GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 4,695
- 6,398
Mwanaharakati maarufu wa Marekani, Dr. Martin Luther King Jr. alishawahi kusema, "An idle mind is the workshop of the devil!". Mtu mmoja anisaidie kutafsiri kwa Kiswahili, tafadhali!🙏
Namna pekee ya kuiepusha akili kuwa "idle" ni kwa kuifanyisha kazi nzuri, na ili akili iweze kufanya kazi nzuri ni lazima uilishe taarifa nzuri kila siku.
Njia gani bora ya kuilisha akili ya mwanao taarifa nzuri zaidi ya vitabu vizuri?
Unaweza kumzoesha kuwa msomaji kwa kutumia njia zifuatazo:
1. Msomee kitabu kila siku mpaka atakapoweza kujisomea mwenyewe
Hili linaweza likafanyika tokea mtoto akiwa tumboni mwa mama yake. Tafuta vitabu vizuri na uanze kumsomea kwa sauti. Usifikiri kwamba haelewi. Utakachokuwa unakifanya kitakuwa kinarekodiwa kwenye akili yake, na kuchochea aina ya tabia atakayokuwa nayo maishani mwake.
Atakapozaliwa, uendelee kufanya hivyo. Mnaweza mkapeana zamu na mwenzi wako kumsomea kitabu Usiku wakati wa kulala, kwa kumsomea kwa sauti hadi asinzie.
2. Hakikisha kuna vitabu vya kutosha vya aina mbalimbali nyumbani kwako. Muhimu, vitabu hivyo viwe ni vitabu vizuri. Jihadhari na vitabu vinavyoweza kuwa hatari kwa afya ya akili ya mtoto.
3. Jijengee tabia ya kujisomea vitabu kila siku ukiwa naye. Wanasema, "like the father, like the son". Watoto wana tabia ya kuwaiga wazazi wao.
4. Mnunulie zawadi ya kitabu kila baada ya muda fulani, au wakati wa tukio fulani zuri. Kama una kawaida ya kumfanyia "birthday", usiishie tu kumlisha ngano na kuku, mpatie zawadi ya kitabu kizuri.
Ni gharama na usumbufu kufanya hivyo? Vyo vyote vile, lakini kama hiyo itamsaidia mwanao, kwa nini usifanye? Isitoshe, hautawafanyia hivyo milele. Wakishajua kusoma na kuandika, watakuwa wakijisomea wenyewe. Na itakuwa rahisi zaidi wao kufanya hivyo ikiwa ulishawazoesha tokea wakiwa watoto wachanga.
Ukiona vyaelea, ujue vimeundwa!
Unafikiri ni mbinu gani tena itakayomsaidia mtoto kuwa msomaji wa vitabu?