Jinsi ya kuishi na boss mjinga mjinga

Jinsi ya kuishi na boss mjinga mjinga

Hamna kazi ngumu kama kufanya kazi chini ya boss mjinga mjinga hasa uwe umemzidi elimu. Wanakuaga hovyo sana hata ufanyeje kazi vizuri yeye atakua anajistukia tu na kuona kama unataka kumzidi ili uchukue nafasi yake.. Na asilimia kubwa ya mabosi uchwara hawashauriki. Ukimshauri yeye anajenga bifu na kuanza kukuona mchawi kwamba unamfundisha kazi. Tabu sana..!!
Mbona kama unamsema Mzee flani#tusipangiane
 
Hamna kazi ngumu kama kufanya kazi chini ya boss mjinga mjinga hasa uwe umemzidi elimu. Wanakuaga hovyo sana hata ufanyeje kazi vizuri yeye atakua anajistukia tu na kuona kama unataka kumzidi ili uchukue nafasi yake.. Na asilimia kubwa ya mabosi uchwara hawashauriki. Ukimshauri yeye anajenga bifu na kuanza kukuona mchawi kwamba unamfundisha kazi. Tabu sana..!!
Hapo ndiyo no 2 inapohusika.
 
Umasikini kitu kibaya sana. Unaweza kumfanya mtu ajivue utu wake na kuwa malaya wa tabia kwa hofu za kijinga.
 
Hujamsaidia chochote boss Bali unazidi kumuangamiza.
Timiza wajibu wa kazi zako tu na kama kumsaidia kazi msaidie tu.
 
Natumaini mko salama mkizidi kulisongesha japo duh usawa mbovu huu, hatukawii kutumbuana ili tuonekane na sisi tupo tupo.

Napenda kuwapa hizi tips chache za kuweza kuishi kwa amani na hawa mabosi kazi wa kidjitali wasiojua kazi zao.

1.Kumbuka kutimiza wajibu wako na hata wake bila kinyongo.

2.Msifiesifie kuwa unajisikia raha sana kufanya kazi chini yake.

3.Mzibie mapengo ya ujinga wake.

4.Bila kutaja jina la mtu, mwambie kuna watu wanamroga lakini wewe utahakikisha anabakia hapo kwani babu yako ni fundi wa huo utaalam.

5.Kama ni mlevi hakikisha kila mara wageni hasa Madiwani na Mkurugenzi anapokuja unamtetea sana kuwa jana mmefanya kazi mpaka usiku mnene na sasa ameenda kuoga, maana ulimuacha kazini.

6.Kama ni mzinzi hakikisha michepuko yake haigongani kazini kwa kumshtua mapema.

7.Hata akiwa hajapendeza mwambie pamba zimemkaa vizuri mno.

8.Chekacheka naye hata kama unahisi kutapika.

Ukifanya hivi kila fursa atakupa.
Hizi ndio tabia za watumishi wa serikalini, lazima use mmbeya,ushirikina,kujipendekeza kwa boss wako ili upate favour,Mimi nilishindwa nikaamua Bora nijiajiri
 
Back
Top Bottom