Mwanamke ukimwambia ni mzuri na ukampa furaha anakuwa Mzuri

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,900
MWANAMKE UKIMWAMBIA NI MZURI NA UKAMPA FURAHA ANAKUWA MZURI.

Anaandika, Robert Heriel
Mastermind.

Ukitaka Mkeo au Mpenzi wako anone, awe pisikali iliyonyooka mpaka Sisi wanaume wengine tumtolee udenda, Kwa maana hiyo ndio Raha ya kuwa na MKE. Sio unakuwa na MKE amekondeana, umemchosha, ananuka, yaani hakuna hata anayemtamani. Sasa huyo ni mke au mjane. Kipimo cha Kwanza Kwa mwanaume ni kumhudumia Mkewe. Yaani ukitaka kujua Fulani ni Mwanaume wewe kaangalie familia yake.
Mtazame Mkewe, kisha Watoto alafu majibu utayapata.

Huwezi jiita mwanaume Wakati unashindwa kumtunza Mkeo. Hakuna mwanaume WA Aina hiyo.

Mwanamke yeyote ambaye utamuona Mbaya au havutii basi elewa hapo kosa nila mumewe. Kwa Sababu Wanawake wanaonekana Wazuri wote wanatunzwa.

Mwanamke anahitaji Furaha Wakati mwanaume anahitaji Utulivu yaani Amani. Nimesemaje? Ukiweza kuifikia furaha ya mwanamke lazima akuheshimu na kukupenda. Nimesemaje?

Nimesema;

1. Msifie Mkeo ni mzuri naye atakuwa mzuri.
Elewa kuwa Mwanamke Saikolojia Yao inategemea zaidi kile wanachokisikia hasa Kwa Watu muhimu kama Mume. Msifie Mkeo. Mtazamo wa Mkeo unajengwa Kwa Yale atakayoyasikia Kutoka kwako.

2. Mtunze Mkeo
a) Matunzo huanzia kwenye Hisia, hakikisha Mkeo au Mchumba wako anahisia na wewe na hapotezi hisia na wewe. Mfurahishe, mchekeshe, mtanie, kuwa mshikaji wake, mshauri, mfariji wake, Mwalimu, director wake, mfanye kama Binti yako.
Mpe mapenzi yote. Hakikisha Ajue yupo pekeake, na haitokuja kutokea ukamuacha. Mpe kujiamini. Mwanamke anahitaji Security. Haya mpe Uhakika wa kihisia.
Onyesha jinsi unavyofurahia penzi lake. Mwambie ni mtamu na uoneshe hivyo. Sio ukimaliza unashindwa hata kutoa Sifa.
Dekeza toto Hilo, petipeti, kumbatia toto Hilo. Wanawake wanapenda hayo. Usijifanye huna Akili au Mwanaume mjingamjinga.

Matunzo ya kihisia ndio namba moja. Mwanamke akiwa stable kihisia na kujua unampenda na akawa comfortable na wewe. Anakuwa na Amani. Utashangaa ananenepa na kunawiri licha ya kuwa mnamaisha ya kawaida.

b) Matunzo ya kimwili.
Hapa tunamaanisha chakula, mavazi, malazi, mafuta na urembo mwingine.
Usimfanyie hivyo Mkeo. Usimtese hivyo Mkeo. Hakikisha Mkeo anakuvutia, sio jukumu la Mkeo kuhakikisha anakuvutia. Ni jukumu lako kumhudumia ili akuvutie vile utakavyo. Sio useme oooh! MKE wangu tangu amejifungua hanivutii ilhali humtunzi! Wee mwehu nini? Akuvutie mara ngapi Wakati ulimuoa? Mnunulie mavazi mazuri hata ya bei ya kawaida, msukishe Mkeo, mnunulie mafuta mazuri mtoto Mkeo ngozi inawiri. Sio ngozi imemparama, mikono migumu kama jiwe la kusugulia magaga, MKE ananuka kisa kumpa mikazi mingi isiyo na Mbele wala Nyuma.
Usimchoshe Mkeo.
Mrahisishie maisha Mkeo uone utamu WA Dunia.
Rahisisha kazi za nyumbani zisimtoe Mkeo jasho. MKE hatakiwi Kutoka jasho, yeye sio mwanaume bhana, mnataka Mtibeli aseme mpaka lini muelewe?

Nunua Mashine za kurahisha kazi. Tupo Duniani kuishi. Mfanye Mkeo ajione anaishi.
Alafu asipokuwa mzuri niite Mbwa.

Mkeo afanye kazi zisizohitaji nguvu, siziomchosha Mwili. Kama ni biashara asimamie biashara, Vijana tupo? Hvyo ndivyo Watibeli hufanya.

3. Mfanye akuamini.
Unashikwaje na SMS mjinga wewe! Unakamatwaje kijinga wewe! Mbona wengine hatukamatwi?
Mwaminishe yupo pekeake. Mwambie siku akikuacha akununulie jeneza maana atakuwa amepuliza filimbi ya mwisho kumaliza Maisha yako. Mwambie bila yeye huwezi ishi. Hata kama sio kweli Ila chezesha domo lako Hilo, Kuwa mwanasanaa.
Mwambie unahisi umekula limbwata la jinni Katarina. Mwambie alichokufanya huoni wakukunasua.
Waponde Wanawake wengine na jifanye kama unawaona kama vikatuni.

Mwambie hata akikuruhusu kuoa au ku-cheat bado utakataa tuu Kwa sababu penzi lake limekupofusha na huoni wala kusikia wengine.

Mpe akaunti zako zote mwambie zote ni zake. Mwambie hujui nini kimetokea kwenye Maisha yako. Mwambie uliapa hutokuja kumpa Mwanamke akaunti zako na namba za Siri za akaunti za simu na benk lakini hujui nini kimetokea kwake ukampa.

Huku kama hujiamini, unaweza ukawa na akaunti zingine za siri na asizijue.
Cheza na Akili yake, cheza na hisia zake. Akilala Usiku cheza na ndoto zake. Yaani unaishi naye Kwa Akili.

4. Nawe Vaa upendeze.
Sio umvalishe alafu wewe uwe mchafu mchafu. Nyuka pamba, nyoa vizuri, nukia., Ongea kijentromen. Tembea kitasha, usizubae zubae.

Mwanamke akishakuwa na furaha lazima uzuri wake ujidhihirishe hata kama ulikuwa umejificha. Nazungumzia uzuri wa kimaumbile.

Lakini Ka humpi furaha hata kama alikuwa ni mzuri, basi uzuri wake lazima ujifiche na kufifia.

Taikon nimemaliza, mwenye swali rukhusa kuuliza.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Back
Top Bottom