Jinsi ya kuishi na boss mjinga mjinga

Jinsi ya kuishi na boss mjinga mjinga

Umetisha mkuu wangu.....umefikiria nini mpaka iandike hivi.....hahahaaaaaaaa kwa viongozi hawa your tips are paramount to my success.....
 
Hamna kazi ngumu kama kufanya kazi chini ya boss mjinga mjinga hasa uwe umemzidi elimu. Wanakuaga hovyo sana hata ufanyeje kazi vizuri yeye atakua anajistukia tu na kuona kama unataka kumzidi ili uchukue nafasi yake.. Na asilimia kubwa ya mabosi uchwara hawashauriki. Ukimshauri yeye anajenga bifu na kuanza kukuona mchawi kwamba unamfundisha kazi. Tabu sana..!!
Well said.
 
Wanaojipendekaza pendekeza kwenye hii awamu ni wale wenye nyeti feki,kwa taarifa tu uhakiki unaanza upya na kiama chako kiko njiani.
 
Natumaini mko salama mkizidi kulisongesha japo duh usawa mbovu huu, hatukawii kutumbuana ili tuonekane na sisi tupo tupo.

Napenda kuwapa hizi tips chache za kuweza kuishi kwa amani na hawa mabosi kazi wa kidjitali wasiojua kazi zao.

1.Kumbuka kutimiza wajibu wako na hata wake bila kinyongo.

2.Msifiesifie kuwa unajisikia raha sana kufanya kazi chini yake.

3.Mzibie mapengo ya ujinga wake.

4.Bila kutaja jina la mtu, mwambie kuna watu wanamroga lakini wewe utahakikisha anabakia hapo kwani babu yako ni fundi wa huo utaalam.

5.Kama ni mlevi hakikisha kila mara wageni hasa Madiwani na Mkurugenzi anapokuja unamtetea sana kuwa jana mmefanya kazi mpaka usiku mnene na sasa ameenda kuoga, maana ulimuacha kazini.

6.Kama ni mzinzi hakikisha michepuko yake haigongani kazini kwa kumshtua mapema.

7.Hata akiwa hajapendeza mwambie pamba zimemkaa vizuri mno.

8.Chekacheka naye hata kama unahisi kutapika.

Ukifanya hivi kila fursa atakupa.
hiyo namba 8 unawashauri watu wa jinsia gani? mimi kama mwanaume nitachekachekaje na mwanaume mwenzangu hata nikijaribu kuigiza tu nitashindwa aisee. nafikiri kuishi na boss wa aina hiyo wewe kuwa mtenda kazi mzuri hadi aamini wewe usipokuwepo mambo yataenda kombo tu, na uonyeshe msimamo wako, limitation zako yeye mwenyewe ajue kuwa wewe sio mjinga akikuzingia unaweza kumuumiza vilevile. kiufupi akuone ni mtu wa faida akikupoteza atajuta...basi.
 
Huo utafiti wako nakupa mia mia.nmekaa na mabosi wa ivyo sna ....dawa yao ndo io tu.utaenjoy kazi kwa amani ya bwana
 
Natumaini mko salama mkizidi kulisongesha japo duh usawa mbovu huu, hatukawii kutumbuana ili tuonekane na sisi tupo tupo.

Napenda kuwapa hizi tips chache za kuweza kuishi kwa amani na hawa mabosi kazi wa kidjitali wasiojua kazi zao.

1.Kumbuka kutimiza wajibu wako na hata wake bila kinyongo.

2.Msifiesifie kuwa unajisikia raha sana kufanya kazi chini yake.

3.Mzibie mapengo ya ujinga wake.

4.Bila kutaja jina la mtu, mwambie kuna watu wanamroga lakini wewe utahakikisha anabakia hapo kwani babu yako ni fundi wa huo utaalam.

5.Kama ni mlevi hakikisha kila mara wageni hasa Madiwani na Mkurugenzi anapokuja unamtetea sana kuwa jana mmefanya kazi mpaka usiku mnene na sasa ameenda kuoga, maana ulimuacha kazini.

6.Kama ni mzinzi hakikisha michepuko yake haigongani kazini kwa kumshtua mapema.

7.Hata akiwa hajapendeza mwambie pamba zimemkaa vizuri mno.

8.Chekacheka naye hata kama unahisi kutapika.

Ukifanya hivi kila fursa atakupa.
Ujinga huo mim Siuwezi yaan hua siwez kuchekacheka na Wajinga
KWANG "BLACK IS BLACK NA WHITE IS WHITE"
 
Back
Top Bottom