viwili vya uchunguzi wa afya yake ilivyokuwa ikiendelea. Mara ya mwisho alitoka huko Septemba mwaka huu.


 
Ningeshauri Mrema astahafu mambo ya siasa maana afya yake pamoja na mimi kutokuwa na ufahamu wa kuwa Daktari hila mzee huyu inaonekana ni mgonjwa sana .

Hili ni gumu kwa wanasiasa wetu wengi tu! Akistaafu atakula wapi?
 
Jamani mnyonge mnyongeni lakini haki mpeni.
Mbona bwana mzee ameshasaidia watu wengi na wengine ni wa kawaida tu wala hawajulikani na jamii?????????
 
Kumbe JK ana moyo wa kujali utu namna hii, okay. Get well soon mzee wa kiraracha.

Kuna Daktari wa Rufaa huku mbeya, kijana mdogo tu a graduate from muchs 2007 amepigwa RISASI tano na Majambazi, mpaka sasa hivi hali yake ni mbaya kwani Madaktari wamefanikiwa kutoa RISASI nne, wanasema hiyo nyingine labda INDIA ndiyo wanaweza kuitoa na mbaya zaidi Nasikia wameshindwa kumsafirisha kumpeleka Dar kwani hali aliyonayo hawezi kusafirishwa kwa Surface transport. Sasa nauliza hivi Serikali yetu inashindwa kuleta private Jet ili huyu kijana Daktari ( Fide) Asogezwe hapo Dar es Salaam

Mungu amsaidie aweze kupona ili aendelee kuwasaidia walalahoi wa Mbeya ambao hawawezi kwenda kutibiwa INDIA
 
Kiranja; Mrema akipitisha bakuri la msaada kuwa anahitaji hela za matibabu kwenda India, je watanzania wangapi wako tayari kumsaidia??

just be honesty!
Mkuu hata katika maandiko kuna sehemu inasema "....KUWA MWAMINIFU HATA KUFA.." Kama habari hii ni kweli basi Mrema hafai asilani, huwezi kuwa kiongozi mzuri kwa kuukana ukweli ulioupigania miaka mingi eti ili ulipiwe gharama ya matibabu ya kisukari.
Kwani anapopotosha ukweli kuwa Uongozi wa JK umeleta maendeleo hajui wananchi wangapi wana poteza maisha yao kwa malaria tu huko vijijini?
Kwa upotoshaji huu hajui anachangia wengi kufa huko mbeleni kutokana na uzembe wa viongozi anaowapamba ili wananchi wanaomwamini yeye Mrema wawachague tena?
Mrema ni msaliti,Mwongo na asiye faa kuwa kiongozi kama ni kweli aliukana ukweli na kujikomba ili kubembeleza kugharamiwa matibabu India.
Hata hivyo namtakia afya njema. Lakini ajue kuna wengi ambao wanakufa kwa kukosa matibabu ambayo yanapatikana hata kwenye Zahanati vijijini na sababu ni hao hao waliomlipia kwenda India.
 
Taarifa nilizozipata hivi punde Nikiwa hapa mjini Dodoma kutoka kwa source ya kuaminika ni kuwa Agustino Mrema amepelekwa Nchini India kutibiwa .

Aliyemsafirisha ni Rais Jakaya Kikwete.

My take;
Ndio maana alikuwa anampigia filimbi JK kumbe alikuwa anataka kupata malipo?
Akirudi anaweza naye kuwa mtabiri kama Sheikh Yahaya,juu ya urais wa JK?
Ni Mrema aliyeandika barua kuomba msaada wa kutibiwa nje na si vinginevyo...
 
jamani mwacheni amsaidie kama ni kweli mrema amefanyia kazi kubwa hii nchi na msisahau kuwa ni afisa mstaafu wa usalama wetu japo haufanyi kazi vyema.
 
Kuna Daktari wa Rufaa huku mbeya, kijana mdogo tu a graduate from muchs 2007 amepigwa RISASI tano na Majambazi, mpaka sasa hivi hali yake ni mbaya kwani Madaktari wamefanikiwa kutoa RISASI nne, wanasema hiyo nyingine labda INDIA ndiyo wanaweza kuitoa na mbaya zaidi Nasikia wameshindwa kumsafirisha kumpeleka Dar kwani hali aliyonayo hawezi kusafirishwa kwa Surface transport. Sasa nauliza hivi Serikali yetu inashindwa kuleta private Jet ili huyu kijana Daktari ( Fide) Asogezwe hapo Dar es Salaam

Mungu amsaidie aweze kupona ili aendelee kuwasaidia walalahoi wa Mbeya ambao hawawezi kwenda kutibiwa INDIA

Ili kuishtua serikali WAFANYAKAZI KATIKA SEKTA YA AFYA HAPO MBEYA WACHANGE KILA MTU HATA SH 10,000 KWA AJILI YA MATIBABU YAKE. RMO SI YUPO NA ANAJUA?
AHAMASISHE SUALA LA MICHANGO TENA WIKI HII NI WIKI YA MISHAHARA.
MKIFANYA HIVYO, UMMA UTACHANGIA NA SERIKALI ITAZINDUKA.
OKOENI MAISHA YAKE.
fanyeni kama vile mnavyochangia harusi.
si mtoto wa malechela au george kahama huyo. atakufa na mtapoteza chombo cha thamani kwa jamii hapo mbeya.
 
aende akatibiwe tu mie namuombea apone hicho kinachomsumbua ..nchi hii ina mengi sana ukiyachokonoa utazimia ..
 
Ni haki yake kulipiwa kwanza amelitumikia taifa hili kuliko huyo Shekhe Yahya ambaye naye alilipiwa na JK kweli Mrema amelitumikia Taifa hili kwa hali na mali uaminifu wake kwa taifa ndio ulimpoza ndugu yangu alifikiri wako wengi wa aina yake serikalini kumbe yupo pekeyake.

Sitasahau kauli ya ofisa mmoja wa ngazi ya juu wa wizara fulani aliyeongea pasipo kigugumizi, kwamba "Unapofikiri unatimiza wajibu vizuri kwa uongozi wako usifikiri kila mtu ana-apprreciate, wako wanaokuona bado wewe ni mbaya"

Kimtizamo na mwenendo wa mazungumzo alielekea kumaanisha kwamba mkubwa hakosei na kama akikosea rejea hilo la kwanza kwamba mkubwa hakosei. Afisa huyo alilazimisha kukiukwa kwa taratibu zote za utawala pasipo kujali maafa yatakayojitokeza kwa sababu ya maamuzi yake. Alikuwa analinda kauli tata ya bosi wake kwa hali na mali kumlinda fisadi mmoja.

Tunaambiwa hapo kwamba sio serikali iliyomlipia Mrema kwa kutambua kazi alizolifanyia Taifa, ni JK kwa moyo wake mwenyewe na kwa pesa yake binafsi sio kama Raisi. Ni marafiki wa siku nyingi hao kwenye system, kamsaidia rafiki yake na hapo hakuna ubaya. Ni wapinzani katika sera lakini sio maadui. Wako vyama tofauti lakini wako karibu sana.

Leka
 
Nimegundua watu wengi hawana uzalendo na nchi yao au kwa maana nyingine hawapendani wao kwa wao,yaani mtanzania mwenzako kupewa msaada wa kutibiwa maradhi yake wewe unachukia na kukasirika halafu unajiita eti mzalendo ni aibu.Tena uchafu huo uondolewe kabisa hapa JF sisi tuna sifa ya umoja toka enzi ya mabwanyenye hadi leo sasa nyie watu wadogowadogo mnataka kuleta dhambi ya ubaguzi!Leo mtasema Mrema,kesho Mbowe na keshokutwa mdogowako wewe unayeona dhambi Mrema kutibiwa na serikali.Aibu,aibu,aibu.
 
Back
Top Bottom