Smart Finance
Member
- Apr 10, 2025
- 35
- 112
Imeandaliwa na Smart Finance SW
Nimekuwa nikifuatilia ushauri wa watu mbali mbali kwenye hii platform na platform zengine huko zinazohusiana na mswala ya fedha. Nilichogundua watu wengi au washauri wengi wanapenda sana kutumia nyakati zilizopita wanapotoa ushauri au kuelezea juu ya fursa fulani.
Utasikia "kama ungewekeza kiasi Fulani wakati Fulani, ungekuwa umetengeneza kiasi Fulani" si jambo baya na napenda jinsi wanavyotoa mifano hai inayosaidia watu kuelewa masuala ya uwekezaji na fedha Kwa urahisi kama wao wanavyodhani.
Ila kiukweli watu wengi hii inawakata sana, unajua binadamu anahamasika zaidi anaposikia fursa zilizo mbele yake badala ya zile alizokosa. Mimi naona tunapotoa ushauri juu ya jambo linalohusu uwekezaji tujaribu kuangazia zaidi hatua tunazoweza kuchukua sasa na fursa zilizopo kwa wakati huu.
Kuna njia nzuri ya kufanikisha ushauri wa kifedha kwa kuzingatia mbinu za sasa na baadaye, badala ya kuangalia tu historia. Hii inaweza kusaidia watu kujisikia kuwa bado wana nafasi ya kuchukua hatua sahihi.
Unajua watu wengine wanakata tamaa wakiona mfano wa fursa waliyoikosa. Mfn unamwambia mtu kama ungewekeza 20M kwenye hisa za CRDB mwaka 2019 now ungekuwa na 118M.. Huyo mtu atajisikiaje? Pengine kwa kumpa mwelekeo wa nini anaweza kufanya sasa kunaweza kumsaidia zaidi. Kuliko kumuonesha Kwa kiasi Gani amekuwa akipoteza muda na faida Kwa miaka mingi nyuma.
Ni ushauri tu lakini, sio lazima ufuatwe. All in all "Tuendelee Kujifunza"
Follow the Smart Finance - SW channel on WhatsApp: Smart Finance - SW | WhatsApp Channel