Jinsi ya kupika tambi

Paul S.S

Verified Member
Aug 27, 2009
6,084
2,000
Wadau wa jukwaa hili naombeni utaalamu wenu kuntu, hatua kwa hatua ya namna bora ya kupika tambi zikawa hazikatiki katiki wala kushikamana kama wali.

Zikawa nzuri na wakati wa kula unaweza kuifyonza tambi moja mwanzo mwisho kama tuonavyo kwenye matangazo.

Natanguliza shukrani.

==========
1593781855376.png

Tambi za hiliki na sukari
Tambi ni rahisi kupika, lakini ladha yake ni tamu. Mchanganyiko wa rangi unakupa hamu ya kula. Unaweza kula pamoja na nyama (kuku, sausage, mbuzi, ng’ombe) au salad ili kuongeza ladha na vilevile rangi tofauti za vyakula.

Ni vizuri pia kama ukila chakula hiki kwa salad ya nyanya, pilipili hoho na karoti ambayo inaongeza appetite sababu ya mchanganyiko wa rangi mbalimbali.

Mahitaji
 • Tambi 500g
 • Sukari vijiko 2 vikubwa
 • Hiliki 3
 • Mafuta ya kupikia 1/4 lita
Maelekezo
Chakula hiki utapika katika sehemu mbili, ya kwanza ni kukaanga na ya pili ni kuchemsha. Kisha utachanganya ili kupata mchanganyiko maridhawa wa mlo kamili. Ni vizuri kama utafanya vyote wakati mmoja, ila kama huna nafasi jikoni unaweza kuanza na kimoja kisha ukamalizia na kingine.
 • Anza kwa kumenya hiliki, kisha hifadhi maganda.
 • Toa tambi kwenye packet, kisha gawa kwenye makundi mawili – kundi moja tambi za kukaanga na lingine za kuchemsha.
 • Anza kuandaa kama ilivyoelezwa hapa chini. Ni vizuri kama utafanya hizi hatua kwa pamoja ili tambi zipate kuiva kwa muda mmoja.
Tambi za Kukaanga
 • Bandika sufuria au kikaango cha mafuta jikoni, acha yachemke vizuri.
 • Mafuta yakishachemka, ongeza fungu moja la tambi ulizotenga (Za kukaanga). Acha kwenye mafuta kwa muda kiasi hazi zianze kubadilika rangi. Ni vizuri kama hutoacha tambi zibadilike sana rangi kuwa za brown, maana zitaungua na kutokuwa na ladha nzuri.
 • Epue tambi mapema kupata rangi ya wastani. Zitakuwa zimeiva vizuri tu.
Tambi za kuchemsha
 • Bandika chungu au sufuria ya maji jikoni kwa ajili ya kuandaa tambi za kuchemsha.
 • Weka maganda ya hiliki kwenye maji ya moto ili kuweka harufu nzuri kwenye tambi. Baada ya dakika kama 5 unaweza kuchuja maganda ya hiliki na kubaki na maji yenye harufu ya hiliki.
 • Chukua kiasi cha tambi zilizosalia, weka kwenye maji ya moto, kisha ongeza sukari na hiliki.
 • Subiria tambi zichemke kutokana na muda ulioshauriwa - dakika 5 hadi 7 - ili zisiwe na kiini kigumu ndani. Hapo tambi zako zitakua zimeiva.
Changanya Tambi
 • Changanya tambi za kukaanga na tambi za kuchemsha pamoja. Katika hatua hii unapata mchanganyiko wa rangi tofauti za tambi, harufu nzuri ya hiliki na utamu wa sukari unamalizia.
 • Usisahau kutoa maoni kama ukishapika na kuonja ladha ya chakula hiki.

Michango ya wadau
1.Hatua ya kwanza unakata tambi kwa ukubwa unaotaka kama unataka kushika moja moja unakata mara tatu.

2. unachemsha maji jikoni yakichemka unatia chumvi halafu unatia tambi zako.

3. unazichemsha kwa muda wa dakika kumi na tano ziive zisirojeke sana, unamwaga yale maji unaacha tambi zenyewe, hakikisha umemwaga maji yote.

4.Baada ya kumwaga maji unatia mafuta kiasi unachopenda unachanganya tambi na mafuta unaacha ichemke kwa dakika kumi hakikisha wakati zinaiva na mafuta moto wako uwe mdogo , Wengine hupendelea kuweka blueband badala ya mafuta inategemea wewe unapenda nini.

5. Baada ya hapo zitakuwa tayai kwa kuliwa.
----
Okay, Benvenuto! (karibu, kiitaliano). Nitakufundisha mimi, twisheni pia ipo.

