Jirani huyu kiboko

Jirani huyu kiboko

Hellow JF

Jirani ni mtu muhimu sana kwenye makazi kwa sababu yeye ndiye mtu wa kwanza kukusaidia pale unapopatwa na shida na unahutaji msaada ,ujirani ni muhimu sana kwa binadamu yoyote yule.

Huyu jirani yangu sijui ananijaribu kwa sababu anamtuma sana mwanaye kuja kuomba hapa home kuomba sio kosa kila mtu anahitaji msaada lakini huyu sijamuelewa.

Picha linaanza ikawa inaletwa simu kuchajiwa na kumbuka hapa sisi tumehamia hivi karibuni tu sio wenyeji kabisa kuna siku umeme wetu wa magumashi huu walikata tukawa kwenye Giza siku 2 hamna umeme dogo akatumwa alete simu mama kasema nilite simu ikae tu umeme ukija umchajie,baadaye akaja tena mama kanituma kama una sukari kidogo anaomba.

Siku nyingine akaja mama anaomba kitunguu kimoja kama unacho umpatie.
Jana sasa ndo kali akaja usiku mida ya saa moja hivi mama kasema anaomba umkopeshe mia tano nikamuuliza tena shilingi ngapi amekwambia akasema shilingi mia tano umkopeshe.Aisee Mungu anisamehe tu nikamwambia sina.

Halafu hapo anavuka nyumba kama 3 ndiyo inakuja nyumba ninayo kaa sasa wakat wa story na jiran mwingine akaniambia yaan hiyo nyumba ya chini hapo wakishakuzoea wanaomba hadi kero sabuni ya kuogea wanaomba sabuni ya kuoshea vyombo wanaomba mafuta ya kupakaa wanaomba yaan ni shida ,nikasema duh hapa kazi ipo kama ndiyo hivyo hapa inabidi kuwa kauzu sasa hivi.
Jirani kachangamka! 😄😄
 
Wakat mwinhn usifikir wanahiyo shida kweli mkuuu inakuwaga basi tuuu nong'wa umnyime aanze ubaya wake!!! Wakazie usiruhusu mazoea ya ajabu ndg heri nusu share kuliko .....!!! Heri wajue upendi mazoea mbuz kuliko kujifanya mwema kutaka kuwaridhisha ilihal ndo haohao kesho na kesho kutwa wanakupulizia!!!
umenena vyema
 
kama uwezo unao wewe msaidie tu ndio baraka zenyewe hizo,fanya kama unatoa sadaka.
 
Hellow JF

Jirani ni mtu muhimu sana kwenye makazi kwa sababu yeye ndiye mtu wa kwanza kukusaidia pale unapopatwa na shida na unahutaji msaada ,ujirani ni muhimu sana kwa binadamu yoyote yule.

Huyu jirani yangu sijui ananijaribu kwa sababu anamtuma sana mwanaye kuja kuomba hapa home kuomba sio kosa kila mtu anahitaji msaada lakini huyu sijamuelewa.

Picha linaanza ikawa inaletwa simu kuchajiwa na kumbuka hapa sisi tumehamia hivi karibuni tu sio wenyeji kabisa kuna siku umeme wetu wa magumashi huu walikata tukawa kwenye Giza siku 2 hamna umeme dogo akatumwa alete simu mama kasema nilite simu ikae tu umeme ukija umchajie,baadaye akaja tena mama kanituma kama una sukari kidogo anaomba.

Siku nyingine akaja mama anaomba kitunguu kimoja kama unacho umpatie.
Jana sasa ndo kali akaja usiku mida ya saa moja hivi mama kasema anaomba umkopeshe mia tano nikamuuliza tena shilingi ngapi amekwambia akasema shilingi mia tano umkopeshe.Aisee Mungu anisamehe tu nikamwambia sina.

Halafu hapo anavuka nyumba kama 3 ndiyo inakuja nyumba ninayo kaa sasa wakat wa story na jiran mwingine akaniambia yaan hiyo nyumba ya chini hapo wakishakuzoea wanaomba hadi kero sabuni ya kuogea wanaomba sabuni ya kuoshea vyombo wanaomba mafuta ya kupakaa wanaomba yaan ni shida ,nikasema duh hapa kazi ipo kama ndiyo hivyo hapa inabidi kuwa kauzu sasa hivi.
Weka picha yake
 
Nimekaa uswahilini. Nawajua wa hivyo. Itafika wakati fulani atataka kukupa mwili wake ili aombe zaidi kwa urahisi. Na ukikataa, mtakuwa maadui wakubwa. Usalama wako, kataa tangu mwanzo huko kwenye vitunguu, chumvi...
 
alafu ana mtuma binti yake sasa yeye mwenyewe hajawahi kuja huko kwenye mwili mume wake yupo wa kazi hiyo aisee
 
Wa hivyo kaa nao mbali sana Wachawi balaa anakuzoea wee kisha anakitafutia visa akufanyie ubaya.

watakuja akina mzee tola hapa kukuwakia ati uache uchoyo
Hivi mchawi kukuwangia mpaka aforce visa
 
halafu sasa mume wake ana wake wawili inakuwaje mme ana wake wawili mkewe anakuja kukopa jero
UKIONA KITU MZUNGU HAFANYI ACHANA NACHO MARA MOJA...Hakina faida! Mzungu kawazaa weee! Kachukua ruler kapima, kachukua venier caliper kapima, micrometer screw gauge kapima, thermometer kapima, Microscope kapima, kachukua vipimo vyote unavyojua kapima...mwisho kapata jibu wake wawili haina faida niwaachie waafrica tu..matokeo yake sisi bado tumeng'ang'ana nayo tuu, matokeo yake ndo hayo
 
Back
Top Bottom