JohnShaaban
JF-Expert Member
- Aug 23, 2007
- 464
- 114
Nahisi kama mwaka huu utakuwa mbaya kwa JK maana baadhi ya watendaji wake wameanza kumuonyesha jinsi gani anatakiwa kushughulikia issues kama BUZWAGI, BoT na nyingine ambazo zina utata. Una'act' promptly pale unapoona maslahi ya jamii yanachezewa!Mwalimu mkuu atimuliwa kazi kwa kusaini mkataba feki
2008-01-05 10:15:24
Na Francisca Jeremiah
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Abasi Kandoro, amemuagiza mkurugenzi wa halmashauri ya Kinondoni Bw. Noel Mahyenga kuwasimamisha kazi mara moja mwalimu mkuu wa shule ya msingi Makumbusho, afisa mtendaji wa kata hiyo, mratibu wa elimu wa kata hiyo pamoja na mwenyekiti wa kamati ya shule.
Hatua hiyo imefikia baada ya viongozi hao kuingia mkataba na kusaini hundi ya Sh. million 136, kati yao na mwekezaji mmoja ambaye jina lake halikufahamika, kwa makubaliano ya kujenga uzio wa shule hiyo utakaokuwa na maduka ya kufanya biashara kwa muda wa miaka 20, bila ya kupata kibali toka mamlaka husika.
Soma zaidi