Jinsi ya kumlinda mumeo

Ni pale mwanaume alipoona kashindwa wajibu wake na kuamua kumtwisha mwanamke majukumu yake[emoji134] [emoji134]
 
Natumaini wenye akili watapima kati ya mleta mada na wewe mchangiaji nani mwenye akili, hekima, maharifa na busara.
 
Hata hivyo wanawake ndio chanzo cha wanaume kuchepuka, hasa pale mnapomkubalia mwanaume huku mkijua anamwibia mwanamke mwenzenu huko nyumbani kwake, na wengine mnafikia kuweka mitego ya kiganga na pia kujiuza mabarabarani.

Kwanini nyie wanawake mliofanikiwa msiwainue wanawake wenzenu wanaotegemea kipato chao kutokana na mifuko ya wanaume?!
 
Kiafrika kuna kuoa na kuolewa, ni kizunguni tu ndio kuna kuoana.
Mtoa mada amewalenga wa afrika.
 
wewe utakuwa mzungu 😀 Wabongo wa hivi wapo kweli?

Hata Mimi nimemshangaa huyu anavyopinga hizo hoja ...

Hawa ni walewale wa haki sawa. Anamaanisha wanaume nao wapike, wadeki, wasafishe vyombo na mambo mengine Kama hayo. Mbona hazungumzii yale yasiyowezekana Kama vile kumnyonyesha Mtoto au kubeba mimba na kujifungua kabisa? Dhana ya division of labor ilikuwa nzuri sana ... Sema kutokana na sababu mbalimbali ambazo ni PAMOJA na ugumu wa maisha, mahubiri juu ya haki sawa hasa pale elimu ya kizungu ilipoingia na uhimizaji wa kumuelimisha Mtoto wa like sawa na wa kiume ndipo mambo yalianza kubadilika ... Mdada amesoma hawezi tena kuwa mama wa familia maana nae anataka aajiriwe aingize kipato ... Ile kampeni ya mwanamke akiwezeshwa anaweza nayo ikaleta promotion kubwa mno ... Mwanamke akaanza kupata nguvu ya kifedha ... Baadhi wakaona kuwa maisha yanawezekana bila kumtegemea mwanaume ... Basi dharau, utovu mwingi wa nidhamu kwenye Jamii ukaanza kwani mwanamke kuwa na Hela kulianza kuonekana ni muhimu . Ndipo wengine wakatamani kuwa na Pesa Kama wenye kazi au biashara zao na baadhi ya wanaume wakaanza kutoa hongo Hata kwa wale wenye ndoa zao wakajikuta wanadharau waume zao ... Sitaki kuendelea ...

Lakini chimbuko la yote haya ni kuukanyaga utamaduni wetu na kuiga uleee ... Na twaendelea kuiga mpaka yasiyofaa. Utamaduni haubadilishwi kwa nguvu, na Kama ukifanikiwa kuubadilisha basi hayo mabadiliko yataambatana na madhara makubwa mno. Hayo ndiyo tunayoyaona katika hizi enzi za wanawake wa kibantu kutaka kuishi na waume wao Kama waishivyo wale wa kizungu!

Kina dada badilikeni; bebeni NAFASI zenu Kama wake na si kujibebesha mivichwa isiyo yenu: mwanamke anayekubali uanawake wake hufurahia Matunda ya ndoa yake na huheshimiwa na mumewe na Jamii nzima kwa ujumla. Yule ajifanyaye sawa au zaidi ya mumewe huiangamiza ndoa yake kwa mikono yake mwenyewe ....
 
Wewe mwenye commitment na mkeo kwa nini usikitulize nyumbani kwako na mkeo? Wewe huna huruma na mkeo, huo mchepuko utaanzaje kumuonea huruma mkeo? Acheni kujifanya victims ebooooo
 
Haya usemayo ni kweli kabisa, lakini palipo utulivu ndoa huwa inadumu hata mwanaume akichepuka nafsi inamsuta na chanzo cha utulivu ni mke mwema.
 
Wewe mwenye commitment na mkeo kwa nini usikitulize nyumbani kwako na mkeo? Wewe huna huruma na mkeo, huo mchepuko utaanzaje kumuonea huruma mkeo? Acheni kujifanya victims ebooooo
Wanawake muweni na huruma wenyewe kwa wenyewe, iweje unayejua hasa maumivu ya mume ukubali kumpokea mwanaume wa mwenzio na kumpa hifadhi?!

Unajua wanawake mkitia ngumu kwa wanaume walio na wake zao hakutakuwa tena na mchepuko??
 
Wanawake muweni na huruma wenyewe kwa wenyewe, iweje unayejua hasa maumivu ya mume ukubali kumpokea mwanaume wa mwenzio na kumpa hifadhi?!

Unajua wanawake mkitia ngumu kwa wanaume walio na wake zao hakutakuwa tena na mchepuko??
Hata nyie mkitia ngumu, mkaheshimu ndoa zenu na viapo vyenu, wanawake wa nje wataingilia mlango gani? Muwe wanaume kweli, muwe responsible na matendo yenu, sio kujifanya watoto wadogo wasiojua walifanyalo
 
Wanawake muweni na huruma wenyewe kwa wenyewe, iweje unayejua hasa maumivu ya mume ukubali kumpokea mwanaume wa mwenzio na kumpa hifadhi?!

Unajua wanawake mkitia ngumu kwa wanaume walio na wake zao hakutakuwa tena na mchepuko??
Huyo mchepuko wako ni mke wa mtu? Maana umesema anajua uchungu wa mume!! Sasa kwani huyo mchepuko wako ndio aliweka ahadi na nadhiri mbele ya Mungu na wanadamu kuwa hatochepuka?? Kwanini kila upuuzi wenu mnataka wanawake ndio wabebe lawama nanyi muwe victims!!!

Wich dau.
 
[emoji122] [emoji122] maoni mazuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…