Cybercurex
Member
- Jan 19, 2023
- 98
- 238
Njia mojawapo ya kukabiliana na maumivu yanayokutesa ni kukubaliana na hali halisi.Kubali ulimpenda ila yeye Hajakupenda sawa na ulivyompenda.Kubali umeachwa,kubali hupendwi Usipokubali kuwa umeachwa utajikuta umewekeza nguvu zako nyingi katika kujenga mahusiano yanayokuumiza kila kukicha. Jipe muda kwa ajili ya kuondoa uchungu na maumivu moyoni.
Pale unapohisi kulia au kuhuzunika fanya hivyo kwasababu itaondoa hasira na chuki za maumivu ndani yako. Jifunze kuwa bize kwa kufanya kazi kwa bidii hatua hii itakupunguzia muuda wa kumfikiria yule aliyekuuumiza.kumbuka Maumivu yako hataisha kama hautakuwa na kitu cha kukipa muda au kitu kitakachochukua umakini wako.
Msamehe mtu huyo kwa kuvunja moyo katika mahusiano,lakini usjaribu au kufikiri kumpa nafasi ya kumwamini tena.Jifunze kumwepuka kadri uwezavyo Ondoa karibu yako vitu vyote vinavyowezekana vya mtu huyo ulivyonavyo,mfano zawadi alizowahi kukupatia au kumbukumbu za matukio ya picha zote ulizowahi kupiga nae,Kuna msemo unasema Ukitaka kuzika yaliyopita basi hakikisha hakuna anayejua kaburi.
Tengeneza wakati wako wa furaha,jitengeneze kumbukumbu nzuri kwa kutumia muda wako mwingi na marafiki zako au watu wanaokuthamini.Furaha yako ya kweli inatoka ndani yako,haitokani na mtu.Kamwe usiruhu kuondoka kwa mtu katika Maisha yako kukusababishie ujipoteze mwenyewe. Shukuru kwa yote yaliyopita hata kama yamekuuumiza kiasi gani,Amini hakuwa chaguo lako.
Unaweza kuanza upya na unaweza kuishi maisha yako bila yeye.Si kila anayekuja katika maisha yako atakuwa sehemu yako. Kuna yule atakayekuja kwenye maisha yako kukupa somo litakalokuonesha udhaifu wako,ujifunze na somo hilo ili uwe imara wakati ujao.