spin twist spin twist. sishangai hata kidogo leo hii kusikia kutoka kwenu kuwa UDOM ilijengwa na nyerere ila ilikuwa haionekani ndo maana kapafanya pale dodoma kuwa makao makuu ya nchi. hivi unafikiri sisi sote ni wajinga kama nyie? Just a simple task, ingia kwenye website ya ujenzi kuna kila kitu, na inakuchukua muda mchache sana kuyaona haya na naamini hutakuja kupost uharo kama huu. tunajua mnaona aibu ndo maana narudia kusema mnatamani leo hii mwendelee kusafiri siku 3 kutoka nanyumbu mpaka dar au mkitaka kwenda kanda ya ziwa mpitie nchi jirani. usiandike kwa kutanguliza tumbo huku ukiwa umelewa mbege, tumia muda kidogo kujisomea. au umekaririrshwa kuwa kila alichofanya kikwete ni kupinga tu?
ieleweke kwamba si underestimate mchango wa mkapa kwa taifa hili ukiachilia maovu yake aliyoyafanya ( kama vile kufanya biashara zake ikulu mfano banki iitwayo anaben, mgodi wa kiwira, mwananchi gold, mikataba yote ya migodi, ndege ya rais, rada ya chenge, ndege za jeshi, magari ya jeshi, NBC mil 70 kwa makaburu, na mengine mengi) ni kimlinganisha na Mwinyi na nyerere (the least). alifanya mazuri mengi tu ikiwa ni pamoja na kujenga barabara km 3000 kwa miaka 10 ukilinganisha na nyerere aliyejenga km chini ya 2000 kwa miaka yote 24 pale magogoni. lakini siwezi kumlinganisha na Kikwete hata kidogo labda rais ajaye ambaye sote hatumjui (japo wewe unaota slaa atakuwa rais-sijui wa kule karatu, anyway...)
nakushauri kama huna data usiandike humu japo hatukujui lakini hujengi zaidi ya kubomoa.