Ni hivi; Tambi ama Spaghetti kwa kiingereza, ni aina mojawapo ya vyakula vitokanavyo na ngano kundi la Pasta. Hivyo pasta zipo nyingi ikiwemo tambi zenyewe/Spaghetti, zingine ni fusil, penne, ravioli, tagliatelle, macharonne na nyingine nyingi tofauti tofauti zaidi ya mia moja.

Zipo pia pasta maalumu kwa ajili ya supu tu, kwa kawaida huwa ni ndogondogo wakati mwingine karibia na mchele. Pasta zote zikiwemo tambi au spaghetti zinaweza kuwa ni kavu (zile zilizopo dukani) ambazo mara nyingi hutengenezwa viwandani na pia zinaweza kuwa fresh (yaani unatengeneza mwenyewe na kuzipika papo hapo), karibu aina zote za pasta zinaweza kuandaliwa na kupikwa zikiwa fresh. Hata tambi zipo fresh, Mi kwa ujumla hupendelea pasta fresh kwa sababu zinaradha ya aina yake nzuri tofauti na zile za dukani. Kama hujawahi hili unaweza usinielewe.

Tambi au pasta karibu zote zinaweza kuwa za rangi pia, unaweza kutengeneza za blue, za kijani, nyekundu, za brown na kadharika na kadharika. Mhimu ni utumie natural coloring agents (usitumie rangi za viwandani sababu zina kemikali, ni tetesi lakini). Kama unataka za kijani kwa mfano, wakati unaandaa unga wa ngano tayari kwa kukandwa kuandaliwa kuwa pasta, ongeza kiasi kidogo cha mchicha uliochemshwa kidogo na kusagwa unga baada ya kuchujwa maji. Mwisho utapata pasta au tambi za rangi ya kijani.

Nimesema twisheni ipo, sasa nisije sababisha usirequest twisheni bure...........

Namna ya Kuchemsha tambi:
Bado kuna mkanganyiko wa juu ni wapi tambi au chakula jamii ya pasta kiligunduliwa kwa mara ya kwanza, baadhi ya wanataaluma wanadai ni China ndiko pasta ziligunduliwa na wengine wanadai ni Italia ndiko ziligunduliwa. Bali inajulikana kote duniani kuwa ukienda nchi yeyote ukakuta mgahwa au hotel ya kiitalia (Italian hotel/restaurants), usipokuta tambi au pasta, basi hapo siyo penyewe!.

Kwa mjibu wa kitabu cha Paolo Urbani alichoshirikiana na Silvano Rodato kiitwacho Laboratorio di Cucina ukurasa wa 190:

 • Tambi au pasta hupikwa katika maji mengi ya kutosha yaliyochemka kufikia nyuzi joto 100, yaani yamechemka.
 • Uwiano ni maji lita 10 kwa kila kilo 1 ya pasta/tambi.
 • Kamwe usijejaribu kuongeza maji ya baribi ndani ya maji hayo ya moto yanayoendelea kuchemka ya tambi au kuzinyunyiza tambi/pasta maji ya baridi baada ya kuzichuja toka maji moto kwa madai kuzisimamisha zisiendele kuiva.
 • Pasta/tambi ni chakula kinachopikwa na kuandaliwa katika hali ya haraka na kutokusimama kushangaa chochote, unapotumbukiza tambi unatakiwa ujihakikishie kuwa huna kazi nyingine itakayokufanya upunguze moto au umsubiri fulani, inatakiwa unaona wote wamekaa mezani ndo unatumbukiza tambi kwenye maji. Mara nyingi waitaliano wengi wanapokuwa njiani kurudi majumbani mwao wanapokaribia na kukunja kona ya mwisho kuingia mtaani kwao huwapigia simu waume au wake zao watumbukize tambi/pasta kwenye maji (buta la pasta!).
 • Mhimu kuliko yote ni kuwa hadi mwishoni mwa kuchemka na hadi kuungwa kwa pasta zako, ni lazima uhakikishe zinabaki bado ni ngumungumu kidogo yaani zinasikika katika meno, kama ni wali unasema bado una kiini (al dente!).

Okay hatua za kuchemsha tambi;
Mahitaji:

 • Tambi kilo 1
 • Maji yaliyochemka lita 10
 • Chumvi ya jikoni gramu 100
 • Mafuta ya kupika (vizuri kama unapata ya zeituni) robo kikombe
MHIMU SANA: Tafadhari tambi haziongezwi sukari kwa sababu yeyote ile.

Namna ya kupika:

 • Tumbukiza tambi zako kwenye maji yaliyochemka vya kutosha yenye chumvi na mafuta ya kupikia. MHIMU, USIZIVUNJE HATA MARA 1 TAMBI IWE KABLA AU UNAPOCHEMSHA!!!, tambi zichemshwe kwa urefu wake wa asili, hii ndiyo sababu uma (fork) ndio hutumika kulia tambi na siyo kijiko wala mkono!!!, unachomeka uma, unazungusha kupata kifundo cha tambi utakazoweza kuzimeza, unatumbukiza mdomoni.
 • Unatakiwa kuzikoroga mara kwa mara kwa kutumia uma mkubwa mrefu, iweleke ninaposema mara kwa mara haina mana basi mtu ashike kiuno na asimame hapo akikoroga tambi kama anakoroga uji wa ugali, unakoroga dakika 2 au 3 unapumzika kisha unarudia tena.
 • Unatakiwa kuzionja moja moja kila mara ili kuvizia zinapoanza kukaribia kuiva uzitoe haraka, usipofanya hivyo lazima utapoteza point, pale unapotaka kujuwa kama tayari zimeiva kumbe ziliiva kitambo kwa sababu we ulikuwa huonjihuonji kabla ili kuzivizia.
 • Kisha kukaribia kuiva tambi huchujwa toka katika maji na kuziunganisha na sauce (sosi) ambayo umeamua kuitumia kuungia tambi zako siku hiyo. Kwa kawaida sosi huandaliwa kabla ya kuchemsha pasta, au huku unaandaa sosi huku maji ya tambi yanachemka. Zipo Sosi (pasta sauce) zaidi ya 100, kila sosi ina jina lake na mahitaji yake maalumu, kadri unavyobadilisha aina ya sosi ndivyo na jina la tambi au pasta uliyopika linavyobadilika. Kwa uchache kuna sosi ya nyanya (tomato sauce), sosi nyeupe (white sauce, hii maziwa hutumia zaidi), sosi ya nyama ya kusaga (bolognaise sauce/minced meat sauce), Fish ragu', amatriciana, alla romana. alio-olio-peperoncino, na kadharika na kadharika.
 • Mifuko mingi ya pasta/tambi huandikwa kabisa dakika za kuchemshwa ubavuni mwake tangu kiwandani.

Nikuchagulie pishi moja la tambi litakalokuduwaza?
----
Tambi
Mahitaji:
1. Kitunguu kikubwa kimoja
2. Nyanya mbili kubwa
3. Karoti kubwa moja.
4. Pilipili Hoho Nusu
5. Tambi gram 250
6. Mafuta ya kupikia
7. Chumvi
8. Nyama ya kusaga 1/4 Kg
9. Tangawizi
10. Limao
11. Kitunguu swaumu

Matayarisho
1. Weka sufuria jikoni, weka mafuta na ukaange vitunguu maji vikifatiwa na vitunguu swaumu
2. Baada ya hapo, chukua nyama yako ya kusaga na uitie kwenye sufuria yenye vitunguu vyote.
3. Kisha tia tangawizi kwenye nyama huku unaendelea kuikaanga, baadae tia nyanya, hoho na karoti
4. Ipua na uweke pembeni
5. Chukua sufuria nyingine, weka maji na uibandike jikoni mpaka maji yachemke
6. Maji yakisha chemka, weka chumvi kiasi na uzitie tambi zako
7. Ukiona zimelainika kiasi, yachuje maji yoote na tambi zibaki kavu.
8. Chukua ule mchanganyiko wako wa viungo na tia tambi zako na uziache jikoni kwa dakika 5 hivi..
9. Hapo zitakuwa tayari kwa kuliwa...
----
Tambi ni mmoja ya vyakula ambavyo unaweza kuandaa kwa haraka sana,uandaaji wake hachukua muda mfupi sana.Ni moja vile vyakula ambavyo mimi huandaa nikiwa nimechelewasha chakula au sina muda wa kupika.

Kuna namna na jinsi nyingi sana ya kuandaa tambi.Unaweza andaa tambi kama mlo mkuu,mlo wa pembeni au kuzitumia kwenye salad.

Jana niliandaa tambi kama mlo mkuu kwa ajili ya chakula cha jioni.

Mahitaji

 • Tambi robo paketi(paketi kubwa)
 • Karoti 1 Kubwa
 • Njegere robo kikombe
 • Vitunguu maji 2
 • Hoho 2
 • Soseji 3
 • Carry powder vijiko viwili vya chai
 • Chumvi
 • Salted Butter vijiko 3 vya chakula

Njia

1.Chemsha tambi,chemsha ngegere,chemsha soseji kisha chuja maji yote.weka pembeni
2.Osha na kata mboga zote za majani kwa urefu
3.Katika kikaango weka butter na karoti kisha weka jikoni ukaange kwa moto mdogo ili butter isiungue. Kaanga kwa muda mfupi tu,ili butter iingie kwenye karoti.

4.Ongeza vitunguu na njegere,kisha nyunyuzia carry powder kwa juu,kaanga kwa muda kidogo .
5.Ongeza Tambi na hoho kisha endelea kukaanga na kugeuza ili vichanganyike.
6.Ongeza Soseji zilizokatwa katika vipande vidogo kisha nyunyuzia chmvi na endelea kukaanga kwa muda kidogo tu ili chumvi iive.
7.Kikiwa tayari ,epua na utenge mezani.chakula hiki kinapendeza zaidi kikiliwa chamoto kabla butter haijapoa.

Chakula hiki kinatakiwa kupikwa kwa muda mfupi sana,kuanzia pale unapoanza kuweka mboga za majani kwani lengo ni kutokuivisha sana mboga hizo,zinatakiwa kuiva kwa juu tu.
Unaweza sindikiza chakula hiki na sosi ya aina yoyote ukipenda.Sisi hupenda kula chakula hiki

kama kilivyo bila sosi wala mchuzi wowote,tunafurahia harufu ya butter na carry powder tunapokula hivyo kuweka mchuzi au sosi ni kuaribu ladha na harufu hiyo.
Chakula hiki ni rahisi sana kuandaa ,ni cha haraka na nikitamu sana.

KAZI KWAKO.
----
Tambi (vermicilli)za maji

Recipe

Tambi vermicilli half packet (250grms)
 • Sukari nusu kikombe.
 • Cardamon powder (iliki)1 teaspoon.
 • Mafuta kiasi.
 • Maji nusu lita
Jinsi ya kupika
Bandika sufuria, weka mafuta yakipata moto weka tambi ukoroge hadi ziwe kahawia "golden brown" . kisha weka maji,.sukari na iliki, koroga acha ziive, kisha osha "dried grapes" (zabibu kavu) weka ndani ya tambi.koroga vizuri na hakikisha zimeiva, tambi zinakuwa tayri kuliwa.

View attachment 1435864
----
Mahitaji
Tambi View attachment 519162
Maji\maziwa\tui la nazi
Chumvi\sukari
Mafuta ya kupikia
Viungo mfano hiliki
Soseji View attachment 519161

Chemsha maji\maziwa au tui la nazi kiasi jikoni weka hiliki,chumvi na sukari kidogo

Chukua soseji kata vipande vitatu,chomeka tambi kama inavyoonekana pichani,fanya hivyo kwa soseji zote. View attachment 519163

Weka mchanganyiko wako wa tambi na soseji kwenye maji yaliyochemka jikoni

Tambi zikishalegea weka mafuta ya kupikia humo humo kisha pika au kaangiza kama kawaida mpaka msosi uive.

unaweza ongezea pia ujuzi kwa aina hii ya upishi
 
Joyceline

JF-Expert Member
Jan 9, 2009
1,010
0
1.Hatua ya kwanza unakata tambi kwa ukubwa unaotaka kama unataka kushika moja moja unakata mara tatu.

2. Unachemsha maji jikoni yakichemka unatia chumvi halafu unatia tambi zako.

3. Unazichemsha kwa muda wa dakika kumi na tano ziive zisirojeke sana, unamwaga yale maji unaacha tambi zenyewe, hakikisha umemwaga maji yote.

4.Baada ya kumwaga maji unatia mafuta kiasi unachopenda unachanganya tambi na mafuta unaacha ichemke kwa dakika kumi hakikisha wakati zinaiva na mafuta moto wako uwe mdogo , Wengine hupendelea kuweka blueband badala ya mafuta inategemea wewe unapenda nini.

5. Baada ya hapo zitakuwa tayai kwa kuliwa.
 
Paul S.S

Verified Member
Aug 27, 2009
6,084
2,000
1.Hatua ya kwanza unakata tambi kwa ukubwa unaotaka kama unataka kushika moja moja unakata mara tatu.
2. unachemsha maji jikoni yakichemka unatia chumvi halafu unatia tambi zako.
3. unazichemsha kwa muda wa dakika kumi na tano ziive zisirojeke sana, unamwaga yale maji unaacha tambi zenyewe, hakikisha umemwaga maji yote.
4.Baada ya kumwaga maji unatia mafuta kiasi unachopenda unachanganya tambi na mafuta unaacha ichemke kwa dakika kumi hakikisha wakati zinaiva na mafuta moto wako uwe mdogo , Wengine hupendelea kuweka blueband badala ya mafuta inategemea wewe unapenda nini.
5. Baada ya hapo zitakuwa tayai kwa kuliwa.
Thanks Joyceline kwa maelezo, vipi kama nataka kuweka na vikorombwezo vingine kama karoti,majani ya vitunguu,hoho nyanya kama zinawekwa nk nk

Hiyo ilionipa darasa itakuwa plain sana.
 
Last edited by a moderator:

Mentor

JF-Expert Member
Oct 14, 2008
20,357
2,000
The SIMPLEST n BEST way out of that dilema is to GET MARRIED...
Au jaribu ile ya kuzikaanga (for lack of a better word) ile kabla hujaweka maji. Kama vile unapika zile za sukari.

Yaani weka mafuta kidogo kwenye sufuria..then tia ndani tambi zako kama unavokaangaga kitunguu (mimi hupendelea kuzikata mara mbili)...zitabadilika rangi na kuwa brown..then tia maji na chumvi kiasi. Uzur wa hii koz zipo sufurian tayar unaeza kukadiria maji kiurahisi zadi.

But as i said before...ukioa utashangaa tambi zako zenyeewe zinanyonyka mpaka mwisho. Au kwenye adverts uliona mwanaume akipika??! Lol ;-)
 
BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
99,507
2,000
The SIMPLEST n BEST way out of that dilema is to GET MARRIED...
Au jaribu ile ya kuzikaanga (for lack of a better word) ile kabla hujaweka maji. Kama vile unapika zile za sukari.
Yani weka mafuta kidogo kwenye sufuria..then tia ndani tambi zako kama unavokaangaga kitunguu (mimi hupendelea kuzikata mara mbili)...zitabadilika rangi na kuwa brown..then tia maji na chumvi kiasi. Uzur wa hii koz zipo sufurian tayar unaeza kukadiria maji kiurahisi zadi.
But as i said before...ukioa utashangaa tambi zako zenyeewe zinanyonyka mpaka mwisho. Au kwenye adverts uliona mwanaume akipika??! Lol ;-)

Kumbe mpishi mzuri eeh! Hizi za hapo kwenye rangi ndizo ambazo mimi huzipenda.
 
King'asti

JF-Expert Member
Nov 26, 2009
27,739
2,000
Kuna tambi flani nyembamba kama mchele, tamu sana. Nazo unakaanga kidogo then unataia maji kidogo. Joyceline, mimi huchemsha na mafuta pia kwenye maji (kama sijazikaanga). Baada ya kuchuja maji, naweka cheese kiduuchu

Recipe ya kivivu hii hapa.
kaanga kitunguu na nyama iliyochemshwa kiwe brown,Weka spices (binzari kidogo)

Tia nyanya zipikwe hadi ziive kabisa.
tia tambi, zikoroge kidogo then tia maji ya moto kiasi cha kufunika tambi
zisipoiva ongeza maji kidogo. Angalia maji yasizidi. Baada ya kuiva, weka karoti zilizokatwakatwa, majani ya vitunguu na hoho. Changanya kisha serve (wakati karoti na hoho bado crunchy)

Unapata msosi full suti, nusu saa inatosha kwa upishi huu.
 
Last edited by a moderator:

Jakubumba

JF-Expert Member
Mar 5, 2011
1,625
1,195
The SIMPLEST n BEST way out of that dilema is to GET MARRIED...
Au jaribu ile ya kuzikaanga (for lack of a better word) ile kabla hujaweka maji. Kama vile unapika zile za sukari.
Yani weka mafuta kidogo kwenye sufuria..then tia ndani tambi zako kama unavokaangaga kitunguu (mimi hupendelea kuzikata mara mbili)...zitabadilika rangi na kuwa brown..then tia maji na chumvi kiasi. Uzur wa hii koz zipo sufurian tayar unaeza kukadiria maji kiurahisi zadi.
But as i said before...ukioa utashangaa tambi zako zenyeewe zinanyonyka mpaka mwisho. Au kwenye adverts uliona mwanaume akipika??! Lol ;-)
Hata sijakupata
 
Mentor

JF-Expert Member
Oct 14, 2008
20,357
2,000
Kuna tambi flani nyembamba kama mchele, tamu sana. Nazo unakaanga kidogo then unataia maji kidogo. Joyceline, mimi huchemsha na mafuta pia kwenye maji (kama sijazikaanga). Baada ya kuchuja maji, naweka cheese kiduuchu

Recipe ya kivivu hii hapa.
kaanga kitunguu na nyama iliyochemshwa kiwe brown,Weka spices (binzari kidogo)
tia nyanya zipikwe hadi ziive kabisa.
tia tambi, zikoroge kidogo then tia maji ya moto kiasi cha kufunika tambi
zisipoiva ongeza maji kidogo. Angalia maji yasizidi. Baada ya kuiva, weka karoti zilizokatwakatwa, majani ya vitunguu na hoho. Changanya kisha serve (wakati karoti na hoho bado crunchy)

Unapata msosi full suti, nusu saa inatosha kwa upishi huu.
Hahahah King'asti kama unanionaga vile. Ila mi hutumia minced meat (nyama ya kusaga) thnx to Madame B.
Btw izo nyembamba ndio zinaitwaje nikatafute au ziko kwenye package ya aina gani??!
 
Last edited by a moderator:

King'asti

JF-Expert Member
Nov 26, 2009
27,739
2,000
Hahahah King'asti kama unanionaga vile. Ila mi hutumia minced meat (nyama ya kusaga) thnx to Madame B.
Btw izo nyembamba ndo zinaitwaje nkatafute au ziko kwenye package ya aina gani??!
Bwana weeh, mie nazitumia ila nasahau jina kila siku! Nikiagiza nasema zile tambi nyembambaaaaaaaaaa, naeleweka hehehe. Inakuwa kama a bag of cookies, nikumbushe nikichungulia jikoni nikupe jina kamili. Pakiti imeandikwa kiarabu na ina green background na white letters sehemu ya kati.

Nyama ya kusaga haifai wavivu, manake mie hupenda kuikausha kwanza ikiwa na spices, kisha kuunga pembeni ndo nichanganyie na tambi zilizochemshwa.
 
Aaaaaaaaaaaaaaah kama nshaionaga supermarket...ntaenda kuzunguka uko nione kama ni iyo. Ukiniwahi unipe jina. Af unakumbuka uliniahidi utakujaga kunipikia one day...am ctil waiting.
 
Fadhili Paulo

Verified Member
Sep 1, 2011
3,227
1,195
Wadau wa jukwaa hili naombeni utaalamu wenu kuntu, hatua kwa hatua ya namna bora ya kupika tambi zikawa hazikatiki katiki wala kushikamana kama wali
zikawa nzuri na wakat wa kula unaweza kuifyonza tambi moja mwanzo mwisho kama tuonavyo kwenye matangazo
Natanguliza shukrani
Okay, Benvenuto! (karibu, kiitaliano). Nitakufundisha mimi, twisheni pia ipo.

Ni hivi; Tambi ama Spaghetti kwa kiingereza, ni aina mojawapo ya vyakula vitokanavyo na ngano kundi la Pasta. Hivyo pasta zipo nyingi ikiwemo tambi zenyewe/Spaghetti, zingine ni fusil, penne, ravioli, tagliatelle, macharonne na nyingine nyingi tofauti tofauti zaidi ya mia moja.

Zipo pia pasta maalumu kwa ajili ya supu tu, kwa kawaida huwa ni ndogondogo wakati mwingine karibia na mchele. Pasta zote zikiwemo tambi au spaghetti zinaweza kuwa ni kavu (zile zilizopo dukani) ambazo mara nyingi hutengenezwa viwandani na pia zinaweza kuwa fresh (yaani unatengeneza mwenyewe na kuzipika papo hapo), karibu aina zote za pasta zinaweza kuandaliwa na kupikwa zikiwa fresh. Hata tambi zipo fresh, Mi kwa ujumla hupendelea pasta fresh kwa sababu zinaradha ya aina yake nzuri tofauti na zile za dukani. Kama hujawahi hili unaweza usinielewe.

Tambi au pasta karibu zote zinaweza kuwa za rangi pia, unaweza kutengeneza za blue, za kijani, nyekundu, za brown na kadharika na kadharika. Mhimu ni utumie natural coloring agents (usitumie rangi za viwandani sababu zina kemikali, ni tetesi lakini). Kama unataka za kijani kwa mfano, wakati unaandaa unga wa ngano tayari kwa kukandwa kuandaliwa kuwa pasta, ongeza kiasi kidogo cha mchicha uliochemshwa kidogo na kusagwa unga baada ya kuchujwa maji. Mwisho utapata pasta au tambi za rangi ya kijani.

Nimesema twisheni ipo, sasa nisije sababisha usirequest twisheni bure...........

