JInsi ya kutunza uso kwa wanaume | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JInsi ya kutunza uso kwa wanaume

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Michael Amon, Mar 31, 2012.

 1. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #1
  Mar 31, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 707
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  NI jambo la kawaida kwa wanaume kutojali mambo yanayohusu urembo wakidhani ni kwa ajili ya wanawake tu, kitu ambacho si sahihi. Muonekano mzuri usoni kwa wanaume husababishwa na kujali vizuri ngozi na uso kwa ujumla.


  Wataalamu wa masuala ya urembo wanasema wanaume wana wajibu wa kujijali katika sekta zote za urembo kama wanawake wanavyofanya bila kupata madhara ya aina yoyote.

  Yafuatayo ni mambo muhimu ya kufanya ili mwanaume uwe na muonekeno mzuri usoni kama ifuatavyo:

  Tumia visafisha uso(facial cleanser), japokuwa wanaume wengi hawapendi kufanya hivyo.

  Takwimu zinaonyesha kuwa ni asilimia 15%tu ya wanaume hutumia njia hii kubiresha nyuso zao. Ndio maana wanaume wengi wanakuwa na mikunjo,madoa meusi, mba kubabuko katika ngozi zao.

  Visafisha uso vinasaidia kutoa uchafu na mafuta yaliyozidi kwenye ngozi na kuacha ngozi yako ikiwa nzuri kabisa.

  Kama uso wako una mafuta mengi basi tumia visafisha uso vyenye sabuni moja kwa moja au ‘jelly’ lakini na kama uso ni mkavu tumia ‘facial’ zenye mafuta.

  Jenga utamaduni wa kusugua uso wako kwa kutumia ‘scrubs’ aina ya ‘Eden Apricot’ kwa sababu inachenga ndogondogo ambazo zitakufanya usiumie tofauti na zenye chenga nene.

  Sugua uso wako angalau mara moja au mbili kwa wiki, hakika itasaidia kuondoa seli zilizokufa kwenye ngozi na kuifanya ngozi yako ya uso kuwa nadhifu na ya kuvutia.

  Paka scrub hiyo ukizungusha uso mzima pasipo kuelekeza msuguo kushuka chini kwani unaweza sababisha nyama za usoni kushuka na hatimaye kukufanya uonekane mzee.

  Safisha uso wako kwa maji baridi kisha paka uliyozoea kuitumia hakikisha haiakisi mwanga wa jua kwa urahisi hasa kama ukijua unaenda kutembea juani ili kuzuia ngozi yako isiathiriwe na mionzi mikali ya jua.

  Matumizi ya losheni pia yanategemea na aina ya ngozi yako mtu kama uso wako una mafuta mengi tumia zisizo na mafuta kama Nivea Milk itakayopunguza mafuta usoni ili uwezekano wa kutokwa na chunusi upungue.

  Ukitaka kunyoa ndevu zilowanishe na maji ya uvuguvugu kwa dakika 1au 2 kisha paka magic powder au krimu ya kuondoa ndevu iliyo na Vitamin E au Aloe vera .

  Baada ya ndevu kulainika unaweza toa kwa kifaa maalum kisha paka After shave ili kuwezesha vinyweleo visivyokuwa vya lazima kutoka

  Baada ya kumaliza hatua hiyo pakaa toner ili kuzuia vipele visiote na kusababisha muonekano mbaya usoni.

  Kama huna uwezo wa kupaka ‘toner’ au ‘after shave’ unaweza tumia mafuta yoyote yatakayoweza kulainisha ngozi yako.

  Tembelea saluni angalau mara moja kwa mwezi ili kusafisha uso wako kitaalam zaidi. Kufanya hivyo kutakusaidia kuondoa chunusi,mabaka meusi usiyoyapenda na vishimo vinavyotokana na chunusi zilizokomaa.


