Jinsi ya kumvuta Mwanamke kupitia Mawasiliano

Kasomi

JF-Expert Member
Sep 3, 2014
11,036
20,338
JINSI YA KUMVUTIA MWANAMKE KUPITIA MAWASILIANO.

Kisaikolojia wanaume hutumia direct communication ndomana mazungumzo ya men to men huwa short and clear.

Men 1: "Oya niletee ile movie"
Men 2: "Baridi mzee baba"...
Story inaishia hapo.

While women was designed to keep conversation going, wao hutumia indirect communication.
Ndomana ni rahisi mwanamke kuongea na simu na mwanamke mwenzie or mwanaume yeyote yule hata lisaa.

Kikao cha wanawake huchukua muda mrefu kuliko cha wanaume.
Kikao cha wanawake huwa na kelele nyingi kuliko cha wanaume, sababu kila mmoja hupenda kuongea.

Ndomana umerudi kazini umechoka, lakini mkeo hawezi kukupa nafasi ya kupumzika kwa amani. Lazima atakuja na kukuuliza viswali swali, kukuhadithia hiki na kile.
Sio kosa lao, ndivyo wao walivyoumbwa.

Inshu iko hapa, kosa kubwa analofanya mwanaume ni pale anapotumia direct communication akiwa anaongea na mwanamke.

Mwanamke huhisi aidha una dharau, or unaboa.
Imagine, anakutumia ujumbe mrefu wa mapenzi, then unamjibu "Ok".
Lazima akuone unadharau.

Imagine unachat na mwanamke kwa mara yako ya kwanza, then unamtext short short hujui kuendeleza mada.
Or unampigia simu, huna la kusema unaishia "Nilikuwa nakusalimia tu" then unakata simu.

Automatically atakuona unaboa, na hatakuwa tena na mood ya kuwasiliana na wewe.
Ndo hapo mwanzo wa kuignore text na call zako.

Infact, mwanamke huvutiwa na mwanaume ambae anajua kumudu mazungumzo. Anaejua kuzalisha mada, anaependa kumsikiliza kwa umakini na kuheshimu mawazo yake.
Mwanaume anaemfanya ajisikie huru kumwambia kuhusu lolote lile, linalomuumiza, linalomfurahisha, linalomkera, na wakajadiliana vizuri.

Here's a thing,
Ukiwa unaongea na mwanamke, tumia indirect communication.
Formula zake ziko mbili, na ni simple tu
1: Answer + Statement(Jibu + Maelezo).
Mfano:
Yeye: "Hi hubby 😘, uko poa?"

Wewe: "Hi honey, Alhamdulillah niko poa hadi najionea wivu 😉😊.
Kukumiss tu mrembo wangu 👸".

2: Answer + Statement + Question(Jibu + Maelezo + Swali).
Mfano:
Yeye: "Kivuruge wangu 😍, mbona umenisusa?"

Wewe: "Sijakususa chafujo wangu, nilikuwa kijijini kule network mbovu sana 😢.
Halafu nimekumbuka, nimepata Money Heist S3. Vipi utakuja ghetto kuchukua? 🤔"

#Mh hivi huyo dada akienda huko ghetto atatoka mzima kweli? 🤔🤔🙄
Hebu tuache umbea, tuendelee na mada yetu 😂😂😂😁😁****

Mwanamke ni kiumbe ambae ili akupende, akuone una umuhimu mkubwa kwake, akuthamini, akuheshimu, basi anahitaji kwanza afeel emotionally attached to you (awe na hisia na wewe).

Kuwe na chemistry kati yenu, ajihisi huru mbele zako, ajihisi mwenye furaha na raha akiwa na wewe.

Na hili linawezekana kama utazingatia suala la kudumisha mawasiliano kati yenu.
1: Penda kumpa muda wako.

2: Penda kumsikiliza anachotaka kuzungumza hata kama mada zake zinakuboa or hata kama umerudi home umechoka.

3: Kuwa mwepesi wa kuendeleza mazungumzo na kunogesha kwa vituko, mada zenye hisia, na zenye huzuni pia sometimes.

4: Kuwa ndo mtu pekee anaemsikiliza na kumshauri pindi anapitia magumu, maumivu, nakadhalika.

Haya yote yatawezekana kama utaacha kuongea na mwanamke kama unavyoongea na mwanaume mwenzio.

Na pia kumbuka tu, ukishindwa kufanya haya kwa mwanamke umpendae, basi usiombee mwanaume mwengine amfanyie. Utaibiwa huku unajiona.

Epuka sana kumfanya mkeo/girlfriend wako ajihisi mpweke wakati upo nae, ajihisi hana wa kushare nae mambo yake wakati wewe upo.
Ni kosa kubwa sana.

NB: Mawasiliano yanayozungumziwa hapa ni ya ana kwa ana, chatting, na kupigiana simu. Yeyote yale yatumie ipasavyo kutengeneza strong connection kati yenu.
 
Acha ujinga, atakuvutia akiona hii meseji

Transaction ID: 811968522. You've received 200,000 TSH from Drone Drake, phone number 255713927734 in Tigo, time 2021/06/05 08:53:38. New balance is 200,001 TSH. Thank you!
Time: 21/06/2021 11:36:47
 
Back
Top Bottom