Nini maana ya ngozi 'Ku glow'?

Nini maana ya ngozi 'Ku glow'?

Mawele

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
896
Reaction score
3,058
Neno 'Glow' limeshika kasi kwenye tasnia ya urembo, wauzaji wa vipodozi wanauza wakisema ukitumia utaglow, huku na watumiaji wakionesha ngozi zao kuwa zimeglow.

Cha ajabu wapo ambao wanashare video huku nyuso zikiwa zimenona futa kama wametoka kukaangwa au kulowekwa kwenye mafuta ya yile Mtume na nabii, huku wakijisifia kiwa tangu waanze kutumia kitu fulani wameglow au wamekiwa wekundu kwa kukoboa ngozi.

Najiuliza, kugolow ni uso kunona mafuta, au kukoboa ngozi au ni kuwaje? Naomba kufahamishwa maaana mpaka sasa nachanganyikiwa mwenzenu.
 
Neno Glow limeahika kasi kwenye tasnia ya urembo, wauzaji wa vipodozi wanauza wakisema ukitumia utaglow, huku na watumiaji wakionesha ngozi zao kuwa zimeglow.

Cha ajabu wapo ambao wanashare video huku nyuso zikiwa zimenona futa kama wametoka kukaangwa au kulowekwa kwenye mafuta ya yile Mtume na nabii, huku wakijisifia kiwa tangu waanze kutumia kitu fulani wameglow au wamekiwa wekundu kwa kukoboa ngozi.

Najiuliza, kugolow ni uso kunona mafuta, au kukoboa ngozi au ni kuwaje? Naomba kufahamishwa maaana mpaka sasa nachanganyikiwa mwenzenu.
Hapa sasa wazee wa michubuko na kukoboa watatusaidia Ila kwa akili zangu ndefu nyembamba nahisi kuwa kuglow ni kuwaka

Asanteni
 
Wana paka mafuta mengi, wanameremeta kama kitumbua wanadai wameglow.

Na huku uswahilini kwetu wanajichubua wanasema wameglow kasheshe tu.

Ngozi ikiwa hydrated inakuwa radiant na plump ndio glow.
oooh!!!! nimeelewa.

Binti yangu aliniletea upuuzi huo wa ku glow akaja na product sizikuzielewa nikampiga mkwala,, nikamwambia humu tunatumia clear essence tu.
akianza kujihudumia ndio ataingia huko
 
Back
Top Bottom