Tanzania Mpya
JF-Expert Member
- Apr 11, 2012
- 252
- 145
Tabia zingine bwana sijui ni za asili? Tuna jirani yetu anatusumbua sana, yaani anasikiliza muziki kwa sauti kubwa sana na hana usiku wala mchana! Anaanza saa 11 asubuhi na anaweka sauti kubwa muda wote mpaka saa 5 au 6 usiku, yaani kelele tu. Yeye na mke wake wote wako hivyo na wana watoto wadogo sana, inanishangaza kwa kweli.
Mkewe huweka taarabu, mipasho kwa sauti kubwa sana, jamaa mwenyewe mfano asubuhi hii kaweka cd ya Remi Ongala (nafikiri kainunua jana) basi kaweka sauti kubwa sana wakati yeye mwenyewe kakaa nje ya nyumba yake akisikilizia. Jamaa ni Mndengereko, sasa sijui ni asili ya uswahili? Siku nyingi tu nilitaka nimfuate kumjulisha tatizo hili, lakini wife anasema huyu kuna analotafuta kwa majirani kwa hiyo tumuache tu na ulimbukeni wake.
Naomba ushauri wenu wadau, tutaishi hivi mpaka lini?