Jinsi ya kufukuza mbu: Rahisi sana

Jinsi ya kufukuza mbu: Rahisi sana

Njia nzuri sana. Nyinhine hii: weka majani ya mchaichai kibunda kimoja chumbani. Mbu watahama nyumba!

Kumaliza tatizo, panda Mchaichai kama Maua kuzunguka nyumba. Matokeo yake utayapenda!
[emoji106] [emoji106] [emoji106] [emoji106] [emoji106] [emoji106] [emoji106] [emoji106] [emoji106]
 
Hiyo karafuu inatakiwa iwe nzima au hata ukiisaga ni sawa
 
Mie niliwahi kusoma humu mchai chai ukiupanda kuzunguka nyumba yako (Kwa wale wenye nyumba) basi mbu hawaisogelei nyumba yako.

Faida mpya ya mmea wa mchaichai

Habari wadau Malaria imekua janga kubwa sana kwa watoto walio chini ya miaka mitano pamoja na watu wazima.

Leo nitazungumzia namna na njia rahisi ya kufukuza mmbu ndani au karibu na wewe.

Ni njia rahisi kabisa ambayo itakuepusha na gharama kubwa unazotumia kununua dawa hizi za kupuliza na nyinginezo.

Ukifanya hivi na ukiwaelimisha wengine utaisaidia jamiii kuepukana na Malaria na kupunguza vifo vitokanavyo na malaria.

Mimi natumia njia hii rahisi na kwa gharama nafuu, Asubuhi Narudisha kwenye fridge muda wa mmbu jioni natoa na kuweka mahali husika.

MAHITAJI;
1. LIMAO/NDIMU..

2. KARAFUU...

3. Kisu

MAELEKEZO
1. KATA LIMAO NUSU/ KATIKATI
2. CHUKUA KARAFUU KISHA CHOMEKA KWENYE LIMAO KAMA PICHA ZINAVYO ONEKANA.
3. WEKA DIRISHANI/PEMBENI MWA KITANDA/CHUMBANI/CHOONI AU POPOTE PALE AMBAPO UTAPENDA KUFUKUZA MMBU.
4. ENDELA NA ZOEZI MARA KWA MARA.

NB; LIMAO LINAKAA MUDA MREFU KULIKO NDIMU. BINAFSI HUA NAPENDELEA LIMAO.

NO. 2

Njia ya nyingine ambayo ni Rahisi pia

MAHITAJI;
1. KARAFUU
2. KONYAGI/SPIRIT/TEQUILA/VINEGAR NA NYINGINEZO ZENYE TABIA YA ALCOHOL.
3. CHUPA YA KUPULIZIA/ AU YA KUHIFADHI
4. MAFUTA YA NAZI/LOTION NYEPESI SANA.

MAELEKEZO;
1. WEKA KONYAGI/SPIRIT KWENYE CHOMBO, LOWEKA KARAFUU KWENYE KONYAGI/SPIRIT

2. KOROGA HUO MCHANGANYO KWA SIKU NNE. KILA SIKU ASUBUHI NA JIONI.

3. BAADA YA SIKU NNE WEKA HUO MCHUZI WA KONYAGI/ SPIRIT KWENYE CHUPA / CHOMBO KITACHOKUFAAA .

4. CHANGANYA MAFUTA YA NAZI AU LOTION NYEPESI. TINGISHA TINGISHA TINGISHA VIZURI.

5. DAWA YAKO IKO TAYARI KWA MATUMIZI PULIZA KWENYE NGUO/ PAKA KWENYE NGOZI.

SHARE NA WENGINE.

Kijana Wenu Mpendwa,

BOB LEE SWAGGER..

View attachment 741738View attachment 741739View attachment 741740
 
Mkuu nakushukuru kwa dhamira yako hii, jana nikiwa katika kuwajibika nilitoka mitaa ya network. Baadaye niliisaka karafuu na kuipata.

Natumia fursa hii kukushukuru kwa dhati kabisa. Ahsante sana, na inafanya kazi vizuri.

Shukrani kwa mrejesho ndugu yangu. Siku ukihitaji tuwasiliane tu.

Ubarikiwe sana na nikutakie siku njema.
 
Back
Top Bottom