Jinsi ya kuomba zuio la Mahakama (temporary injunction) kuzuia mali yenye mgogoro isiharibiwe, kuuzwa au kupotea

Apr 26, 2022
70
104
Je unaweza kuomba temporary injunction/ stop order (zuio) wakati kesi iko kwenye hatua ya rufaa?

Kwa mujibu wa Sheria ya Mwenendo wa Kesi za Madai (Civil Procedure Code/ CPC) unaweza kuomba zuio la muda mfupi Mahakamani ikiwa utaona mali inayobishaniwa kwenye kesi iko hatarini kupotea au kuharibiwa na upande wa pili kwenye kesi au iko hatarini kuuzwa na hivyo kuharibu hatima ya kesi. Soma Order XXXVII Rule 1 ya CPC.

Sasa, mojawapo ya masharti ya kuomba zuio la muda mfupi (temporary injunction) chini ya sheria ya Mwenendo wa Kesi za Madai (CPC) lazima kuwepo na kesi (suit) Mahakamani. Swali ni je rufaa pia ni kesi (is an appeal a suit?).

Inawezekana wakati mnaanza kesi hapakua na usumbufu wa mtu kutaka kuharibu au kuficha au kuuza mali ambayo ndiyo kiini cha kesi, hivyo haukuomba temporary injunction. Lakini uamuzi ulipotoka hujaridhika ukakata rufaa, ghafla upande wa pili anaanza visa, je utafanyaje kwenye hiyo hatua?

Mahakama Kuu inatoa majibu kwenye kesi ya MOHAMED AHMAD MBARAK Vs HILAL AHMAD MBARAK, MISC. LAND APPLICATION NO. 290 OF 2022. Kwenye hii kesi, Mahakama Kuu ya Tanzania ilitamka kwamba, hata rufaa inaingia kwenye maana ya kesi. Hivyo (kwa mujibu wa hii kesi) unaweza kuomba temporary injunction/ stop order hata wakati kesi iko kwenye hatua ya rufaa.

(Nimeweka screenshot hapo chini kesi nzima ipo Tanzlii).

Screenshot_20240516_153613_Drive.jpg
 
View attachment 2991704
Yah hii Iko pouw.
 
Back
Top Bottom