  E-mail: meezy@youngmaster.co.tz
   
 2. gozo

  gozo JF-Expert Member

  #2
  Mar 31, 2012
  Joined: Sep 15, 2011
  Messages: 460
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  dah sasa kwa mimi ambae hata hela ya kula ni shida hiyo hela ya kwenda baber shop kusafisha uso ntaitoa wapi?mwee!
   
 3. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #3
  Mar 31, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 707
  Trophy Points: 280
  Tatizo lako wewe mbishi. Nilikwambia ulichukue lile jimama lililokuwa linakutaka ukajidai unaringa matokeo yake sasa hivi unakula joto ya jiwe. Ungekuwa unang'aa sasa hivi mkuu.
   
 4. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #4
  Mar 31, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  Mwanaume anafanya scrub, anatumia cleanser na toner!
  Aisee!
   
 5. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #5
  Mar 31, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Mwanamme asifiwi sura,mwanamme kazi stukaaaa!!!
   
 6. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #6
  Mar 31, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 160
  aisee ulikuwa wapi?
  Nina kesi sana na wewe, kwa nini ulipotea??

   
 7. SALOK

  SALOK JF-Expert Member

  #7
  Mar 31, 2012
  Joined: Sep 20, 2011
  Messages: 2,675
  Likes Received: 866
  Trophy Points: 280
  kongosho umerudi? Kweli jela mbaya umekondaaaa!
   
 8. bht

  bht JF-Expert Member

  #8
  Mar 31, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  mle vizuri na kupumzika vya kutosha pia...
  Sio mnakesha vilabuni, bia na choma halafu mnategemea scrub, cleanser na toner ndo zinalainisha na kufanya ngozi nyororo
   
 9. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #9
  Mar 31, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Neno hili...
   
 10. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #10
  Mar 31, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 707
  Trophy Points: 280
  Message imewafikia walengwa mkuu.
   
 11. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #11
  Mar 31, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 707
  Trophy Points: 280
  Kwani cha ajabu nini hapo?
   
 12. Negrodemus

  Negrodemus JF Gold Member

  #12
  Mar 31, 2012
  Joined: Dec 30, 2010
  Messages: 2,128
  Likes Received: 101
  Trophy Points: 160
  Huon kuna utofaut?
   
 13. WaliNazi

  WaliNazi JF-Expert Member

  #13
  Apr 1, 2012
  Joined: Mar 7, 2012
  Messages: 853
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  .....young master waanza nipa wasiwasi...
   
 14. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #14
  Apr 1, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 707
  Trophy Points: 280
  Wasi wasi gani?
   
 15. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #15
  Apr 1, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 707
  Trophy Points: 280
  Kwani wale wanaume wanaofanya kazi saloon sio watu? Inamaana wanaume hawatakiwi kujifunza mambo ya urembo?
   
 16. WaliNazi

  WaliNazi JF-Expert Member

  #16
  Apr 1, 2012
  Joined: Mar 7, 2012
  Messages: 853
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33

  ....unafanya kazi gani...!?
   
 17. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #17
  Apr 1, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 707
  Trophy Points: 280
  Mimi ni IT Technician
   
 18. Muuza Sura

  Muuza Sura JF-Expert Member

  #18
  Apr 1, 2012
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 1,990
  Likes Received: 218
  Trophy Points: 160
  Kama ni kosa kutumia!nadhani mimi ntakuwa mkosa na kuendelea kuwa mkosa!
   
 19. Muuza Sura

  Muuza Sura JF-Expert Member

  #19
  Apr 1, 2012
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 1,990
  Likes Received: 218
  Trophy Points: 160
  kama una sura nzuri inabidi uiharibu ili uonekane mwanaume?mauzo muhimu!
   
 20. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #20
  Apr 1, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 707
  Trophy Points: 280
  Mwambie huyo mkuu maana watu wengine wanadhani kuwa na sura kama fenesi ndio uwanaume.
   
Loading...