Jitihada zinazofanywa na Zambia kutafuta mbadala wa bandari ya DSM zisipuuzwe

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Mar 29, 2012
10,223
22,299
Wakuu kwa muda mrefu nimekuwa nikitazama na kusoma jitihada mbalimbali zinazofanywa na serikali ya Zambia kupitia Rais wake Hakainde Hichilema kutafuta namna rahisi ya kusafirisha bidhaa zao kutoka ndani ya Zambia na za kuingiza nchini mwao bila kusahau zinazopita kuelekea nchi zingine hasa DRC. Bila kupepesa macho ni kuwa wazambia wanataka kuachana na Dsm port. Ingawa hawataweza kuachana na Dsm port kwa 100% lakini wataleta athari kubwa hasa kwa wakazi wa Tunduma. Bila Zambia ile Tunduma itakuwa hata nyuma ya Chato kibiashara.

Kwa msiofahamu ni kwamba tayari Zambia kwa kushirikiana na EU, US, Angola na DRC wanafanya jitihada za dhati kuhakikisha wanatumia bandari ya Lobito, Angola (Lobito Corridor). Uwepo wa hao mabeberu, EU & US, sio wa kuchukulia poa. Tusisahau pia Zambia, Msumbiji na Malawi wako kwenye jitihada za dhati kuhakikisha Nacala port, Mozambique inatumika huku wakiwa wameenda mbali zaidi kwa kuhakikisha reli kutoka Msumbiji, Malawi hadi Zambia inafanya kazi.

Kwa sababu za kijiografia, kiuchumi na zingine bado Dsm port haiwezi kuachwa ila biashara itapungua kama kweli hawa jamaa watafanikiwa malengo yao. Mimi ninawasihi wataalamu wetu waendelee na jitihada zao kuhakikisha wanakuwa mbele ya hawa majirani zetu kimkakati ili wasilete madhara kwenye biashara.
 
Diipii weldi wanasemaje kwani?
 
Back
Top Bottom