JK aenda Uingereza kikazi

Nadhani yuko juu mno kiasi cha kutojua hali halisi ilivyo nchini, sidhani kama anaelewa shida iliyopo kwa wananchi wake. Nimemuona PM anazeeka maana kila kitu anaachiwa yeye.
 
una maana anaenda kufanyiwa kazi kwenye ofisi hii???

Hapana........moja ya sababu za mgomo wa madaktari ni uduni wa mazingira ya kazi.........kwa hivo hii ni study tour kwake ajionee vitendea kazi huwaje

Operating+theater+%25284%2529.jpg
 
Kwa kweli inakera sana sasa! Yaani kucha kulala yeye safari hazimuishi hata safari ambaya waziri angeweza kwenda yeye anakwenda. Mara utasikia Mh. Rais aenda Denmark kujifunza jinsi Wanavyosindika maziwa!!! Kitu kama hiki kinatija kweli? Kama si ufujaji ni nini? Tena unaambia gharama anazotumia raisi kwa safari moja kama hiyo unaweza kujenga vyumba saba vya madarasa ya shule ya msingi huu je si ufujaji? Inasiktisha sana kibaya zaidi anadai anakwenda kutafuta wawekezaji!!!!?

Hebu tuangalie mifano ya wawekazaji waliopo ambao Mh Rais hujinasibu kwamba anachangia Kuwaongeza anapokwenda nje:

1. Muarabu wa Loliondo alimilikishwa Loliondo kwa miaka 90.....Matokeo yake badala ya taifa kunufaika yeye anawinda pamoja na kupeleka wanyama Uarabuni!!! Akili zako changanya na zakeee!
2. Muekezaji kutoka India kwa ajili ya shirika la Reli.....Matokeo yake kashindwa kuleta Treni mpya badala yake anatumia vichwa vibovu vya treni,pia kashindwa kulipa wafanyakazi badala yake serikali inalipa kwa niaba yake...Mwisho kaliacha shirika mahutihuti....
Akili zako changanya na zake!!!
3. Wawekezaji wa madini kutoka South Africa wamepewa migodi wanalipa kodi kidogo sawa na bure, wanachukua udongo kupeleka nje eti kwenda kuucheki kumbe wanatuibia.....Akili zako changanya na zake J en K..!!!
4. Wawekezaji wa Kufua umeme wa Siimbioni,TOL n.k ambao wanachuma mamilioni yetu walalahoi wa Kishapu...Akili zako changanya na zake j...k

Kwa kifupi hao ndo anaenda kuwatafuta ili waitafune nchi vizuri = '''AKILI ZAKO CHANGANYA NA ZAKE''
 
Nimesoma kwenye michuzi blog, JK ameenda UK leo asubuhi kwa ziara ya kikazi.

Ni juzi tu nilikuwa najiuliza kama ameshawahi kukaa japo mwezi akiwa ofisini anaangalia files au anasoma vitabu au ku'review' mambo mbalimbali yanayoendelea nchini sikupata jibu.

Vile imeandikiwa ziara siwezi kujua kama ina tija kwa Taifa au ila ifike wakati ambapo ziara zake ziwe zinaratibiwa ili kupunguza matumizi. Nchi yetu ni tajiri lakini inakuwa maskini kwasababu ya kutokuwa na maono na vipaumbele

Sidhani kama utapata jibu kwani unafikiri kwa kutumia kichwa na si ubongo.

Siku hizi ofisi ni ya kukutana tu na watu.

Ma faili na kila kitu unayapata hata ukiwa na ki BB mkononi. Mambo ya kukaa ofisini ni kizamani, office inakuwa ni popote ulipo. JMK ni kiboko, he is everywhere all the times, Hivyo ndivyo inavyotakiwa. Kukaa kaa sana ofisini unaweza kuota sugu za makalio.
 
Siku Mwenyezi akichukia, hiyo ndege itajateremka. Hapo ndipo kutakapokuwapo kilio na kusaga meno.
 
mwee...!!,kwani marais waliopita walikua hawasafiri?na kama walikua hawasafiri tulipata maendeleo ama vitamini gani ambao tunaikosa.mitanzania kwa lawama za kijinga hatujambo
 
kwanza amesafiri na shirika gani la ndege..? maana najua ile G5 bado iko savanna haijalipiwa.. mara ya mwisho aliondoka na Qatar Airways mpaka davos.. halafu akarudi na another commercial Airline mpaka Ethopia ambako alifuatwa na fokker 28 na kurudishwa home..
 
mwee...!!,kwani marais waliopita walikua hawasafiri?na kama walikua hawasafiri tulipata maendeleo ama vitamini gani ambao tunaikosa.mitanzania kwa lawama za kijinga hatujambo
 
Maybe kaenda kwenye huu mkutano
The London Conference on Somalia is being held on Thursday next week, February 23rd. Chaired by UK Prime Minister, David Cameron, over fifty
delegations are expected.

In addition to members of the international community and frontline states, there will be representatives from the TFIs, of the Puntland and Galmudug administrations, of Ahlu Sunna wal Jama’a, and from Somaliland. Last week, the UK Foreign
Secretary, William Hague, following his own visit to Mogadishu, laid out the UK’s aims for the
Conference including the need for a better
international strategy to address Somalia’s
problems and help its
people. He described a
more stable Somalia as vital to the UK’s national security, essential for the
stability for the Horn of Africa........
Continue Reading Here
 
Safari salama baba MwanaAsha.. maana nchi hii sasa inaongozwa na PM Pinda maana namuonekana Pinda kachakaa kama kandambili ya muuza karanga
 
Nimesoma kwenye michuzi blog, JK ameenda UK leo asubuhi kwa ziara ya kikazi.

Ni juzi tu nilikuwa najiuliza kama ameshawahi kukaa japo mwezi akiwa ofisini anaangalia files au anasoma vitabu au ku'review' mambo mbalimbali yanayoendelea nchini sikupata jibu.

Vile imeandikiwa ziara siwezi kujua kama ina tija kwa Taifa au ila ifike wakati ambapo ziara zake ziwe zinaratibiwa ili kupunguza matumizi. Nchi yetu ni tajiri lakini inakuwa maskini kwasababu ya kutokuwa na maono na vipaumbele

Cent ya mwisho hazina ikiisha atatulia
 
hamfikii yule raisi wa nigeria ambaye yeye kila wiki safari za nje eti anatembelea balozi na kujifunza yanayoendela huko
 
kwanza amesafiri na shirika gani la ndege..? maana najua ile G5 bado iko savanna haijalipiwa.. mara ya mwisho aliondoka na Qatar Airways mpaka davos.. halafu akarudi na another commercial Airline mpaka Ethopia ambako alifuatwa na fokker 28 na kurudishwa home..
kama ameondoka asubuhi basi atakuwa amesafiri na britishi airways ya saa kumi na mbili na nusu
 
Nimesoma kwenye michuzi blog, JK ameenda UK leo asubuhi kwa ziara ya kikazi.

Ni juzi tu nilikuwa najiuliza kama ameshawahi kukaa japo mwezi akiwa ofisini anaangalia files au anasoma vitabu au ku'review' mambo mbalimbali yanayoendelea nchini sikupata jibu.

Vile imeandikiwa ziara siwezi kujua kama ina tija kwa Taifa au ila ifike wakati ambapo ziara zake ziwe zinaratibiwa ili kupunguza matumizi. Nchi yetu ni tajiri lakini inakuwa maskini kwasababu ya kutokuwa na maono na vipaumbele

Kaenda kikazi kwani kaajiriwa na waTZ au waingereza?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom