Jipatie Mbegu Bora ya Samaki Kambale kwa bei nafuu

BwanaSamaki012

Senior Member
Jan 13, 2023
114
139
Karibu nikuuzie mbegu bora ya Kambale kwa bei nafuu ya Tsh 300 kwa kifaranga kimoja.

Kambale ni aina ya samaki mstahimilivu na anayefugika kwa urahisi kuliko aina nyingine ya samaki. Mbali na kuwa mstahimilivu, pia wana sifa ya kukuwa haraka mara mbili zaidi ya sato.

Unaweza kuboreshe mazingira ya nyumbani au shambani kwako kwa kuanzisha kibwawa kidogo. Baada ya miezi kadhaa (6-9) utaweza kujipatia kitoweo cha uhakika na kuongeza kipato chako

Faida za kununua vifaranga kutoka kwetu:
 • Utapata uhakika wa mbegu bora ya Kambale
 • Bei nafuu ya Tsh 300 kwa kifaranga badala ya Tsh 500
 • Huduma ya ushauri bure kuanzia mwanzo hadi siku ya mavuno
 • Packaging na usafirishaji mzigo hadi Mkoa wowote ulipo

Tunapatikana Dar es Salaam - Bunju B.

Kwa maelezo zaidi na mawasiliano, tafadhali piga simu au tembelea shambani kwetu
Call/WhatsApp: 0758-779-170

 
Naweza kununua vifaranga elfu 1 halafu nikawatupia ziwani huko?

Je watastahimili mazingira ya ziwa Victoria?
 
Naweza kununua vifaranga elfu 1 halafu nikawatupia ziwani huko?

Je watastahimili mazingira ya ziwa Victoria?
Ndio inawezekana, lakini haishauliwi ni muhimu kufanya tathmini ya kina na kushauriana na wataalamu wa mazingira kabla ya kuchukua hatua kama hii ili kuzuia madhara yanayoweza kutokea. Pia, ni vyema kufuata sheria na taratibu za kitaifa na kimataifa kuhusu uzalishaji na kuingiza spishi mpya kwenye maji ya asili.
 
Pia tunazalisha na kuuza mbegu/vifaranga vya sato kwa wale wanaohitaji sato

Tunazo aina mbili mono-sex (all male fish) na mixed sex. Bei ni Tsh 250 kwa kifaranga
 

Attachments

 • VID-20240516-WA0073.mp4
  2.5 MB
Sample
 

Attachments

 • VID-20240516-WA0070.mp4
  479.7 KB
 • IMG-20240516-WA0064.jpg
  IMG-20240516-WA0064.jpg
  397.5 KB · Views: 3
Nataka nianzishe hii project kilimanjaro, nimepitiwa na kajito shambani kwangu, sitaki kuingia gharama za kuwalisha, je inawezekana kwa kuwawekea mazingira rafiki ili wale vile vilivyomo katika kajito hako!
 
Nataka nianzishe hii project kilimanjaro, nimepitiwa na kajito shambani kwangu, sitaki kuingia gharama za kuwalisha, je inawezekana kwa kuwawekea mazingira rafiki ili wale vile vilivyomo katika kajito hako!
Ndio Mkuu inawezekana, kihasiri samaki wanakula wadudu na mimea midogo midogo kitaalamu inafahamika kama zooplankton and phytoplanktons

Ukirutubisha maji unayofugia samaki kwa kuweka kiwango sahihi cha mbolea kwenye maji unachochea uzaliji wa wingi wa hiyo mimea na wadudu (Zooplankton & Phytoplanktons) ambayo ikiwepo kwa wingi samaki wanatumia kama chakula na kupunguza gharama za ulishaji

Njia nyingine ni kuzalisha mimie kama Azolla au wadudu mfano magotts, nje ya bwawa na kuwalisha wamaki wako

Kwa kambale kama unaweza unaweza kusanya vyura au samaki wadogo wadogo toka kwenye vyanzo vya maji na kuwapa kambale kama chakula
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom