Hata Mimi nimemshangaa huyu anavyopinga hizo hoja ...
Hawa ni walewale wa haki sawa. Anamaanisha wanaume nao wapike, wadeki, wasafishe vyombo na mambo mengine Kama hayo. Mbona hazungumzii yale yasiyowezekana Kama vile kumnyonyesha Mtoto au kubeba mimba na kujifungua kabisa? Dhana ya division of labor ilikuwa nzuri sana ... Sema kutokana na sababu mbalimbali ambazo ni PAMOJA na ugumu wa maisha, mahubiri juu ya haki sawa hasa pale elimu ya kizungu ilipoingia na uhimizaji wa kumuelimisha Mtoto wa like sawa na wa kiume ndipo mambo yalianza kubadilika ... Mdada amesoma hawezi tena kuwa mama wa familia maana nae anataka aajiriwe aingize kipato ... Ile kampeni ya mwanamke akiwezeshwa anaweza nayo ikaleta promotion kubwa mno ... Mwanamke akaanza kupata nguvu ya kifedha ... Baadhi wakaona kuwa maisha yanawezekana bila kumtegemea mwanaume ... Basi dharau, utovu mwingi wa nidhamu kwenye Jamii ukaanza kwani mwanamke kuwa na Hela kulianza kuonekana ni muhimu . Ndipo wengine wakatamani kuwa na Pesa Kama wenye kazi au biashara zao na baadhi ya wanaume wakaanza kutoa hongo Hata kwa wale wenye ndoa zao wakajikuta wanadharau waume zao ... Sitaki kuendelea ...
Lakini chimbuko la yote haya ni kuukanyaga utamaduni wetu na kuiga uleee ... Na twaendelea kuiga mpaka yasiyofaa. Utamaduni haubadilishwi kwa nguvu, na Kama ukifanikiwa kuubadilisha basi hayo mabadiliko yataambatana na madhara makubwa mno. Hayo ndiyo tunayoyaona katika hizi enzi za wanawake wa kibantu kutaka kuishi na waume wao Kama waishivyo wale wa kizungu!
Kina dada badilikeni; bebeni NAFASI zenu Kama wake na si kujibebesha mivichwa isiyo yenu: mwanamke anayekubali uanawake wake hufurahia Matunda ya ndoa yake na huheshimiwa na mumewe na Jamii nzima kwa ujumla. Yule ajifanyaye sawa au zaidi ya mumewe huiangamiza ndoa yake kwa mikono yake mwenyewe ....
asubuhi asubuhi kukuta MTU wa hivi kaku Quote ni kuharibiana siku ujue.
kwa taarifa tu Mimi nimevutiwa sana na huyo member.
ndio kaongelea kufanya kazi za nyumbani na si kunyonyesha kwa sababu wewe kuwa mwanaume hakukuzuii kufanya kazi za nyumbani, ni UVIVU TU.
na unataka kuniambia mwanamke kujiweza kiuchumi ni jambo baya??
mnataka mwanamke mnyonge atakayeishi matesoni kwa sababu hana uwezo wa kujitegemea?? unataka turudi kwenye kurithishana wake? hutaki mwanamke naye amiliki mali na a Control maisha yake?
kwanza Leo hii una uwezo kweli wa kulea mke na watoto na mshahara wako peke yako? au ndo waenda na kidumu shule?
ni roho ya kutawala wenzio tu inakuandama, ushindwe. Badilisha hiyo roho ya utawala iwe ya upendo.
NDIO, mwanamke anaweza kuishi bila mwanaume, UKWELI NDO HUO. Unataka kuturudisha enzi za kung'ang'ania ndoa chungu kisa imani potofu kama hizi?
wala hamna cha kiburi wala dharau. Kwani wanaume kinachowapa sense of POWER ni nini? Anayecontrol uchumi wako ndo anaControl maisha yako!!
Ndo ilivyo MTU akiwa na uwezo wa kuControl uchumi wake. Atakuwa na POWER, STANDARDS, SAY, na FREEDOM, kitu ambacho hujazoea kuona kwa mwanamke sio?
wala mwanamke kufanya kazi hamzuii kuwa mama. kuwa mama kwako ni kupika na kufua kila siku?? Huo sio umama ni uHouse maid. atleast not when the child is of a school age.
ndo Hawa wanaume wanaona jukumu la kulea ni la mwanamke. Not FATHER FIGURES. I need a man who cooks and cleans after his own children.
kushikilia tamaduni sio sifa. kuna watu wanakeketa hadi Leo kwa sababu ya "tamaduni". shika mazuri acha mabaya.
na wala kubadilisha hizi tamaduni hakuleti madhara yoyote. kuna WAVIVU tu wanaofanya makusudi kabisa ili ilete madhara.
Division of labor mpya ya karne hii haina ubaya wowote, ni mbaya kwa WAVIVU na WASIOPENDA WAKE ZAO.
Hiyo lifestyle ya " kizungu" ndo niliyoitaka, INAVUTIA, INAPENDEZA.
kuna wanawake KIBAO bado wanapenda lifestyle ya zamani ya kukaa nyumbani kujipikilisha. me sipendi kazi za nyumbani wala kupika. Don't worry there's a man for everyone lol.