Namna ya Kuchemsha tambi:
Bado kuna mkanganyiko wa juu ni wapi tambi au chakula jamii ya pasta kiligunduliwa kwa mara ya kwanza, baadhi ya wanataaluma wanadai ni China ndiko pasta ziligunduliwa na wengine wanadai ni Italia ndiko ziligunduliwa. Bali inajulikana kote duniani kuwa ukienda nchi yeyote ukakuta mgahwa au hotel ya kiitalia (Italian hotel/restaurants), usipokuta tambi au pasta, basi hapo siyo penyewe!.

Kwa mjibu wa kitabu cha Paolo Urbani alichoshirikiana na Silvano Rodato kiitwacho Laboratorio di Cucina ukurasa wa 190:

 • Tambi au pasta hupikwa katika maji mengi ya kutosha yaliyochemka kufikia nyuzi joto 100, yaani yamechemka.
 • Uwiano ni maji lita 10 kwa kila kilo 1 ya pasta/tambi.
 • Kamwe usijejaribu kuongeza maji ya baribi ndani ya maji hayo ya moto yanayoendelea kuchemka ya tambi au kuzinyunyiza tambi/pasta maji ya baridi baada ya kuzichuja toka maji moto kwa madai kuzisimamisha zisiendele kuiva.
 • Pasta/tambi ni chakula kinachopikwa na kuandaliwa katika hali ya haraka na kutokusimama kushangaa chochote, unapotumbukiza tambi unatakiwa ujihakikishie kuwa huna kazi nyingine itakayokufanya upunguze moto au umsubiri fulani, inatakiwa unaona wote wamekaa mezani ndo unatumbukiza tambi kwenye maji. Mara nyingi waitaliano wengi wanapokuwa njiani kurudi majumbani mwao wanapokaribia na kukunja kona ya mwisho kuingia mtaani kwao huwapigia simu waume au wake zao watumbukize tambi/pasta kwenye maji (buta la pasta!).
 • Mhimu kuliko yote ni kuwa hadi mwishoni mwa kuchemka na hadi kuungwa kwa pasta zako, ni lazima uhakikishe zinabaki bado ni ngumungumu kidogo yaani zinasikika katika meno, kama ni wali unasema bado una kiini (al dente!).

Okay hatua za kuchemsha tambi;
Mahitaji:

 • Tambi kilo 1
 • Maji yaliyochemka lita 10
 • Chumvi ya jikoni gramu 100
 • Mafuta ya kupika (vizuri kama unapata ya zeituni) robo kikombe
MHIMU SANA: Tafadhari tambi haziongezwi sukari kwa sababu yeyote ile.

Namna ya kupika:

 • Tumbukiza tambi zako kwenye maji yaliyochemka vya kutosha yenye chumvi na mafuta ya kupikia. MHIMU, USIZIVUNJE HATA MARA 1 TAMBI IWE KABLA AU UNAPOCHEMSHA!!!, tambi zichemshwe kwa urefu wake wa asili, hii ndiyo sababu uma (fork) ndio hutumika kulia tambi na siyo kijiko wala mkono!!!, unachomeka uma, unazungusha kupata kifundo cha tambi utakazoweza kuzimeza, unatumbukiza mdomoni.
 • Unatakiwa kuzikoroga mara kwa mara kwa kutumia uma mkubwa mrefu, iweleke ninaposema mara kwa mara haina mana basi mtu ashike kiuno na asimame hapo akikoroga tambi kama anakoroga uji wa ugali, unakoroga dakika 2 au 3 unapumzika kisha unarudia tena.
 • Unatakiwa kuzionja moja moja kila mara ili kuvizia zinapoanza kukaribia kuiva uzitoe haraka, usipofanya hivyo lazima utapoteza point, pale unapotaka kujuwa kama tayari zimeiva kumbe ziliiva kitambo kwa sababu we ulikuwa huonjihuonji kabla ili kuzivizia.
 • Kisha kukaribia kuiva tambi huchujwa toka katika maji na kuziunganisha na sauce (sosi) ambayo umeamua kuitumia kuungia tambi zako siku hiyo. Kwa kawaida sosi huandaliwa kabla ya kuchemsha pasta, au huku unaandaa sosi huku maji ya tambi yanachemka. Zipo Sosi (pasta sauce) zaidi ya 100, kila sosi ina jina lake na mahitaji yake maalumu, kadri unavyobadilisha aina ya sosi ndivyo na jina la tambi au pasta uliyopika linavyobadilika. Kwa uchache kuna sosi ya nyanya (tomato sauce), sosi nyeupe (white sauce, hii maziwa hutumia zaidi), sosi ya nyama ya kusaga (bolognaise sauce/minced meat sauce), Fish ragu', amatriciana, alla romana. alio-olio-peperoncino, na kadharika na kadharika.
 • Mifuko mingi ya pasta/tambi huandikwa kabisa dakika za kuchemshwa ubavuni mwake tangu kiwandani.

