Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,474
- 39,987
- Thread starter
- #41
Mkuu nashukuru kwa maelezo ya namna ya kujiunga na chama kipya. Mimi ninaomba msaada kwa machache.
1. Chama hiki kipya kinasimamia sera gani?
2. CCJ ina imani na malengo gani?
3. Kwa ambao hawako ndani ya nchi kwa sasa, wafanyeje ili nao waweze kujiunga na CCJ?
Inawezekana baadhi ya maswali yangu hapo juu yameshawahi kujibiwa hapa jamvini siku za nyuma. Ila naomba univumilie na kunipa majibu, kwani sijawahi kuyapata.
Recta.. sasa hivi CCJ ina katiba na uongozi wa muda; Nimeamua kuambatanisha tena Katiba hiyo hapa japo ilishawekwa tayari.. nimeweka kwenye posti ya kwanza. Suala la sera sasa hivi kuna timu ya kimataifa ambayo inaandika sera na pamoja na hivyo platform ya kitaifa ya uchaguzi pamoja na kuangalia muundo wa CCJ.. Kila kitu kikiwa tayari na usajili wa muda ukipatikana kama tunavyotarajia CCJ kitakuwa ni chama pekee nchini ambacho sera, muundo na itikadi yake inaelekea kuharakisha mabadiliko tunayoyataka ili tuweze kurudisha taifa katika misingi yake na mikononi mwa wananchi.