Kaonewa? sijui....kitu kimoja ninachojua ni kwamba zamani corruption ilikuwa almost non existent kwenye primary schools kwa sababu kulikuwa hakuna pesa.Pesa zote zilikuwa halmashauri.
Halmashauri ndio zilikuwa responsible kununua kila kitu.
Issue kama hii ya ujenzi wa ukuta wakati huo,ni halmashauri ndio ingeamua na hapo shuleni wangeona tu ukuta unajengwa.
Lakini sikuhizi pesa za vitabu,ukarabati wa majengo na nk zinapelekwa moja kwa moja kwenye shule zinazohusika,na walimu wakuu wanazipiga kisawasawa!Kuanzia kwenye pesa za vitabu.Kuna wengine walishafungwa.
Kwangu mimi corruption ni corruption tu.Kwa hawa walimu,hicho ndio kiwango cha juu wanachoweza kuiba na wanaiba sana tu,ina maana hata ingekuwa ni bilioni or so,wangeiba.HAo wanaoiba mabilioni ni kwa sababu ndio pesa zilizo mbele yao.
Ninacholaani mimi,ni pale PCB wanapoenda kutumia resources kubwa tu kumkamata hakimu anayehongwa shs laki tatu au tano na kesho yake kuisoma kwenye gazeti-front page,wakati haohao wanasema mkataba wa Richmond ni swaaafi,lakini huo ndio ulimwangusha Lowassa NEC na bado unazua mjadala Bungeni na kwingineko.
Hapo tu!