Jirani anamaliza kuku wa watu

Kuna wengine wanafundishwa kutokusema 'hapana' na waume zao. Halafu wanafikiria ndio mtindo wa maisha. 99% of cheating married women wanafanya kama survival method (source: king'asti, 2020)
Hivi hao wake za watu hawajuagi kusema 'hapana'?
 
kizuri kwangu ni wao kuheshimu ndoa but naweza mkataza kwa jirani then akahamia kwangu mara mzinga wangu utakapo tu joh.

Mbona una wasiwasi sana? Unakula vya watu nini?

Sent from my BlackBerry 9100 using JamiiForums
 
Mimi naamini wanawake wote almost, they were innocent once upon a time. Mwalimu wa mwanamke ni mwanaume. Anatendwa weeeeh, hadi anajiuliza maybe nauchukulia huu mwili too serious. Mbona mwenzangu karelaksi na mwili wake? Anajionea what the hell? Ni hatari sana kujikuta unakuwa pushed to the point ya kukubaliana na stds ambazo sio zako. Ndo maana kuna mwanamke haoni hatari kila mwisho wa mwezi kuwa na dume jipya!
king'asti wewe ni 'jiniasi'
 
Hahaha! Naskiliza clouds hapa. Counsellor anasema kuna 'relationships tourists'. Hawezi kutunza mahusiano. Kumbe CV inahusika, aisee!
 
Acha umbeaaa! Mdomo uliponza kichwaaa! Pilipili ya shamba inakuwashia nini? We kuku sio wako akiliwa unapungukiwa nini? Wewe huwezi jua labda huyo mwanamke na njemba zinajuana na amehamia hapo SPECIFICALLY ILI WAWE CLOSE NA KUJILIA TUNDA LA MTI WA KATI bila kujali yaliyowakuta Adam na Hawa. Mwenzio alikuwa na kiherehere aliona ishu kama yako, kujitia ANGAZA akamuita yule mke wa mtu, na kumshauri aache uovu sio fare kwa mumewe blah! blah! blah! Kumbe yule dada namba ya mwananyamala, akaona picha ishaanza kuungua, alivorudi mumewe akamwambia kuna mpangaji(cha umbea) anamtokea tena anamganda na kamuahidi gari! Mumewe kachukia huyo ila kanyuti! Ikawa uzinzi anauendeleza huku haachi kumchomea cha umbea kwa mumewe, Mwisho cha umbea uzalendo ukamshinda akamuita mume mtu amueleze uasherati wa mkewe!!!! Loh! PATASHIKA LILILOTOKEA USITAKE KUSIA. Mume kangaka yaani kumtongoza my wife umeona haitoshi, sasa UNAMZUSHIA ILI NIMUACHE UMUOE WEWE???? Chaumbea kikamshuka shuuuu! shuuuuu!
 
Hayakuhusu, waache waendelee mpaka mwenyewe ashtuke, ukimwambia tu na ww utakuwa ni adui wa huyo jamaa, kwa kuwa wanaume wengine wazembe sana, anaweza kwenda kwa mkewe na kumuuliza kuwa jamaa anasema eti wewe unatembea na fulani.... mwanamke atakataa na atajitetea kuwa wewe ndiye unayemtaka. balaa litakurudia mkuu, achana nao endelea na mambo yako.
 
usinikumbushe,mimi mwenyewe Demu wa Rafiki yangu ambaye pia ni Demu wa Afisa Mmoja wa Juu Jeshini,ananishobokea na kuniletea stori za Mahaba kila tunapokutana,Anataka Muhogo,Mimi hata mshipa wa wazo kumpanda sina.Leo pia nimekutana nae yaani ataisoma namba nakwambia,Hawa Dada zetu wengi wao hewa sana siku hizi,hawaridhiki kabisa...
 
hebu geuza swali hili Nyani Ngabu kisha unipe jibu.

Hivi hao waume za watu hawajuagi kusema 'hapana'?

Jibu: Kikawaida mwanaume ndiyo hutongoza, hufukuzia, n.k. Na kwa asili ni vigumu sana kwa mwanaume kukataa ngono endapo mwanamke ataridhia. Hivyo, fursa ya mwanamke kufanikisha ama kutofanikisha uzinzi ni kubwa sana. Kwa minajili hiyo, mwanamke akisema 'hapana' basi huo uzinzi hautatokea. Na kwenye hii mada ni mwanaume ndiyo aliyemfukuzia hadi kumpata huyo mke wa mtu. Kwa hiyo huo ndiyo msingi wa mimi kuuliza hilo swali.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom