Jinsi ya kuishi kwa amani nyumba ya kupanga

KikulachoChako

JF-Expert Member
Jul 21, 2013
15,525
2,000
Habari za muda huu wanajamii wenzangu....bila ya shaka, kwa neema za Mungu sote tu wazima wa afya......wenye maradhi Mungu awanyooshee mkono wa baraka......

Ni wazi wengi wetu tunaishi kwenye majumba ya kupanga au tulishawahi kuishi huko.....kwa hivyo kwa namna moja au nyingine tunafahamu kero na kadhia za nyumba za kupanga.....

Lakini pamoja na kero hizo bado kuna amani kwenye nyumba hizo.....ingawa mikwaruzano lazima iwepo......

Mbinu zifuatazo zinaweza kukusaidia kuishi kwa amani kwenye nyumba ya kupanga au chumba.........

>Tambua kuwa kulipa kodi ni jukumu lako.....
Mikwaruzano mingi baina ya mpangaji na mwenye nyumba huwa inaanzia hapa....lakini kikubwa ni suala la kuchelewesha kodi.......sikatai kuwa kuna wakati tunayumba kiuchumi.....na mambo huenda mrama......lakini vile vile unapokaa kimya hali ya kuwa unajua kuwa ikifika siku ya kufanya malipo huna hela ni kama dharau kwa mwenye mali na jambo hilo linakera......

Mfuate mapema mwenye nyumba....umueleze ugumu wako.....huku ukimuhakikishia siku chache zijazo uwe umeshamkamilishia mzigo wake......lakini vile vile ingependeza pia kuwa kwenye mazungumzo hayo uwe na cha kumuongopea.....sio maneno bali ni fedha...japo ya miezi miwili......

Nasisitiza tena kulipa kodi ni jukumu lako na wajibu wako....hivyo unapaswa kuwajibika bila ya shuruti........

>Tambua kuwa wewe ni mpangaji tu.....
Utakapo tambua hilo tangu siku unahamia hapo.....kutakufanya usijisahau katika kutekeleza majukumu ya mpangaji kama vile kulipa kodi kwa wakati kuheshimu mkataba wa pango......kuna watu baada ya kuishi miaka mingi kwenye nyumba wanajisahau kuwa wao ni wapangaji.....hivyo hupelekea kusahau wajibu wao....na kuzusha migogoro.....

>Epuka mazoea yasiyo ya lazima na mwenye nyumba......
Kufahamiana na watu kuna mipaka yake....ukaribu uliopitiliza na mwenye nyumba unakufanya unakuwa mtumwa wa mwenye...na kukufanya uondokewe na confidence ya kusimamia haki zako kama mpangaji.....wakati mwingine wenye nyumba....hutumia mazoea hayo vibaya kwa kukukopa fedha zisizo na mpangilio....ambapo atakuambia kuwa malipo mtakatana kwenye mkataba.....ambapo labda mwenye ulishaamua kuwa mwisho wa mkataba huo ungependa kubadili makazi........

>Heshimu mkataba wa pango......
Kitendo cha kukubali kulipa kodi na kuishi hapo ni maana yake ni kuwa umekubaliana na yaliyomo kwenye mkataba......pamoja na masharti mengine....ya mkataba.....hivyo basi ni wajibu wako kuheshimu huo mkataba....
Kuenda kinyume na yaliyomo kwenye mkataba maana yake utasababisha mtafaruku usio na lazima......

>Jali mambo yako
Wakati mwingine mifarakano haisababushwi na mwenye nyumba bali ni nyie wenyewe wapangaji....na hiyo inasababishwa na watu kufuatilia mambo ya wenzao....
Jali mambo yako.....fuata mambo yako.....achana na ya wenzako......
 
msemakweli2

JF-Expert Member
Jul 28, 2013
1,638

vipi mbinu za kuishi kwenye nyumba binafsi?
 
Ngongo

JF-Expert Member
Sep 20, 2008
13,740
2,000
Kama wewe ni kidume epuka kutembea na Mtoto wa mwenye nyumba,unaweza kujikuta unalazimishwa kuoa wakati haukuwa na mpango kisa wewe ni mpangaji huna mahali pengine pa kwenda.
 
Bavaria

JF-Expert Member
Jun 14, 2011
48,163
2,000
1. Usikae na mwenye nyumba sehemu moja.
2. Usitumie luku au mita moja ya maji na wapangaji wenzio.
3. Mkae sehemu ambayo ni mabachela wote.
4. Kila kitu chako hakikisha unakimalizia ndani.
5. Hakikisha wapangaji wenzako hawana mazoea na wewe.
 
KikulachoChako

JF-Expert Member
Jul 21, 2013
15,525
2,000
Maoni yako ni one sided aisee maana unatuongelea tu wapangaji unasahau wapangishaji nao ndo kero kubwa sana hasa ukute mwenye nyumba anategemea nyumba pekee kumuingizia kipato
Mimi nimegusia.....yale maeneo yanayosababisha zogo na mitafaruku baina ya mwenye nyumba na mpangaji....
 
Blaki Womani

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
11,231
2,000
upo sahihi braza mie hadi ninaondoka nilikuwa namdai mwenye nyumba yangu....Kama ni nyumba ya wapangaji wengi fuata mambo yako acha kukalia umbeya zaidi ya salamu hakuna ziada.......nimeishi nyumba ya kupanga sijawahi kugombana na wenzangu hata wakisema unaringa ipo siku wataelewa kwanini unaamua kuwa hivyo........kama unataka amani kwenye nyumba ya kupanga ishi unavyotaka wewe
 
Idofi

JF-Expert Member
Dec 14, 2010
1,998
2,000
ila wenye nyumba wengi wanajiona wafalme na masharti kibao, kama bachelor utaambiwa usiingize mwanamke, usipike kitimoto, mchana umeme unakatwa, mwenye nyumba anachangiwa pesa ya umeme na hamji kama amenunua umeme pesa yote nk bora ukajenge chumba kimoja malamba mawili
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom