JK Ampeleka Augustino Mrema kutibiwa India?

Lakini ni binadamu kama binadamu wengine hivyo kama Jk ameamua kulipa Gharama za usafiri ni vizuri tu hakuna shaka kabisa
 
Hii ni haki yake kutibiwa,amelitumikia taifa hili kwa uaminifu sana. Leo hii kupelekwa kwake nje kutibiwa watu wanataka kujizolea sifa.

Nchi hii tunapenda sifa zisizo na msingi kabisa,sasa kama Rais kampeleka binafsi pia ni jambo jema lakini asije akawa anafanya hivyo ili kulipwa fadhili kwani mrema kama Naibu waziri mkuu wa Zamani anastahili hayo yote.

Sijui Ni lini tutaendelea!
 
So now whatever J.K. Does tends to annoy someone (if not everyone!)? Wait till your Paps falls sick and you can't afford that hard cash to Indian medical services (let alone Apollo Medical Centre 'as quoted'), there now you'll discover what's good and what's bad for you and for J.K.

let him be paid for and get well soon!

Ndugu kizomanizo

I think this is your first post cant you say Hello to your fellow members please or it doesnt matter!
 
Hata kama ni serikali, mbona wengi wanapelekwa nje kupitia wizara ya afya?
Kwani Mrema ndiyo inakuwa kuna jambo nyuma?
Kuwe na jambo (string attached) au hakuna Mrema anastahili kutibiwa na serikali. Alishakuwa naibu waziri mkuu na amefanya kazi nyingi kwa wananchi wa "inji" hii.
Tunamatakia matibabu mazuri apone haraka!
 
Ni haki ya kila raia kugharamiwa nje matibabu ambayo hayapatikani hapa nchini. Najua wizara ya afya inao utaratibu kama huo wa rufaa za kwenda kutibiwa nje. Sioni cha ajabu wala siasa yoyote katika hili. Mbona watoto wadogo wasiojulikana katika siasa zozote zile wanapelekwa nje kutibiwa na serikali, sema tu ni kunakuwa na foleni kubwa ya kusubiria. Na hatujui huyo Mrema alipewa hii rufaa lini na kasubiri hii fursa toka lini.

Tupunguze tafsiri zisizo na maana nzuri kwenye kila kitu. Siku hizi hata mwanamke yoyote akipewa cheo kikubwa tu utasikia wakisema ni 'chakula ya JK'. Ujinga mtupu huu.

Mtu B,
Hiyo foleni ya kwenda kutibiwa nje isiyoeleweka nani yuko mbele na nani anafuatia ndio inayoleta hisia ya matibabu kutumika kama hongo au kuwepo kwa wananchi walio bora zaidi kuliko wengine.

Mrema ana haki ya kutibiwa lakini ingekuwa vema waTZ wakafahamishwa na wao wakiugua watasaidiwaje maana nchi itakapodaiwa deni litakuwa ni la kwetu wote?
 
So now whatever J.K. Does tends to annoy someone (if not everyone!)? Wait till your Paps falls sick and you can't afford that hard cash to Indian medical services (let alone Apollo Medical Centre 'as quoted'), there now you'll discover what's good and what's bad for you and for J.K.

let him be paid for and get well soon!

That's the plight of the majority who, unfortunately, are not in a position to attract the attention of their government or JK. Motives aside, JK funding of the medical care of Mzee wa Kiraracha on its own cannot elicit annoyance. But note that Mrema just got lucky whatever the circumstances. :(
 
Taarifa nilizozipata hivi punde Nikiwa hapa mjini Dodoma kutoka kwa source ya kuaminika ni kuwa Agustino Mrema amepelekwa Nchini India kutibiwa .

Aliyemsafirisha ni Rais Jakaya Kikwete.

My take;
Ndio maana alikuwa anampigia filimbi JK kumbe alikuwa anataka kupata malipo?
Akirudi anaweza naye kuwa mtabiri kama Sheikh Yahaya,juu ya urais wa JK?
Acha utani wakati ndugu huyu anaumwa,
 
Taarifa nilizozipata hivi punde Nikiwa hapa mjini Dodoma kutoka kwa source ya kuaminika ni kuwa Agustino Mrema amepelekwa Nchini India kutibiwa .

Aliyemsafirisha ni Rais Jakaya Kikwete.

My take;
Ndio maana alikuwa anampigia filimbi JK kumbe alikuwa anataka kupata malipo?
Akirudi anaweza naye kuwa mtabiri kama Sheikh Yahaya,juu ya urais wa JK?
Hii taarfa yako haijakamilika.
nina mashaka na soucre yako.
 
Taarifa nilizozipata hivi punde Nikiwa hapa mjini Dodoma kutoka kwa source ya kuaminika ni kuwa Agustino Mrema amepelekwa Nchini India kutibiwa .

Aliyemsafirisha ni Rais Jakaya Kikwete.

My take;
Ndio maana alikuwa anampigia filimbi JK kumbe alikuwa anataka kupata malipo?
Akirudi anaweza naye kuwa mtabiri kama Sheikh Yahaya,juu ya urais wa JK?
Taarifa yako haijakamilika.
Nina mashaka na source yako.
 
Amelipiwa gharama zote na JK ,na hapa sisemi kuwa ni serikali no. Ni JK personaly ndio amelipia gharama zote kuanzia tiketi ya ndege hadi matibabu yake yote akiwa huko.

Ameonyesha uungwana kuokoa maisha ya binadamu mwenzake. Abarikiwe.:D
 
Mkuu hata katika maandiko kuna sehemu inasema "....KUWA MWAMINIFU HATA KUFA.." Kama habari hii ni kweli basi Mrema hafai asilani, huwezi kuwa kiongozi mzuri kwa kuukana ukweli ulioupigania miaka mingi eti ili ulipiwe gharama ya matibabu ya kisukari.
Kwani anapopotosha ukweli kuwa Uongozi wa JK umeleta maendeleo hajui wananchi wangapi wana poteza maisha yao kwa malaria tu huko vijijini?
Kwa upotoshaji huu hajui anachangia wengi kufa huko mbeleni kutokana na uzembe wa viongozi anaowapamba ili wananchi wanaomwamini yeye Mrema wawachague tena?
Mrema ni msaliti,Mwongo na asiye faa kuwa kiongozi kama ni kweli aliukana ukweli na kujikomba ili kubembeleza kugharamiwa matibabu India.
Hata hivyo namtakia afya njema. Lakini ajue kuna wengi ambao wanakufa kwa kukosa matibabu ambayo yanapatikana hata kwenye Zahanati vijijini na sababu ni hao hao waliomlipia kwenda India.

acha cheap conclusion na kusema vitu visivyo practical, nimekuuliza je sisi wananchi wangapi wangekuwa tayari kumlipia gharama za matibabu Mrema? umesema anatakiwa kuwa mwaminifu mpaka kufa!!! yaani yeye afe kwa jina la kuwa mpinzani? kwani anawasaidia nani? huoni kuwa msemo wako dio uliomfanya basi ajikombe kwa JK(kwa maneno yako)? na msemo wako huu ndio unawafanya wapinzani wengi kutokuwa waaminifu! kama mwananchi mwenyewe ni wewe!!

To my side, I do believe Mrema angesaidiwa na serikali hata kama asingemfagilia JK, Mrema usimfananishe na wewe.By the way kwa conclusion yako vipi kuhusu Kubenea si naye alipelekwa na JK? Unasemaje sasa kuwa mwanahalisi ni la JK?-I do believe so but on on the ground ya kuwa Kubenea alipelekwa India!

acheni utani na kifo jamani!!
 
Taarifa nilizozipata hivi punde Nikiwa hapa mjini Dodoma kutoka kwa source ya kuaminika ni kuwa Agustino Mrema amepelekwa Nchini India kutibiwa .

Aliyemsafirisha ni Rais Jakaya Kikwete.

My take;
Ndio maana alikuwa anampigia filimbi JK kumbe alikuwa anataka kupata malipo?
Akirudi anaweza naye kuwa mtabiri kama Sheikh Yahaya,juu ya urais wa JK?

JK na Mrema,ni kama chanda na pete no body can watenganisha them
 
haya ni majungu Mtu yeyote aliyewahi kuwa na cheo cha katibu mkuu au zaidi anatibiwa na serikali hivyo si JK bali ni serikali.
 
Ni vizuri kuwa na Mkuu wa Nchi kama JK anayeona huruma kwa raia wake aliye na ugonjwa usiotibika nchini, halafu akamgharimia binafsi kumpeleka nje kutibiwa.

Ingekuwa ni jambo la kutukuka kama huruma hii ingesimikwa nchini ili Watanzania wajue kuwa endapo watapatikana na bahati mbaya kuugua ugonjwa unaoweza kutibiwa nje tu, basi watapelekwa huko kwa matibabu. Kutibiwa nje na Serikali, sio tu fedha za kodi yetu zinatumika, bali hata akiba yetu ya fedha za kigeni zinatumika.

Kutumika kwa fedha za kigeni kunapungaza uwezo wetu kitaifa wa kununua madawa toka nje na vifaa vingine muhimu kwa maendeleo na ustawi wa umma kwa jumla. Kwa hiyo inafaa kuwe na utaratibu unaoeleweka na wa wazi, badala ya huduma kama hiyo kutolewa kama zawadi au hongo kwa kupigia viongozi kampeni za kisiasa.
 
Huyo anayeitwa JK ni Wizara ya afya au ni mtu binafsi. Mbona ni wengi wanapelekwa India na hatusemi JK kawapeleka. Sifa za bei nafuu.

Kuna haja ya kuwa na Wizara ya afya? Matibabu yote naona sasa hivi ni India.

Napendekeza Wizara ya afya ifutwe.
 
Mzee Mrema amekuwa mgonjwa kwa muda mrefu sana; amehitaji matibabu kwa muda mrefu. Hivyo kupatiwa matibabu haya kwa msaada wa mtu yeyote siyo jambo la kubeza bali la kuunga mkono na kushukuru. Kama Mrema angeomba asaidiwe michango ili apelekwe nje kutibiwa nina uhakika wa asilimia kubwa kati yetu tutakaa pembeni na kuombea wengine wachangie!

Of course kuna politics behind but that is irrelevant. Kwa kumsaidia sasa hivi JK amehakikisha kuwa Mrema kamwe hawezi kusimama against him in an election.. now that is the story behind the story.. .. you do this, we will do that.. isn't that what quid pro quo is? Mrema did his part for JK, and JK has just returned the favor.
 
Back
Top Bottom