Jitahidi kuwa mpole unapokosewa na boss wako

Hell is real

JF-Expert Member
Aug 14, 2021
204
364
Habari wakuu!! Mara nyingi wanadamu hatufanani, kitabia, kimtazamo, na hata kimawazo!! Hivyo usishandane na mtu ambaye tiyari ana hasira juu yako kwa maana anaweza kufanya limpendezalo kwako(Mhubiri 8:3 Usifanye haraka kutoka mbele ya uso wake; usiendelee kufanya lililo baya; maana yeye hufanya lo lote limpendezalo. Mhubiri 8:4 Kwa kuwa neno la mfalme lina nguvu; naye ni nani awezaye kumwambia huyo, Wafanya nini?)

Hivyo ukiona mkuu wako au boss wako amekuwa juu!! Wewe kuwa mpole hilo ndo jibu ambalo biblia inatuelekeza tufanye sio kujibizana
(
Mithali 15:1 Jawabu la upole hugeuza hasira;
Bali neno liumizalo huchochea ghadhabu. Mithali 15:2 Ulimi wa mwenye hekima hutamka maarifa vizuri;
Bali vinywa vya wapumbavu humwaga upumbavu.)
Barikiwa sana wakuu
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom