Jinsi ya kuondoa umaskini tanzania .nini kifanyike?naomba maoni yenu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jinsi ya kuondoa umaskini tanzania .nini kifanyike?naomba maoni yenu

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by houseboy, Sep 21, 2009.

 1. h

  houseboy Member

  #1
  Sep 21, 2009
  Joined: Jul 22, 2007
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tumekua tukishuudia jinsi umaskini unavyoizamisha Tanzania,asilimia 85%ya waTanzania wanaishi chini ya maisha ya umasikini mkubwa,uku baadhi ya viongozi na wafanyakazi wa umma wakiikwangua na kujikandamizia utajiri wa hali ya juu.viongozi wengi na wafanyakazi wa umma wengi wanachangia 100% kulididimiza taifa kwa wizi,ruswa,kubebana nk.kwa mtazamo wangu,inabidi sasa tuwe makini sana na tukifanya mchezo Bongo katika miaka 10 ijayo itakuwa imefirisika kabisa.nomba maoni yenu jinsi gani ya kulikwamua taifa letu kutoka tulipo sasa na kupigaga maendeleo,naomba watu wasifanye mchezo kwani nitachapisha maoni mazuri na kuyapeleka kwa wausika.
  Kitu cha kwanza kwa maoni yangu nadhani tuanze na kupunguza ukubwa wa serikali,kwani tuna wizara nyingi sana na watu wanaofanya kazi kwenye wizara wanatumia mamilioni ya pesa nyinyi sana bila kuzalisha chochote kile,mimi naona kuwe na wizara 7 tu aya nimaoni yangu naomba tusifanye hii kuwa ndio ajenda ,nipe mawazo yako ili tuifanye bongo iwe mfano katika Africa tuna kila kitu na sababu ya kuwa taifa tajiri duniani,au tumetupiwa voodu nini?asanteni naomba maononi yenu .asanteni na karibuni
   
 2. MwalimuZawadi

  MwalimuZawadi JF-Expert Member

  #2
  Sep 21, 2009
  Joined: Sep 1, 2007
  Messages: 643
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Houseboy
  Muulize Kikwete maana 2005 alisema anajua matatizo ya Watanzania ingawa alipopanda ndege kwenda Ufaransa alisahau akasema hata yeye hajui kwanini Tanzania ni nchi maskini. Kwa kuwa tunaelekea 2010 labda sasa anajua
   
 3. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #3
  Sep 21, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Umaskini wa Watanzania unaanzia na umaskini wa mawazo..ngazi zote na wakati mwingine umaskini wa roho.Mungu kajalia TZ kila kitu cha kuifanya nchi inyanyuke kwa spidi ya roketi lakini bado hakuna hata dalili.Baada ya Azimio la Arusha, Sera zililenga kuweka njia kuu za uchumi kwa serikali..lakini serikali ni nani? Ni watu..watu hao hawakuwa na nia ya kweli ya kulifanya taifa lifaidike na rasilimali.Kuhodhi bila kuzifanyia kazi zilete manufaa ni sawa na kuwa bila kitu.

  Hapo hapo wajanja wachache wakachukulia "ujinga" wa Watz walio wengi kujinufaisha huku wakiwakaririsha watz kuwa kila kitu ni mali ya umma!Mali ya umma isiyokuwa na mwenyewe?Hulka ya umimi inayoendelea kujengeka hasa kwa wale wenye dhamana ya mali ya umma, nafasi na fursa zaidi ya wengine isipoangaliwa na kudhibitiwa basi tujiandae kuwa na taifa fukara lisiloweza kujikwamua tena kutoka katika rindi la umaskini uliokithiri.Rasilimali nazo zinaenda zikiisha ( depleted) wakati hatujaweza kujiwekea miundombinu sahihi ya kuleta maendelea kwa watanzania wali wengi.
  Tutaweza kuwa na maendeleo kama atatokea kiongozi radical mwenye nia ya kweli ya kupambana na ufisadi, asiyekuwa na umimi, aliye tayari kuwabadilikia hata maswahiba ili kuondoa vizingiti vyote vinavyofanya mapinduzi ya kiuchumi yasiwezekane.Hapo ndipo pa kuanzia.Pili ni kuhakikisha kuwa waliokaa kwenye gari ni abiria sahihi, vinginevyo inabidi kuwashusha wale wasiostahili! This is the only way to move from good to great!
   
