Jinsi ya Kujiunga na CCJ kwa njia ya Simu

Status
Not open for further replies.

Mkuu hata mimi nina wasiwasi isijekuwa ni janja ya CCM kuwadaka wenye mawazo tofauti nao ili kupunguza kura za wapinzani. Mbona wanaifagilia sana?
 
Baada ya kikao cha bunge kilichoanza leo, wapambanaji watajitokeza kwa namna moja ama nyingine kukipigia debe CCJ! Ndiyo, Ninamaanisha haya ninayoyasema hapa!
 


Hapa cjaelewa kidogo MWaNAkiJIji ni mdau mkubwa wa CCJ?? hapa nataka nipate
huakika mana inaweza kuwa kama yale ya Mrema na his party,
 
Wazalendo wa kweli wanayoitakia mema Tanzania, wangependa kujiunga na CHADEMA; lakini kwa sababu tayari CHADEMA imekamilisha safu ya uongozi ukienda kule huwezi pata safu ya mbele au kukaribishwa jikoni, hivyo wajanja wachache ambao wanataka kutoka CCM wanaona it is only through new and young part like CCJ ndio unaweza kukaribishwa jikoni na kuruhusiwa kusali safu ya mbele.

Kuna uwezekano mkubwa sana wa CCJ kunyoofisha upinzani badala ya kuimarisha kwa kugawa kura! Ngoja tuone.

Kujiunga kwa SMS na kujitoa je? kwa SMS, kwa e-mail, kwa blog, kwa facebook etc......
 
Asnate mkuu,

Nashauri matangazo ya redio na TV kuhamasisha wengi kwenye hili.
Au kuna tatizo?

Ni wazo zuri lakini ni muhimu kufanya maamuzi fedha ziende wapi kwanza.. ni vigumu kutangaza namna hiyo wakati bado miundo mbinu ya chama haijajengwa vizuri.. sasa hivi CCJ inafanya uhakiki wa wanachama wake chenyewe kabla hakijaomba usajili wa kudumu maana kulikuwa na njama fulani ambayo imeshtukiwa..
 
Wazalendo wa kweli wanayoitakia mema Tanzania, wangependa kujiunga na CHADEMA;

Siyo lazima. Uzalendo haupimwi kwa kujiunga na Chadema au na chama kingine chochote kile cha siasa.


siyo kila mtu anayeingia kwenye siasa anataka uongozi; wenye kutaka uongozi wanajua pa kwenda... CCM..!
Kuna uwezekano mkubwa sana wa CCJ kunyoofisha upinzani badala ya kuimarisha kwa kugawa kura! Ngoja tuone.

unaandika kana kwamba upinzani tanzania ni imara; siyo jukumu la CCJ kuimarisha upinzani kama vile hilo siyo jukumu la Chadema wala CCM. NI jukumu la kila chama kujiimarisha.


Kujiunga kwa SMS na kujitoa je? kwa SMS, kwa e-mail, kwa blog, kwa facebook etc......

Siyo lazima kujitoa kwa jinsi ulivyoingia..
 
Mwanakijiji,mimi napenda sana articles zako katika Jamii forums na ktk kijarida chako,i have considered u as a MwanaJAMII forums mzalendo. ila kwa hili la kupromote CCM by Proxy i.e CCJ hapa unachanganya watu,je kama unapenda maendeleo ya tanzania kwa nini usidumishe upinzani via vyama vilivyosimama kidete katika upinzanii mfano chadema,cuf.
ni heri kuimarisha upinzani kwa njia hiyo kuliko kuudilute upinzani uliopo kwa kupromote ccj ambacho ni wapinzani feki waliokuja kuupunguza kura za wanaCCM ambao wangepigia kura upinzani.
 
SMS si anaweza kutuma hata mtu ambae si raia? How do they take care of this matter? Au ukishaenda kuchukua kadi ndiyo unaenda na vyeti vya kuzaliwa nk?
 
Strategy ya kutumia text message ni nzuri katika muda mfupi , lakini sidhani kama itaweza kukisaidia chama katika muda mrefu. Kwanza majority ya watanzania walioko vijijini hawana hizo cell phone , kwa hiyo sijui hiki Chama kina strategy gani ya kuwafikia.

Pili , kuanzisha chama cha siasa miezi sita kabla ya uchaguzi, na kutegemea kupambana na CCM, ni nija ya wazi ya kuumaliza upinzani. Kitu kilichokuwa kinatakiwa ni kuviunganisha vyama. Nadhani CCJ wanafanya exactly CCM walichokuwa wanakiitaji, nacho ni kuumaliza upinzani.

Watu waache kuweka interest zao mbele, waangalie picha kubwa !
 

Nimejaribu hayo mengine nimeshindwa and believe me I did. Lakini kwa vile si muumini wa vyama mimi ni muumini wa itikadi.

ni heri kuimarisha upinzani kwa njia hiyo kuliko kuudilute upinzani uliopo kwa kupromote ccj ambacho ni wapinzani feki waliokuja kuupunguza kura za wanaCCM ambao wangepigia kura upinzani.

wengine nao walisema vyama vya upinzani vilivyopo navyo vilikuwa ni CCM-B na hata baadaye viongozi wake waliorudi CCM walithibitisha dhana hiyo. Sasa, wakati mwingine ni bora kuunda kitu kwa jinsi unavyoona wewe kuliko kudandia maono ya watu wengine.
 

Rufiji.. kwa wakati huu chama kinatafuta usajili wa kudumu kwanza; kwa sababu mambo mengine yote yatakuja mbele ya hili. Kutafuta wanachama vijijini kuna mikakati mipya kabisa ambayo haijajaribiwa vizuri bado.. tusubiri usajili wa kudumu kwanza.



Hadi hivi sasa sielewi kwanini CCJ ilaumiwe kwa kudhoofisha upinzani kana kwamba kwa karibu miaka 15 upinzani umekomaa! Yawezekana ina lengo la kuwa chama hasa cha upinzani na hivyo ujio wake ndio utaimarisha upinzani sasa.
Watu waache kuweka interest zao mbele, waangalie picha kubwa !
[/QUOTE]

Ni kweli, hata hivyo kwa wengine picha kubwa kwao ni kuwa kila mtu awe Chadema, CUF, au TLP.. na nje ya hapo haieleweki.. sijui kama hiyo ni picha kubwa..
 
Any idea kuhusu uwezekano wa kupata usajili kabla ya uchaguzi na kuwa je chama kitashiriki kwenye mchakato! Siyo watu wajiunge halafu chama haieleweki kama kina mtu anayegombea urais!
 
Duh.hiii ndo raha ya Mawasiliano, Hii ni hatua nzuri.Lakini mie nasitakujiunga sbb sijaelewa Muundo wa hiki chama.hata katiba yake hatujaiona.Leteni katiba yenu hapa JF, ili tupate wasaa wa kuzijua Sera zenu.
 
Mkuu nashukuru kwa maelezo ya namna ya kujiunga na chama kipya. Mimi ninaomba msaada kwa machache.

1. Chama hiki kipya kinasimamia sera gani?

2. CCJ ina imani na malengo gani?

3. Kwa ambao hawako ndani ya nchi kwa sasa, wafanyeje ili nao waweze kujiunga na CCJ?

Inawezekana baadhi ya maswali yangu hapo juu yameshawahi kujibiwa hapa jamvini siku za nyuma. Ila naomba univumilie na kunipa majibu, kwani sijawahi kuyapata.
 
CCJ zao la waraka wa kikatoliki kuwa macho wenye kupenda nchi yetu...maaskofu wana makazi yao vatican wakishawasha moto na kuwagawa they quit..

Hili ni angalizo..angalia kwa makini safu yao kwa wenye akili...
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…