Jinsi ya kumlinda mumeo

Jinsi ya kumlinda mumeo

Mbona huwa sioni mafundisho ya aina hii kwa wanaume? Au ndoa ni ya mwanamke peke yake?
Kwanini mwanamke atumie affort kubwa sana kuilinda ndoa as if ni yake peke yake?

Kwanini muwafanye wanawake wajione watumwa kwa ndoa zao? Hivi yule aloambiwa atumie akili, hiyo akili aitumia wapi?

Na hii mentality inaitafuna jamii kwa kiasi kikubwa sana, kiasi kwamba wanaume wanajiona kumuoa mwanamke ni kumfanyia fadhila tu hivyo apaswa kuhakikisha anabaki humo.
Ndoa ni ya wawili, hizo effort lazima ziwe pande zote, lasivyo ni kutwanga maji kwenye kinu tu.
 
Unazungumzia wanaume wa sayari ipi, hawa watu hata ubinuke hawalindiki yaani kama ni wa kutoka ataenda tuuu, kuna muda huwa nawaza hata maombi ambayo ni silaha kuu yanadunda sijui huwa inakuwaje yaani
Ha ha ha! Laughing loud, pray for your husband, usikate tamaa.
 
Siku mtakapojua jua kuwa hakuna kishawishi wala sababu za kuchepuka ndipo fikra sahihi zitakuwa zimeeleweka.
Fanya zoezi dogo
Tafuta wanaume kumi wanaochepuka kisha waulize kwa nini wanachepuka?
Tafuta watu wa kada/uwezo/elimu/dini tofauti.
Hakuna atayekwambia anachepuka eti kwa kuwa mkewe ni mchafu au hajui kupika.
Hizo ni vijisababu tu ambavyo havina maana.
Kwa masomo yenu haya yasio na maana mmewafanya wanawake wengi waone kuwa iwapo mumewe anachepuka basi wa kulaumiwa ni yeye. Mnawatesa hawa wanawake hata kufikia hatua ya kuwa watumwa kwenye ndoa ili tu kukidhi haja na tamaa za.mwanaume.
Wengine mpaka wanaingiliwa kinyume na maumbile na wanaume wao wa ndoa kwa hofu asipompa hilo tundu basi atachepuka.
Sijui ni aina gani vitabu vya kiroho unavyosoma ikiwa una fikra na mtazamo hafifu kiasi hiki.
Kwani inamgharimu nini mwanaume kufua nguo za.mkojo za mtoto wako au kuhakikisha kuwa nyumba yako ni safi?
Wanawake na wanaume wanaochepuka kutoka kwenye mahusiano ya ndoa hawana sababu zaidi ya maamuzi ya makusudi ya kuvunja uaminifu na viapo vya ndoa.
Let's change instead of entertaining kuchepuka.
Kweli kabisa
 
Usimavyo labda ni kweli mkuu, sidhani kama ni uchafu au kutopikiwa vizuri au kukalipiwa kunawafanya wanaume watoke nje ya mahusiano yao. Wapo wanawake wanafanya hayo yote hata si kwasababu ana mme ndani bali kwa kuwa anaona ni vyema kuishi mazingira safi na kula vitu vilivyopikwa vizuri na kuongea kwa lugha nzuri na watu. Ila binadamu tuna tabia ya kutamani vitu vipya, tunashindwa kukumbuka kua unapooa si kwamba mkeo ndio mzuri pekee, ila umeamua kujinyima na umechagua mfumo huo wa maisha. Hakuna jambo lenye faida pekee, hata ndoa ina challenge zake. Hivyo kuoa sio kuwa tamaa zako za mwili zimekoma daima utatamani wanawake wengine, ila tu tunatakiwa kujinyima na kusimamia tulicho kichagua.
 
Mbona huwa sioni mafundisho ya aina hii kwa wanaume? Au ndoa ni ya mwanamke peke yake?
Kwanini mwanamke atumie affort kubwa sana kuilinda ndoa as if ni yake peke yake?

Kwanini muwafanye wanawake wajione watumwa kwa ndoa zao? Hivi yule aloambiwa atumie akili, hiyo akili aitumia wapi?

Na hii mentality inaitafuna jamii kwa kiasi kikubwa sana, kiasi kwamba wanaume wanajiona kumuoa mwanamke ni kumfanyia fadhila tu hivyo apaswa kuhakikisha anabaki humo.
Ndoa ni ya wawili, hizo effort lazima ziwe pande zote, lasivyo ni kutwanga maji kwenye kinu tu.
Aaah yani haya mafundisho wangekuwa wanapewa na hawa wenzetu, kwa kweli ndoa zingekuwa paradiso ndogo. Ila ndo hivyo, ndoa ikifanikiwa "hongereni wanandoa", ila ikifail eeeeeeh "mwanamke mjinga huvunja ndoa yake mwenyewe". Ndoa inahitaji continous efforts za wanandoa, sio mmoja yupo busy anajenga, mwingine yupo busy kubomoa.
 
Aaah yani haya mafundisho wangekuwa wanapewa na hawa wenzetu, kwa kweli ndoa zingekuwa paradiso ndogo. Ila ndo hivyo, ndoa ikifanikiwa "hongereni wanandoa", ila ikifail eeeeeeh "mwanamke ******** huvunja ndoa yake mwenyewe". Ndoa inahitaji continous efforts za wanandoa, sio mmoja yupo busy anajenga, mwingine yupo busy kubomoa.
Yaani dota acha tu, kila kitu mwanamke!! Hatuna jema kwa hawa viumbe. Ukizaa kabla ya ndoa unatukanwa mwanamke as if hiyo mimba umejipacjika mwenyewe, ndoa ikiyumba ni mwanamke, mwanaume akichepuka lawama ni mwanamke,mwanaume akiwa mlevi wa bia na vitimoto akavimbiwa na gutambi lawama ni mkewe, yaani hizi lawama sijui huwa zinawapa realieff!!!

Ule ulemavu nadhani sio wa viungo tena bali umehamia kichwani sasa.
 
Eeeh yani mwanaume anachukuliwa kama malaika, yani kila tatizo likitokea, mwanaume anaonekana ni victim tu. Akichepuka kosa sio lake, ni kosa la mkewe au la huyo mchepuko, atakuwa alitegwa tu. Nachokaga mie jamani, unakuta baba jitu zima limemrubuni housegirl likatembea naye, afu mke bila haya anampiga housegirl, na kuliacha jitu zima hovyo, si udeal na mumeo jamani khaa. Hivi nani ni victim kati yao wawili. Ila yote haya na sisi wanawake tunachangia, ndivyo tunavyowalea

Haha kweli ulemavu umehamia kichwani
 
Habari za majukumu wapendwa?

Wanawake wengi hawajui nafasi ya mume, hivyo kufanya mambo kiholela na kujikuta NDOA inaanza kuleta matatzo.

Jinsi ya kumlinda mumeo:

1. MAPISHI
Unapokua upo jikoni unaandaa chakula, ni lazima ujue kuwa anaekula ni mumeo, hivyo ni vizuri ukatumia ujuzi wako wote kuhakikisha mumeo anakula chakula kizuri. Wanawake wanapika chakula kizuri siku za sikukuu ndo anajitahidi kutumia uelewa wake wote katika kupika ili tu aonekane na majirani.
Au siku ukisikia mumeo anakuja na mgeni rafki yake alafu yamkini ni mtu mwenye cheo fulani ndo unataka upike vizuri.
KWA IYO USITAKE KUPIKA VIZURI ETI KWA SABABU KUNA MGENI AMEKUTEMBELEA BALI IWE NDO TABIA YAKO KWA MUMEO

2. USAFI
Wanawake bado hawajajua kuwa usafi ni kivutio pia kikubwa kwa mwanamume. Na kama tunavyojua kuwa usafi maana yake ni "kila kitu mahali pake"
Sasa wanawake utakuta vijiko vya chakula vipo kwenye kitanda eti kwa sababu tu ana mtoto mdogo. Au nguo za mikojo ya mtoto unaweka chini ya kitanda mpaka zinaanza kutoa harufu. USAFI NI MUHIMU SANA, IWE KWAKO MKE, AU MAZINGIRA YA NYUMBA. NA HAPA SIMAANISHI KUWA MSAFI KWA MAANA YA KUJIPODOA.

3. MANENO MAZURI
Mke ni lazma ujue maneno ya kuongea na mumeo. Maneno mazuri yatamlinda mumeo pale atakapoyasikia kwa wengine. NA HATA KAMA MUMEO HATAONYESHA KUJALI, BADO WEWE MKE UNATAKIWA KUENDELEA KUKAA KWNYE HIYO NAFASI.

Mungu akusaidie ewe mke kuitumia nafasi yako. Kama una swali katika NDOA na huwezi kuliweka hapa njoo inbox au piga simu 0788 599211, 0757 856336 kwa ushauri zaidi na maombezi au fika Kanisani kwetu Mlima wa Neema hapa Tegeta Kibo.
K2 umehama siku hizi?
 
Umesahau 'kukaa kimya'

wakati mwingine mwanamke anatakiwa tu anyamaze kiimya
ili mtu kichwa kitafakari ya maana

sio kuta tu kuongea ongea
usimkataze mwanamke kuongea, akiongea we cheka tu, akinuna mpige mabusu, ukimkataza kimoyomoyo atakua anakutukana tu.
 
usimkataze mwanamke kuongea, akiongea we cheka tu, akinuna mpige mabusu, ukimkataza kimoyomoyo atakua anakutukana tu.

Sijasema tuwakataze
nimesema wakiweza wakae kimya...
 
Wasichunguze simu za waume zao...kutongoza ni hobby kwa mwanaume.
 
Wanaume wengi hata wafanyiwe nini ni bureee michepuko IMO kwenye damu zao hawatosheki
 
Eeeh yani mwanaume anachukuliwa kama malaika, yani kila tatizo likitokea, mwanaume anaonekana ni victim tu. Akichepuka kosa sio lake, ni kosa la mkewe au la huyo mchepuko, atakuwa alitegwa tu. Nachokaga mie jamani, unakuta baba jitu zima limemrubuni housegirl likatembea naye, afu mke bila haya anampiga housegirl, na kuliacha jitu zima hovyo, si udeal na mumeo jamani khaa. Hivi nani ni victim kati yao wawili. Ila yote haya na sisi wanawake tunachangia, ndivyo tunavyowalea

Haha kweli ulemavu umehamia kichwani
Unampiga house girl au unagombana na mwanamke mwenzio as if yeye ndio aliweka commitment na wewe!! Thats bullshit!!
Kuendekeza upuuzi tu, ndio maana wanajiona wajanja.
 
Back
Top Bottom