 4. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #4
  Sep 21, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,601
  Likes Received: 82,171
  Trophy Points: 280
  Ulichoandika hapo juu ndiyo ukweli halisi wa nchi yetu. Ahsante sana kwa mawazo yako mazuri na yaliyotulia.
   
 5. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #5
  Sep 21, 2009
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,305
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Mimi nadhani kikubwa ni kuwa na serikali inayowajibika tu. Hili litafanikiwa pale kila mwananchi atakapotumia nafasi yake kuwajibika sawia pale alipo. Hii pia ihusishe kuishinikiza serikali isiyotaka kuwajibika ikiwa ni pamoja na kujenga mfumo shirikishi na usioegemea kikundi cha watu wachache wenye masilahi binafsi. Kuishikiza serikali kujenga mfumo sawa mbele ya sheria, na kuwapunguzia watu/tasisi (mfano rais) madaraka makubwa ambayo yanamfanya aendeshe nchi kama mradi wake na wapendwa wake. Hili likifanikiwa, hatuna sababu ya kutoendelea kwani rasilimali zote zitatumika kwa maslahi ya watanzania, ikiwa ni pamoja na kutoa fursa kwa wale wenye uwezo na wala sio kwa kigezo cha huyu kuwa mwenzetu.
   
 6. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #6
  Sep 21, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  I think we need visionary leaders, na sio wanao kwenda kufungua mafail tu.

  A leader must have a vision,
   
 7. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #7
  Sep 21, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Having a vision without action is a nightmare!
  Nadhani kila kiongozi anayeingia madarakani atasema anayo vision....na ndio maana yuko madarakani.Aliuza sera kwa wananchi wakavutika na ndio maana wakampa dhamana.
  What is lacking is actualising the vision through actions directed towards attaining the vision.Perhaps a steer with the buy-in of those he chooses to help him to realise goals.
   
 8. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #8
  Sep 21, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Hizo vision za CCM za kuandikiwa sidhani kama ni vision bali ni ndoto tu walizo nazo. A man with a vision, first, he will tell us his vision; second, he will give us the way how he will execute hiyo vision, na sio kusema tu ataleta kazi milioni moja, bila ya kutuambia ni kivipi atazitengenza hizo kazi na zitawagusa wananchi kivipi?

  Now, enforcing his vision hilo nalo ni jambo lingine ambalo viongozi wengi hawana, kwasababu hizo position wamepewa na watu, hivyo basi wapo tayari kucompromise na hao walio wapa, ulaji. When you enforce your vision, kumbuka kuwa wengi watakuona mbaya, lakini, mwishoni watu wataelewa kuwa ni kwa manufaa ya nchi.
   
  Last edited: Sep 21, 2009
 9. Ramthods

  Ramthods JF-Expert Member

  #9
  Sep 24, 2009
  Joined: Jun 2, 2009
  Messages: 494
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Mengi yaliyosemwa kwenye thread hii ni ya kweli. Hata hivyo naona kuna jambo moja halijaangaliwa kiundani - ELIMU

  85% ya wantanzania ni masikini, lakini utakumbuka kuwa 1% ya wanafunzi wanaomaliza darasa la 7 ndio wanaopata nafasi ya kuendelea na elimu ya juu (university education).

  Maendeleo ya taifa hayawezi kufanywa na mtu mmoja, bali taifa kwa ujumla. Watu wakielimika, wataweza kutofautisha kati ya kiongozi mzuri na mbaya - kama leo hii wewe uliyeelimika unavyoweza kuona ubaya wa SISIEM au chama kingine chochote hapa Tanzania.

  Pia kumbuka, KURA ya MJINGA na ya ALIYEELIMIKA zote zina uzito sawa. Usipomwelimisha mwenzako leo, kura yake kesho itakugharimu na wewe pia!
   
Loading...