Jinsi ya kufukuza mbu: Rahisi sana

Jinsi ya kufukuza mbu: Rahisi sana

Lee Swagger

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2018
Posts
1,070
Reaction score
1,816
Habari wadau Malaria imekua janga kubwa sana kwa watoto walio chini ya miaka mitano pamoja na watu wazima.

Leo nitazungumzia namna na njia rahisi ya kufukuza mmbu ndani au karibu na wewe.

Ni njia rahisi kabisa ambayo itakuepusha na gharama kubwa unazotumia kununua dawa hizi za kupuliza na nyinginezo.

Ukifanya hivi na ukiwaelimisha wengine utaisaidia jamiii kuepukana na Malaria na kupunguza vifo vitokanavyo na malaria.

Mimi natumia njia hii rahisi na kwa gharama nafuu, Asubuhi Narudisha kwenye fridge muda wa mmbu jioni natoa na kuweka mahali husika.

MAHITAJI;
1. LIMAO /NDIMU..

2. KARAFUU...

3. Kisu

MAELEKEZO
1. KATA LIMAO/ NUSU/ KATIKATI
2. CHUKUA KARAFUU KISHA CHOMEKA KWENYE LIMAO KAMA PICHA ZINAVYO ONEKANA.
3. WEKA DIRISHANI/PEMBENI MWA KITANDA/CHUMBANI/CHOONI AU POPOTE PALE AMBAPO UTAPENDA KUFUKUZA MMBU.
4. ENDELA NA ZOEZI MARA KWA MARA.

NB; LIMAO LINAKAA MUDA MREFU KULIKO NDIMU. BINAFSI HUA NAPENDELEA LIMAO.

NO. 2

Njia ya nyingine ambayo ni Rahisi pia

MAHITAJI;
1. KARAFUU
2. KONYAGI/SPIRIT/TEQUILA/VINEGAR NA NYINGINEZO ZENYE TABIA YA ALCOHOL.
3. CHUPA YA KUPULIZIA/ AU YA KUHIFADHI
4. MAFUTA YA NAZI/LOTION NYEPESI SANA.

MAELEKEZO;
1. WEKA KONYAGI/SPIRIT KWENYE CHOMBO, LOWEKA KARAFUU KWENYE KONYAGI/SPIRIT

2. KOROGA HUO MCHANGANYO KWA SIKU NNE. KILA SIKU ASUBUHI NA JIONI.

3. BAADA YA SIKU NNE WEKA HUO MCHUZI WA KONYAGI/ SPIRIT KWENYE CHUPA / CHOMBO KITACHOKUFAAA .

4. CHANGANYA MAFUTA YA NAZI AU LOTION NYEPESI. TINGISHA TINGISHA TINGISHA VIZURI.

5. DAWA YAKO IKO TAYARI KWA MATUMIZI PULIZA KWENYE NGUO/ PAKA KWENYE NGOZI.

SHARE NA WENGINE.

Kijana Wenu Mpendwa,
BOB LEE SWAGGER..

1330-2T.jpg
download%20(7).jpeg
mosq.jpg
 
Good.

Pia ebu check pale kwenye "...NUNUA vitu vifuatavyo" ungebadilisha, badala ya neno hilo NUNUA tumia neno ANDAA. Maana baadhi ya watu hawanunui, wanavyo tayari.

Mchango wangu ni huo tu
Ok.
 
Rejea kichwa cha habari ndugu. (Kufukuza) Kwa lugha ya kingereza wanaita (repellant)
ivi hii dawa inapofukuza hao mbu wanaenda wapi?? Maana ni chumbani na ni usiku umelala (yumkini madirisha/mlango umefunga)

Au unatakiwa kulala mlango/madirisha wazi?

Nielewesheni nimeshatengeneza dawa hapa ila sasa jinsi ya kuset ndo nachemka.
 
Back
Top Bottom