Nikuchagulie pishi moja la tambi litakalokuduwaza?
 
Mentor

JF-Expert Member
Oct 14, 2008
20,357
2,000
Kha..umesoma mahali ukatafsiri ama wajua kweli??! U av amazed me kwakweli kwa upembuzi wako yakinifu..yan mtu haulizi swali.

We King'asti unaniletea pozi eti nitangoja milele wala ctaki unachek mshkaji anavojua pishi ilo?? Dah...

Babu Asprin fanya hima uwalete wake zako cacico, BADILI TABIA, Yummy, et al 'TUISHIENI'.

Mai waifu Catherine uko wapi uje huku...
Binti yetu mpendwa Eversmilin Gal njoo na ww utapoolewa usijeachika...

NB: kwann sisi tumezoea kuvunja spaghetti??!
 
Last edited by a moderator:

Paul S.S

Verified Member
Aug 27, 2009
6,084
2,000
Okay, Benvenuto! (karibu, kiitaliano). Nitakufundisha mimi, twisheni pia ipo...............................

Nikuchagulie pishi moja la tambi litakalokuduwaza?
Dah fadhili paulo unatisha, nashukuru kwa udadafuzi wako wenye weledi wa kutosha
kwenye red nasubiri kwa hamu...........
 
Last edited by a moderator:

Bibi yaga

Member
Aug 5, 2012
31
95
Tambi
Mahitaji:
1. Kitunguu kikubwa kimoja
2. Nyanya mbili kubwa
3. Karoti kubwa moja.
4. Pilipili Hoho Nusu
5. Tambi gram 250
6. Mafuta ya kupikia
7. Chumvi
8. Nyama ya kusaga 1/4 Kg
9. Tangawizi
10. Limao
11. Kitunguu swaumu

Matayarisho
1. Weka sufuria jikoni, weka mafuta na ukaange vitunguu maji vikifatiwa na vitunguu swaumu
2. Baada ya hapo, chukua nyama yako ya kusaga na uitie kwenye sufuria yenye vitunguu vyote.
3. Kisha tia tangawizi kwenye nyama huku unaendelea kuikaanga, baadae tia nyanya, hoho na karoti
4. Ipua na uweke pembeni
5. Chukua sufuria nyingine, weka maji na uibandike jikoni mpaka maji yachemke
6. Maji yakisha chemka, weka chumvi kiasi na uzitie tambi zako
7. Ukiona zimelainika kiasi, yachuje maji yoote na tambi zibaki kavu.
8. Chukua ule mchanganyiko wako wa viungo na tia tambi zako na uziache jikoni kwa dakika 5 hivi..
9. Hapo zitakuwa tayari kwa kuliwa...
 
Asprin

JF-Expert Member
Mar 8, 2008
61,614
2,000
Kha..umesoma mahali ukatafsiri ama wajua kweli??! U av amazed me kwakweli kwa upembuzi wako yakinifu..yan mtu haulizi swali.
We King'asti unaniletea pozi eti nitangoja milele wala ctaki unachek mshkaji anavojua pishi ilo?? Dah...
Babu Asprin fanya hima uwalete wake zako cacico, BADILI TABIA, Yummy, et al 'TUISHIENI'.
Mai waifu Catherine uko wapi uje huku...
Binti yetu mpendwa Eversmilin Gal njoo na ww utapoolewa usijeachika...
NB: kwann sisi tumezoea kuvunja spaghetti??!
Mi nshazoea kupikiwa bana, sina haja ya kujifunza.

Damn! Hivi leo jumangapi? Nafa mie....
 
King'asti

JF-Expert Member
Nov 26, 2009
27,739
2,000
Mentor, unachonga tu mdomo hapa una sefuria ya kuchemsha tambi bila kuvunja wewe? Unalo, utakoma!

BADILI TABIA, sina hakika kama ndo jina hilo. Ila ni tamu balaa, mie pia mwanzo nilikuwa nakosea kupika. Muhimu ni ku-balance maji, wawe kidogo kama ya kupikia ubwabwa. Ukiweza kubalance usiongezee tena juu (japo ya moto) inakuwa vema zaidi.
 
Last edited by a moderator:

Mentor

JF-Expert Member
Oct 14, 2008
20,357
2,000
Mi nshazoea kupikiwa bana, sina haja ya kujifunza.

Damn! Hivi leo jumangapi? Nafa mie....
Ila wakezo nna uhakika hawana utaalamu huu!!!!
Leo ni...siku moja baada ya utatu..sor moja baada ya wikienda!!!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom