Samson Ernest
JF-Expert Member
- Aug 28, 2014
- 404
- 651
Shelfu imejaa vitabu vizuri ikiwemo na biblia, vimepangwa katika utaratibu mzuri.
Meza ya ofisi imejaa vitabu vikubwa vikubwa, vimepangwa vizuri na vinapendeza.
Hatua kubwa sana kwako, mtu kukumbuka kuwa na kabati/shelfu zuri la vitabu na kuvijaza ni hatua kubwa sana.
Mtu kununua vitabu mbalimbali na kuvipanga mezani kwake, hatua kubwa sana.
Swali la msingi, hivyo vitabu kwenye kabati/shelfu zuri umevisoma? Kama hujavisoma umemwekea nani? Au umewaandalia watoto wako urithi?
Mtu anaweza kupata sifa nyingi sana nzuri, akapata hongera nyingi sana kwa marafiki zake.
Hongera hizi ni za kuona vile amejaza vitabu vizuri, wanaona anavisoma na ana maarifa mengi.
Hili ninalolisema hapa sio wote wanalo, ila wapo tunanunua vitabu ila hatuvisomi, tunapewa zawadi mbalimbali za vitabu ila hatuvisomi.
Tuna vitambulisho vizuri vya kutuwezesha kuingia library, ila hatuendi kusoma vitabu.
Tabia hii imeingia hadi kwenye neno la Mungu, tuna matoleo mengi ya biblia ila hatuyasomi hadi tusikie tumepangwa kuhubiri/kufundisha neno la Mungu.
Hatuna muda wa kusoma biblia, ila tunazo biblia nzuri na kuzipanga mezani na kwenye makabati yetu ya vitabu.
Tuna muda mwingi wa kutembea kwenye mitandao mbalimbali na wengine kuchati tu, na wengine kuongea na simu masaa mengi pasipo kiasi.
Ikiwa umepiga hatua hii kubwa ya kununua vitabu mbalimbali ila hujawa na muda wa kuvisoma, Bora uvigawe kama huna muda wa kuvisoma.
Ikiwa umerudika vitabu kwenye nyumba/ofisi yako pasipo kuvisoma, uza hilo kabati na vitabu vyake vyote.
Ukiona ngumu gawia watu hivyo vitabu, ukiona na wao watakuwa na utaratibu ule ule wa kutokusoma kama wewe. Nenda library ya chuo cha dini yako, vigawe vyote.
Hiyo ndio njia sahihi, kuliko kukaa na vitabu vingi alafu huna muda wa kuvisoma, kuliko kukaa na biblia yako alafu huna muda nayo.
Nakueleza haya kukuonyesha unachofanya sio sahihi, unapaswa kujirekebisha haraka sana, kama umejisikia vibaya baada ya kusoma ujumbe huu, hakikisha unaweka utaratibu mzuri wa kusoma neno la Mungu na vitabu vingine.