Jirani yetu limbukeni anatuboa

Jirani yetu limbukeni anatuboa

Enzi zangu nilikuwa nawakomesha wenye tabia hizo, baada yakuona nanyanyasika, niliamua kumfuata mshikaji wangu aliyekuwa na vyombo vya mziki vya kukodisha,

Nikamuomba viwe vinakaa kwangu,

Sasa limbukeni yule tuliyepanga nyumba moja akiwasha tu kiredio chake, mie namuwashia vyombo vyangu kwa mziki wa Bob Marley mpaka nyumba inatikisika!

Mbona aliamua yeye kwenda kwa mjumbe, mjumbe mwenyewe tayari nilishampa taarifa, hivyo akampuuza!

Mwisho aliama kuhama yeye!
 
Miziki mikubwa hata sisi tunayo ila huwa inafanya kazi hapo kwa hapo! Meaning ukifungua yako anazima then kesho anarudia! Sanasana labda na wewe uwe unafungua kila siku! (Sasa sijui una muumiza au unajiumiza mwenyewe)
Haina haja ya kubishana nae kufungulia muziki kila siku ndio maana nikasema mpaka akiwa anaumwa maana kuanzia hapo atajifunza kuwa anapofungulia muziki kwa sauti ya juu ajue kuwa wenzake huwa wanakuwa katika hali hiyo pia.
 
he he he, mbona mie si mdengereko ila kwa sauti tu, sijambo.

Heheh utakua tu ni jamii ile ile, kama si Mzaramo, M'kwere ambao sasa Tokomwile mmeifanya kidijitali zaidi...makelele mtindo
 
Tanzania Mpya; kwa Mjibu wa sheria za nchi na sheria ndogo za Manispaa hilo ni kosa. Ninao uhakika akiripotiwa vyombo husika Police au Serikali ya Mtaa ataacha. asiposikia anaweza kushtakiwa.

Pili hiyo ni Noise Pollution ambayo pia haitakiwi katika makazi ya watu.
 
Last edited by a moderator:
Pole sana mkuu, hao jirani zako, kwa akili yao wanadhani huo muziki unaufurahia pia, hivyo bila kuwaambia utaendelea kupigiwa mipasho mpaka Yesu arudi mara ya pili, sijui lini! Ushauri wangu ni kuwa vunja ukimya kawaambie for sure hawawezi kukupiga, ila nakusihi kama walivyosema wachangiaji wengine, please usiende ukiwa na hasira au namna yoyote ya kuonyesha umekerwa, utarudi umelowa matusi na mengine ya nguoni kutoka kwa hao jirani zako.
 
Mh hii imenikumbusha miaka ile maafande wametoka Uganda vitani, kuna afande mmoja tulikaa naye jirani jamani alikuwa mbabe anawasha mziki kwa sauti kubwa jaribu umwambie anatoka na kutishia usalama wenu.

Watu wakawa wanajifia kiofisa kelele mtindo mmoja na hajali mtu madent tulikuwa tunamlaani na weekly test zetu maana nayeye muzic ilikuwa anaupiga jmamosi na jmspili na jmatatu unatakiwa kwenda kupimwa shule!
 
aisee hapo kama ni mpangaji mwenzenu ni kumchana live tuu...ila uswahilini huwa tunaishi kwa kuvumiliana tu na sio kwa ustaarabu.......
 
Hahah kumbe ni Mdengereko....!!!
Baada ya ulimwengu kuhamia dijitali basi hata wao wamehama kutoka ngoma za "Mdundiko, Segere" nk na kuja kwenye ulimwengu wa kubofya...

Ila hao dawa yao ni moja tu, ongea na vishoka wa mtaani wapige shoti nyumbani kwake, hizo tabu hutazipata tena

hahahaha,how?
 
zungumza nae 2 atakuaelewa kwa hekma na busara haina haja ya kulumbana
 
Kuna jamaa mmoja alikua anasumbuliwa na wajinga wa dizain hii
"
Alipozifuma hela alienda kukodisha live band akawalipa wapige muziki mchana kutwa usiku kucha
"
Ilipofika saa kumi jioni jamaa alikuja kumuomba wapunguze sauti,yule mwenye live band akamwambia nadhani umeona kero ya kelele ilivyo
"
Tangu siku hiyo kukawa na utulivu
"
Ndugu yangu nenda kamshtaki kwa wahusika asiposikia zichange ukawaite wazee wa ngwasuma wapige sebene wiki nzima atie adabu
"
Punda haendi bila viboko!
 
We unapiga nyimbo nzuri tafuta nyimbo mbaya kama vile katitu ya wakenya halafu unafungulia full blast then mnatoka na my wife wako kutembea mnaacha unapiga, si dhani kama atarudia
 
Ukiona kabila ambalo watu wake wako radhi kuandaa ngoma for a millions on money halafu mtoto wao haendi xcul kwa kukosa ADA ujue lina matatizo! kuna mtu aliwahi kuniambia huwezi kukuta Mdengereko tajiri ila huwa wanapata tu nafuu ya maisha! maybe tunaweza kupprove, kaka kazi unayo kwa hao watu! full vijembe
Mkuu nenda kwao kawatie bakora familia nzima, ukishawatia mikwaju ya kutosha ndo uwaambie kwanini.... kesho hawatorudia tena kuweka sauti kubwa!!!!! :fencing:
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom